Changamoto ya Mawakala kutolipwa kamisheni

Acceptable

Member
Oct 7, 2020
34
125
Habari wakuu.

Kuna changamoto ambayo mawakala wa huduma za kifedha kama vile M-pesa, Tigo pesa, Airtel money, Halopesa na T-Pesa wanazopitia hasa katika upande wa kufanya miamala. Lakini tatizo lipo sana upande wa M-pesa.

Nikiri kwamba kufanya miamala ni biashara kama biashara zingine duniani ambazo zinahitaji mtu apate faida ili aendelee kufanya biashara hiyo. Inapotokea mtu hapati faida basi biashara yake itakufa.

Kumekuwa na tahadhari kutoka mitandao ya simu hasa Vodacom (M-Pesa) kwamba wakala ukimuwekea pesa mtu ambae yupo mbali hautalipwa kamisheni yako ya muamala huo. Hii inaweza kuwa sawa kwasababu za kibiashara lakini kwa mawakala hili ni tatizo kwasababu mtu anaweza kudanganya kuwa anaweka pesa kwenye simu yake kumbe anamtumia mtu wa mkoa mwingine tofauti na alipo (Kumbuka huwezi kumwambia mteja lete simu yako hapa nione kama SMS ya muamala unaingia kwako). Mwisho wa siku hii inakuwa imekula kwako wewe wakala kwa kukosa kamisheni yako.

Nini kifanyike?

Makampuni haya ya simu yatengeneze mfumo (Automatic Location Detection) ambao utawawezesha mawakala kupewa WARNING wakati wanaweka pesa kwa mteja kama yuko mbali simu ikutahadhalishe kwamba "mtu unaemuwekea hela yupo mbali na eneo lako hivyo hautalipwa kamisheni yako, kuendelea bonyeza labda "1" kusitisha muamala bonyeza "2".

Hii itasaidia kuwapatia kamisheni zinazostahili mawakala wanaowasaidia kuwafikishia huduma karibu na wananchi.

NAOMBA TUSAIDIE KUFIKISHA UJUMBE HUU SEHEMU HUSIKA.

ASANTE
 
marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
13,654
2,000

Achana na vodacom shughulika na makampuni yanayomtengenezea mteja unafuu wa maisha hali inabana
 
mvaa viatu

JF-Expert Member
Nov 6, 2017
280
500

Vitu vyengine ni ushamba tu! Benk unaweka fedha hata kama unaemuekea yupo shimoni tena kwa mawakala,hawa wamitandao masharti yakiwa mengi pigeni chini,tumia benk.wanacholenga wao uweke ktk simu ya aliekuja kukupa fedha ili amtumie yeye wamkate na yakumtumia kisha mpokeaji anapotaka kuitoa wamkate tena
 
darubin ya mbao

JF-Expert Member
Aug 3, 2016
942
1,000
Vitu vyengine ni ushamba tu! Benk unaweka fedha hata kama unaemuekea yupo shimoni tena kwa mawakala,hawa wamitandao masharti yakiwa mengi pigeni chini,tumia benk.wanacholenga wao uweke ktk simu ya aliekuja kukupa fedha ili amtumie yeye wamkate na yakumtumia kisha mpokeaji anapotaka kuitoa wamkate tena
Ndio hivyo na sisi wateja tumestuka kukatwa mara mbilimbili na gharama zenyewe mpaka pesa ifiki unakuta 8-10% ni makato

sasa dawa yao ni kushika namba kichwani na kutiririka huku ukiangalia angalia simu yako kama mtu anaesubiri kupigiwa kisha unaondoka zako
 
Santos06

JF-Expert Member
Mar 11, 2019
710
500
Habari wakuu.

Kuna changamoto ambayo mawakala wa huduma za kifedha kama vile M-pesa, Tigo pesa, Airtel money, Halopesa na T-Pesa wanazopitia hasa katika upande wa kufanya miamala. Lakini tatizo lipo sana upande wa M-pesa.

Nikiri kwamba kufanya miamala ni biashara kama biashara zingine duniani ambazo zinahitaji mtu apate faida ili aendelee kufanya biashara hiyo. Inapotokea mtu hapati faida basi biashara yake itakufa.

Kumekuwa na tahadhari kutoka mitandao ya simu hasa Vodacom (M-Pesa) kwamba wakala ukimuwekea pesa mtu ambae yupo mbali hautalipwa kamisheni yako ya muamala huo. Hii inaweza kuwa sawa kwasababu za kibiashara lakini kwa mawakala hili ni tatizo kwasababu mtu anaweza kudanganya kuwa anaweka pesa kwenye simu yake kumbe anamtumia mtu wa mkoa mwingine tofauti na alipo (Kumbuka huwezi kumwambia mteja lete simu yako hapa nione kama SMS ya muamala unaingia kwako). Mwisho wa siku hii inakuwa imekula kwako wewe wakala kwa kukosa kamisheni yako.

Nini kifanyike?

Makampuni haya ya simu yatengeneze mfumo (Automatic Location Detection) ambao utawawezesha mawakala kupewa WARNING wakati wanaweka pesa kwa mteja kama yuko mbali simu ikutahadhalishe kwamba "mtu unaemuwekea hela yupo mbali na eneo lako hivyo hautalipwa kamisheni yako, kuendelea bonyeza labda "1" kusitisha muamala bonyeza "2".

Hii itasaidia kuwapatia kamisheni zinazostahili mawakala wanaowasaidia kuwafikishia huduma karibu na wananchi.

NAOMBA TUSAIDIE KUFIKISHA UJUMBE HUU SEHEMU HUSIKA.

ASANTE
ni wizi
 
Lihove2

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
1,238

Hovyo kabisa hii .yaani mtu aliyoko mbali asitumiwe hela na wakala moja kwa moja sababu ni nini sasa,wizi au? yaani uingize kwako halafu utume tena,ili wakupige charge.hapa ndiyo wizi unapoanzia.
 
Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
1,160
2,000
Ni kwamba hulipwi commission kwa hiyo transaction 1 au zote kwa mwezi husika au milele hawalipi??

Dadavua!

Everyday is Saturday.............................. :cool:
 
Uzalendo Installer

JF-Expert Member
Nov 8, 2014
2,686
2,000
Tujifunze kufuata maelekezo tu...sio kulalamika...
mteja unaemtumia pesa awe na simu yake ili hata kama akisema haijafika iwe rahisi na wewe kuhakikisha...
'Training wanatoa bure, nenda branch ya voda karibu iliyo karibu yako au wakala mkuu wako atakupa training'...
hivyo ndio vigezo na masharti, uliyakubali..kwahiyo tufanye kazi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom