Changamoto za choo cha kukaa na jinsi ya kukabiliana nazo

Entreprenuare

JF-Expert Member
Aug 24, 2019
1,616
1,714
1606071155143.png

Ni dhahiri kuwa uwepo wa huduma ya choo katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu ni jambo lisilo na mjadala kwa sababu hutumika kujisitiri na kulinda afya za watu wa eneo husika.

Kwa wanaotembelea katika majengo mbalimbali hasa maeneo ya mjini, lazima utakutana na vyoo vya kisasa vya kukaa vilivyotengenezwa kwa ubunifu tofauti wa teknolojia na malighafi mbalimbali ili kumpa mtumiaji starehe na uhuru wakati ukimaliza haja zake.

Lakini upande wa pili vyoo hivyo hivyo vimekuwa ni sehemu ya maambukizi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo kibofu cha mkojo maarufu kama UTI (Urinary Tract Infection).

Huenda wewe ni umekuwa ukipatwa na UTI mara kwa mara licha ya kutibiwa lakini hujui kiini chake nini? Basi vyoo vya kukaa vinachangia kwa sehemu kubwa kusambaza ugonjwa huo kutoka mtu mmoja hadi mwingine.

Nukta inakuletea suluhisho au hatua muhimu unazopaswa kuchukua wakati ukitumia vyoo vya kukaa ili kuepuka maambukizi ya UTI:

Funika eneo la kukaa kwa kitambaa au karatasi laini
Karatasi hizo zinajulikana kama ‘Toilet seat cover’. Hii ni njia nyingine ya kuzuia bakteria kuingia mwilini kupitia njia ya mkojo. Hutumika kama huna dawa ya kusafisha eneo la kukaa au vyote kwa pamoja ili kujihakikishia ulinzi zaidi.

Baada ya kukamilisha hatua hizo, sasa kaa na maliza haja yako vizuri huku ukijiamini. Ukikamilisha mchakato wote basi nawa mikono yako kwa maji safi na sabuni ili kuondoa harufu na bakteria.

Muonekano wa vitambaa vinavyotumika kufunika eneo la kukaa ili kukupa starehehe lakini kukinga na maambukizi. Picha|Mtandao.

Hata hivyo, ipo njia nyingine ya kuvaa kifaa maalum cha kutolea haja ndogo (waterproof funnel-urinary device) ambapo kinawafaa zaidi wanawake kwa kuwawezesha kukojoa wakiwa wamesimama.

Kimetengenezwa maalum kuwakinga na maji maji ambayo yanaweza kuwa na vimelea vya magonjwa yasiwafikie sehemu za siri.

Kumbuka hizi ni hatua za awali unazoweza kuzitumia kujikinga na UTI lakini kinachotakiwa zaidi ni kuhakikisha vyoo vinakuwa visafi wakati wote.

Wataalam wa afya wanashauri kunywa maji mengi, hakikisha unakojoa kila unapojisikia kukojoa, hakikisha sehemu za siri zipo kavu na pendelea kuvaa nguo za ndani zilizotengenezwa kwa pamba, pia zenye kuacha unafasi (loose-fitting).

Hatari iliyopo ya kukaa na UTI kwa muda mrefu inaweza kukuletea matatizo ya kibofu cha mkojo na hata matatizo ya figo. Choo (pia: msala) ni mahali ambako watu hutoa kinyesi, yaani mkojo na mavi. Neno hili latumiwa pia na watu kwa kutaja kinyesi, hasa wakilenga kuepukana na majina husika.

Ni dhahiri kuwa uwepo wa huduma ya choo katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu ni jambo lisilo na mjadala kwa sababu hutumika kujisitiri na kulinda afya za watu wa eneo husika.

Kwa wanaotembelea katika majengo mbalimbali hasa maeneo ya mjini, lazima utakutana na vyoo vya kisasa vya kukaa vilivyotengenezwa kwa ubunifu tofauti wa teknolojia na malighafi mbalimbali ili kumpa mtumiaji starehe na uhuru wakati ukimaliza haja zake.

