Husika na kichwa cha habari hapo juu..
Je ni changamoto zipi umeshakutana nazo ukiwa ndani ya ndoa ama katika mahusiano zilizosababishwa na smartphone..
Binafsi nikiwa kama mtoa huduma flani, kwa wiki nashika simu za watu zaidi ya 1000, contacts list yangu Ina majina zaidi ya 15000, hili ni tatizo kubwa kwa upande wa pili( home) wateja huwa hawachagui muda wa kuwasiliana na wewe, anaweza piga hata saa nane ya usiku..inatokea sana aidha kwa nia nzuri, Ama nzuri zaidi, ama binafsi zaidi nje ya kazi Ama vyovyote vile..inafikia kipindi namba ya kazini c namba ile inayofahamika nyumbani lakini bado changamoto haziishi.