Wakati mkuu wa kaya kasema hakuna muda wa nyongeza kwa atakayechelewa bado changamoto ni nyingi hapa nitazungumzia chache:
1. Watu bado ni wengi walioko kwenye foleni na waliohudumiwa hawajapata namba na hazijulikani zitatoka lini.
2. Huduma ya nida inatolewa wilayani hivyo wananchi wanaacha shughuli za shamba kwenda kupanga foleni siku nzima na hakuna la maana wanaloambulia kwani unakuta wilaya nzima mashine ni moja au mbili tofauti na tume ya uchaguzi walikuwa na mashine kila kata tena zaidi ya moja
3. Mtandao wa NIDA uko slow sana sijui hizo server zao wamezinunua china? Sitegemei server kama chubb au LG zinaweza kuwa hivi?
4. Wakati huu wa masika barabara nyingi ni changamoto na maeneo mengine madaraja yamesombwa na maji hivyo wananchi wameamua kusema potelea mbali
5. Wananchi wanaona kazi ya namba za NIDA ni kusajili simu wanaposajili huzitupa
6. Baadhi ya familia wameamua kuwa na line moja tu ya familia badala ya zamani itakuta familia ina simu tano yaani baba, mama, watoto, dada wa kazi, mlinzi, shambaboy na kila simu ilikuwa na line mbili, sasa inabaki simu moja yenye line moja au mbili hivyo tutegemee mapato ya simu kushuka.
7. Wapo waliosajili line kwa kutumia namba za majirani au ndugu waliopata namba za NIDA hivyo zoezi kupoteza maana.
8. Wananchi wanaona hayo ni manyanyaso tu, kwani wakati wa kuandikisha wapiga kura zoezi lilifanyika kwenye kata na mitaa na mashine zilikuwepo za kutosha na zoezi hili lilichukua mwezi mmoja na kila mtu alipata kitambulisho chake pale pale.
Sasa kwanini utaratibu ule ule kwa kutumia mashine zile zile za tume ya uchaguzi au kutumia wafanyakazi wale wale wa tume ya uchaguzi kwanini haukutumika kurahisisha zoezi?