Lakini upande wa pili vyoo hivyo hivyo vimekuwa ni sehemu ya maambukizi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo kibofu cha mkojo maarufu kama UTI (Urinary Tract Infection).

Huenda wewe ni umekuwa ukipatwa na UTI mara kwa mara licha ya kutibiwa lakini hujui kiini chake nini? Basi vyoo vya kukaa vinachangia kwa sehemu kubwa kusambaza ugonjwa huo kutoka mtu mmoja hadi mwingine.

Nukta inakuletea suluhisho au hatua muhimu unazopaswa kuchukua wakati ukitumia vyoo vya kukaa ili kuepuka maambukizi ya UTI:

Funua mfuniko wa choo kwa kutumia karatasi laini
Kutokana na vyoo hivyo kutumika na watu wengi, ni vema kufunua mfuniko wa choo kwa kutumia karatasi laini (Tissue) ili kuzuia bakteria waliopo sehemu ya kukalia kupenya kwenye mikono yako. Hii ni hatua muhimu kukinga na UTI.

Matumizi sahihi ya choo cha kukaa yanaweza kukusaidia kujikinga dhidi ya maambuki ya njia ya mkojo. Picha|Daniel Samson.

Safisha eneo la kukaa
Kabla hujaanza kutumia choo, ni vema usafishe eneo la kukaa kwa karatasi laini iliyolowekwa kwa dawa au sabuni ya maji ya kuua wadudu (Toilet seat sanitizer). Hii itakusaidia kuua bakteria walioachwa na watu wengine wakati wakitumia choo.

Flashi kwa maji
Bakteria hawapatikani tu kwenye eneo la kukalia tu, hata kwenye maji maji yanayobaki baada ya kutumia choo. Ni kuflashi choo kabla hujatumia ili hata maji maji yakigusana na sehemu za siri hutapunguza maambukizi mwilini.

Katika maeneo mengi, maji ya kuflashi yanakuwa yamewekewa dawa ya kuua wadudu.

Karatasi hizo zinajulikana kama ‘Toilet seat cover’. Hii ni njia nyingine ya kuzuia bakteria kuingia mwilini kupitia njia ya mkojo. Hutumika kama huna dawa ya kusafisha eneo la kukaa au vyote kwa pamoja ili kujihakikishia ulinzi zaidi.

Baada ya kukamilisha hatua hizo, sasa kaa na maliza haja yako vizuri huku ukijiamini. Ukikamilisha mchakato wote basi nawa mikono yako kwa maji safi na sabuni ili kuondoa harufu na bakteria.

Muonekano wa vitambaa vinavyotumika kufunika eneo la kukaa ili kukupa starehehe lakini kukinga na maambukizi. Picha|Mtandao.

Hata hivyo, ipo njia nyingine ya kuvaa kifaa maalum cha kutolea haja ndogo (waterproof funnel-urinary device) ambapo kinawafaa zaidi wanawake kwa kuwawezesha kukojoa wakiwa wamesimama.

Kimetengenezwa maalum kuwakinga na maji maji ambayo yanaweza kuwa na vimelea vya magonjwa yasiwafikie sehemu za siri.

Kumbuka hizi ni hatua za awali unazoweza kuzitumia kujikinga na UTI lakini kinachotakiwa zaidi ni kuhakikisha vyoo vinakuwa visafi wakati wote.

Wataalam wa afya wanashauri kunywa maji mengi, hakikisha unakojoa kila unapojisikia kukojoa, hakikisha sehemu za siri zipo kavu na pendelea kuvaa nguo za ndani zilizotengenezwa kwa pamba, pia zenye kuacha unafasi (loose-fitting).

Hatari iliyopo ya kukaa na UTI kwa muda mrefu inaweza kukuletea matatizo ya kibofu cha mkojo na hata matatizo ya figo.

MADHARA YA VYOO VYA KUKAA YANAPATIKANA VIPI?

Mtu anapokaa misuli yake inayoshikiria kihifadhi kinyesi hua imebana nusu kwahiyo kuzuia tendo la kuondoa kinyesi chote.

kama picha ya kwanza inavoonyesha, mtu anapokua amechuchumaa misuli yake hua inakua imeachia kabisa hivo kuruhusu.

kinyesi kutoka kwa wepesi zaidi na kutoka chote.

Baada ya mmeng'enyo wa chakula chakula upita kwenye utumbo mdogo ambapo ufyonzwa na kuingia kwenye mfumo wa damu,chakula ambacho hakipati nafasi ya kufyonzwa uendelea na safari mpaka kwenye utumbo mkubwa ambako uko maji na madini ufyonzwa na kuingizwa kwenye mfumo wa damu, chakula hiki kinachobaki kikiwa na kias kidogo cha maji upelekwa kwenye kihifadhi kinyesi kwa jina la kimombo rectum na hapo kihifadhi kinyesi kinapojaa basi mtu ujisikia kubanwa na haja.

Hii yote ni bado haijaeleza madhara yanatokea vipi vya matumizi ya vyoo vya kukaa na haya ndo majibu ya jinsi gani madhara yanamfika mtu. Mtu anapokaa kwenye choo njia yake ya kihifadhi kinyesi hua imebanwa kiasi kwa hiyo hua hatoi kinyesi chote wakati wa kujisadia hali hii uchangiwa kutokujikunja vya kutosha na kuweka presha kwenye mfuko huo.

Kwa hali hii misuli inayoshikiria kihifadhi kinyesi kua imelegezwa nusu tu ya jinsi inavotakiwa iwe imelegezwa. Lakini mtu anapochuchumaa, hukunja eneo hili kwa nyuzi za kutosha kuruhusu misuli (sphincter muscles) hiyo kulegea vya kutosha na kurahisisha kinyesi chote kutoka nje na hivo kukidhi haja nzima.

Mdau aeleza jinsi anavyokichukulia choo cha kukaa

Wakuu!

Binafsi mimi hivi vyoo vya kukaa, huwa sivielewi kabisa, juzi niliingia kwenye ofisi fulani hivi, sasa tumbo likanishika, daaaah kuingia Toi, nakuta choo cha kukaa,

Aisee, honestly nilipata shida sana kukitumia, ilinichukua kama dk 5, ndio nikapata position nzuri ya kuachia mizigo, ila sio position ya kukaa.

Sikupenda nikae kabisa pale kwenye sink, Kwa sababu

1. Ule ubaridi wa pale juu ya sink
2. Mikojo iliyopo juu ya lile sink,
3. Halafu hau enjoy kabisa, yani unaona kama utajinyea vile. Yani shida tupu.

Hivi vyoo, sio salama kabisa kiafya:

Michango ya wadau mbalimbali kuhusu choo cha kukaa
Mkuu ustaarabu ndiyo changamoto kubwa kwenye matumizi ya hivi vyoo!​

Ukishashusha, jitawadhe kisha flash na ukague kinu kwa umakini.

Tumia Toilet Paper ama tissue kukaushia maji maji yaliyopo juu ya 'siti'.

Ukiisha kuflash pia huwa kuna mabaki yanayosomeka kwenye kuta za mzunguko wa ndani, hivyo tumia brash ndogo ku clear.

Sasa tatizo wengine wakishamaliza anaflash haraka haraka bila kukagua then anaondoka, hapo lazima takataka za mabaki yako hazitakosa, lazima mtumiaji mwingine akute tu dosari.

Hakuna choo kinachostiri binadamu wenye umri mkubwa na vilema kama vyoo vya kukaa!

Na ukishavizoea imetoka hiyo, kwako kuchuchumaa itakuwa ni muhali baba.
 
Ukipata shida ya miguu ndo utaelewa umuhimu wake....kwangu natumia cha kukaa. Ikitokea nikaenda cha kuchuchumaa huko nje shida ya miguu kuuma nitakayoipata hapo si mchezo....na hapo bado sina tatizo la magoti au nyonga.

Hicho cha kukaa unatumia mwenyewe?
 
Hata uki-flashi, uchafu hauendi wote! Nashauri kiwe tu kwenye master room ili kitumiwe na watu wawili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom