Changamoto za ndoa .

Changamoto za ndoa .

Binti zanda

Member
Joined
Sep 11, 2017
Posts
39
Reaction score
38
Mm ni msichana mw umri wa miaka 24 ni miongoni waliojaaliWaa kuolewa ndoa za mapema maana nilifunga ndoa na mume wangu nikiwa na miaka 20:mpaka sasa nimedumu kwa takriban miaka minne.

Nisiwachoshe sana niende moja kwa moja kilichonifanya nifungue huu uzi.mm na mume wangu kwa miaka hiyo minne tumeishi katika changamoto nyingi ikiwemo ugomvi wa mara kwa mara ,visirani kupigana pamoja na tabia ya ulevi za mara kwa mara na matatizo haya yote yapo upande wa mume wangu kwa sababu hata tunavyokaa vikao mara nyingi yy ndio huwa na hatia.kifupi mume wangu ni mlevi kupindukia inafika hatua mpaka hujitapikia ndani (usiombe kuona matapishi ya pombe) mkari aliyepitiliza hana muda wa kukaa nyumbani yy ni starehe mpaka usiku wa manane ingawa alishakutana na majanga mengi usiku wa manane akiwa anarudi lakin haikusaidia yy kuacha na kujirekebisha.

Imefikia hatua tulifikishana mpaka bakwata ili anipe talaka yangu maana nilihisi yamenishinda maisha ya ndoa.tukiwa na wazazi wa pande zote wakiwemo alikiri kuwa pombe ndio inayosbabisha awe na tabia zote chafu anazofanya hivyo nimsamehe atorudia tena hata kushika pombe na endapo ataishika au kuonja pombe basi hiyo iwe ndio taraka zangu tena zote tatu.tukazameheana kwa makibaliano hayo.

Alipumzika kwa muda wa mwezi mmoja baada ya hapo aliludia tena kunywa pombe kufabya fujo na kurudi usiku wa manane kama kawaida .

Sasa jamani kwa imani ya dini ya kiislam hapo kuna ndoa tena au tunapoteza muda tuu.na je kama ni taraka zinahesabika tatu kama alivyosema au nimoja nipo njia anda .naombeni mnisaidie kutatua hii changamoto kwa imani ya dini ya kiisalam ahsante.

NB:Hekima na busara zitumike katika kutoa ushauri

Ahsanteni
 
Ndoa uvumilivu mama,
Talaka sio solution alafu hiyo tabia ya ulevi ulimkuta nayo au ameanza baada ya kuingia kwenye ndoa...?
 
We bado ujakomaa kua na ndoa,.. Uwez kumudu mwanaume kwa kumlaumu,... Ajakamilika kweli, lakin kabla ya jambo kutokea kuna sababu ya ilo jambo kutokea, uyu anatumia pombe sio kwa bahati mbaya, inawezekan wewe pia unachangia, ila kwa sabab unahisi mwanaume ni kila kitu, kamwe uwez pata jawabu la maisha yako,.. Kaa na mumeo mzungumze tatizo liko wapi mlitatue, kuliko kulaumu na kupoint fingers,.. Marriage is not walking in the park
 
ninachofaham hata akisema kwa mdomo nimekuacha kuanzia leo sio mke wangu mama hiyo ni talaka tayari

na kama mliwekea hayo makubaliano hamna ndoa hapo talaka n hayo makubaliano kama mliyowekeana
 
Kuna wanawake wavumilivu mashaallah! Ningekushauri udai talaka lkn jaribu kuipigania ndoa yako kwa kutafuta dawa za asili za kuachisha mtu pombe. Mi sijui zinapatikana wapi ila naskia ziko very effective..mlengwa hatogusa teeeeenaa pombe then utaona km mtakuwa na amani basi maisha yaendelee na msahau yaliyopita!
 
Tulia kwenye ndoa yako... Jee ukichuka hiyo talaka utabaki hivyo bila kuolewa?? Na jee ukiolewa ukakuta shida zaid ya hizo utaachika tena?? Na je ikiwa shida utaendelea kuachika? Ndoa ni uvumilivuu... Na kusameheana hakuna ndoa iliyokamilika!! Tulia kwenye ndoa maana huyo ndio ulimuona ni bora kuliko wote duniani na ukaamua kuoana naye... Kumbuka viapo vyenu siku ya harusi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndoa uvumilivu mama,
Talaka sio solution alafu hiyo tabia ya ulevi ulimkuta nayo au ameanza baada ya kuingia kwenye ndoa...?
Jitahidi usome kwa umakin nilichouliza.nisingekuwa mvumilivuwiki ya kwanza tu ingenishinda ndoa lakin sasa miaka minne
 
Miaka minne tu ndoa shaghalabaghala tyr Duuh!!

time will tell
 
Poa inshu kubwa na ninachotaka kufahamu na msome kwa umakini sana hiyo paragraph ya pili kutoka mwisho .hapa sio inshu ya uvumilivu au nn tatiz lipo hapo
 
Nim
Kuna wanawake wavumilivu mashaallah! Ningekushauri udai talaka lkn jaribu kuipigania ndoa yako kwa kutafuta dawa za asili za kuachisha mtu pombe. Mi sijui zinapatikana wapi ila naskia ziko very effective..mlengwa hatogusa teeeeenaa pombe then utaona km mtakuwa na amani basi maisha yaendelee na msahau yaliyopita!
Nimeshatumia sana hizo dawa nimetumia gmitishamba na za makombe
 
Wee ndiyo unayepitia hayo magumu...

Maamuzi unyao wewe.. Kusuka au kunyoa...


Cc: mahondaw
 
Zipo bana, jaribu kuulizia humu humu jf hutatoka mtupu. Kuna mpaka waganga wa kienyeji humu, cc mshana jr hahahahaaa...
 
Back
Top Bottom