Buzi Maarufu
JF-Expert Member
- Oct 30, 2019
- 422
- 330
Katika harakati za kutafuta maisha unakutana na mwanamke, mnaanzisha mahusiano na hatimaye mnaamua kuishi pamoja kama mke na mume. Llakini kabla hamjaanza kuishi pamoja, mara moja moja ulikuwa unaenda nyumbani kwake unakula msosi na tunda na kurudi kwako.
Kwahiyo, baada ya kuamua kuishi pamoja, mwanamke anahamia kwako na vitu vyake vyote: meza, godoro n.k, na maisha yanaendelea. Baada ya mwaka mmoja mnatembelewa na mama mkwe, sasa huyo mwanamke wako anamwandalia malazi mama mkwe lakini cha kustaajabisha anamtandikia mikeka tu bila godoro; unamuuliza mbona umefanya hivyo hali ya kuwa hapa ndani kuna godoro ambalo ulikuja nalo?
Baada ya kumuuliza hivyo anakujibu: "Siwezi kumlaza mama yangu kwenye godoro ambalo wewe Rajabu na wengine mlishalala". Unamwambia hao wengine wataje kwa majina basi kama ulivyonitaja mimi, anasema "Nakwambia siwataji majina, ni wote unaofahamu nilikuwa nao"
Anakwambia hivyo wakati anajua kabisa kwamba kuna watu wake unawafahamu (wawili kazaa nao). Je, kama mwanaume utachukuwa maamuzi gani? Pia, nakuuliza wewe mwanamke unayesoma uzi huu. Je, ni sahihi kumtamkia hayo mtu wako ambaye mnaheshimiana na ameamua kuishi na wewe pamoja kwamba anajua wewe ulikuwa malaya, au ukimtamkia hivyo unakua unaashiria nini?
A: Umemchoka?
B: Unaona fahari kuwa na wanaume wengi ambao yeye mtu wako anawafahamu?