Changamoto za kupata mwenza JF

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
27,019
49,885
Sio kwamba huku wanaopost kutafuta wenza wana kasoro kwamba wamekosa wenza, huko walipo ni maisha tu mke au mume anaweza kupatikana popote pamoja na kuwepo post nyingi hapa ila imekuwa ni shida sana kupata mtu kwa upande wangu mimi nimeona changamoto zifuatazo;

Moja; Ukurupukaji na unafiki
Mtu anapost sifa za mtu ambae anazitaka mtu unajijua kabisa huna hata robo ila unaanza kumfukuzia huko ni kupotezeana muda, soma posti kwa makini kama huna acha kabisa subiri wa kufanana nae.

Mbili; Matapeli
Hawa nao wana familia zao basi tu kukusanifu ili akujue, kwani ukishamjua mtu huku unadhani unapata nini? Au utamfanya nini? Kama unajiona unajua kupeleleza sana kasaidie serikali kule kibiti mfyu.

Tatu;
Kutojipanga mtu hajajipanga kimahusiano au kindoa, posti inasema mtu anahitaji ndoa unaanza kumtafuta kumbe mipango yako ya kuoa au kuolewa hadi 2025! Subiri wakati wako ukifika ndo utafute ukiona mtu anatafuta mwenza ujue kachoka kuishi peke yake anataka mtu asap! Muache acha kumpotezea muda.

Nne
Location
Soma vizuri location ya mtafutaji mtu yupo songea anatafuta mke au mume na wewe upo chato na unajijua kabisa huwezi kuhama hata kwa winchi au yeye unajua kabisa kukufata alipo ni ndoto bado unajifanya kumfukuzia huko ni kupotezeana muda na mb pm na muda wa maongezi.

Tano
Dini
Mtu anasema kabisa dini yake na dini aitakayo unajijua kabisa wewe ni msabato bado unajilazimisha kwenda kwenye pm ya mtoto wa mtume wa saudi arabia kweli? Masalia na dini ya haki wapi na wapi?
 
Nadhani dunia ni dunia Miss Natafuta . Yaani ina mazagazaga yote. Ukijua kuwa ni dunia, tegemea yote. Kisha wewe angalia kule unakotaka kufika. Ukipigizana kelele na wanadamu, utapoteza mwelekeo. Yaani ili iwe dunia - lazima waongo wawepo, wezi, wavuta bangi, mabazazi, nk. Hapo ndipo inakuwa dunia haswa. Sasa cha kufanya, be focused --- unataka nini? Unataka 1, 2, 3. Basi shikilia hapohapo. --- ukifanya hivyo, mbona utafika tu.
 
Nadhani dunia ni dunia Miss Natafuta . Yaani ina mazagazaga yote. Ukijua kuwa ni dunia, tegemea yote. Kisha wewe angalia kule unakotaka kufika. Ukipigizana kelele na wanadamu, utapoteza mwelekeo. Yaani ili iwe dunia - lazima waongo wawepo, wezi, wavuta bangi, mabazazi, nk. Hapo ndipo inakuwa dunia haswa. Sasa cha kufanya, be focused --- unataka nini? Unataka 1, 2, 3. Basi shikilia hapohapo. --- ukifanya hivyo, mbona utafika tu.
ni kweli mkuu nashukuru kwa ushauri wakatishaji tamaa ni wengi.ila ni bora kuamini kile unachokitaka
 
Mtu unakuwa hadi unavuka umri wa kuolewa Hakuna anae kuona mtaani kwenu ni Hatari moja wapo katika maisha ila msijali na bahati yenu haikuwa mtaani kwenu ipo siku wenye Sifa na vigezo watapatikana Jitaidini kumshirikisha Mungu katika utafutaji wenu
 
msife moyo wadau, hata mm niliopoa kifaa toka humu jf, kabint kananiitaga dume la mbegu
FB_IMG_1496076189299.jpg
 
Back
Top Bottom