KERO Changamoto ya Stendi ya daladala Kigamboni Ferry

KERO Changamoto ya Stendi ya daladala Kigamboni Ferry

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba kuwasilisha kero yangu huku nikiomba faragha yangu ilindwe, hivyo sipendi kutajwa au kujulikana kuwa mimi ndiye mtoa taarifa hii.

Mimi ni mkazi wa Kigamboni, eneo la Geza Ulole. Kumekuwa na changamoto kubwa ya usafiri kwa watumiaji wa vyombo vya umma hususan majira ya jioni hadi usiku katika njia ya Ferry kuelekea Cheka. Hali hii mara nyingi husababisha wananchi kupata tabu kubwa ya usafiri au kulazimika kulipa nauli kubwa kuliko kawaida.

Kumekuwa na tabia ya baadhi ya madereva wa daladala kufika katika kituo na kuegesha magari yao kwa muda wakidai kuwa yana hitilafu au hayaendi, lakini baada ya muda hupandisha nauli au kusababisha wananchi kugombania usafiri. Kitendo hiki kinawaathiri sana wananchi wa kawaida pamoja na wanafunzi wanaotegemea usafiri huo kwa shughuli zao za kila siku.

Aidha, kuna changamoto kubwa katika stendi ya daladala ya Kigamboni Ferry. Hususan kipindi cha mvua, eneo hilo hujaa tope na kuwa kero kubwa kwa watumiaji wa stendi hiyo.

Naomba mamlaka husika ichunguze hali hii na kuchukua hatua stahiki. Pia ningependa kujua ni nani anayenufaika na tabia hii ya baadhi ya madereva kujipangia nauli au kuunda mazingira yanayowafanya wananchi kuteseka au kugombania usafiri, ilhali magari mengi hupita katika njia hiyo.

Naomba mtusaidie kupaza sauti ili ziifilie mamlaka husika ili kuboresha huduma ya usafiri na kuondoa usumbufu kwa wananchi.

Asanteni.
 
Hii kero inapaswa kufika haraka kunakohusika na ifanyiwe kazi accordingly! Hiyo stand hizo changamoto ni za kitambo sana
 
Back
Top Bottom