Changamoto ya maji ndani ya manispaa ya Shinyanga

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,615
3,909
Mamlaka ya maji safi manispaa ya Shinyanga SHUWASA tarehe 9.11.2020 iliwatangazia wakazi wa manispaa hiyo kuwa kuna ukarabati wa mabomba ambao utachukuwa mda wa Siku nne wakimaanisha kuwa kipindi cha ukarabati huo kutakuwepo ukosefu wa maji kwa wakazi wote wa manispaa hiyo jambo la kushangaza tarehe 13.11.2020 ambayo waliahidi kukamilisha ukarabati huo bado maji hayajatoka!

Kinachofanyika kwa sasa mamlaka hiyo inaendelea kutoa taarifa za uongo kuwa baadhi ya mitaa maji yanatoka jambo ambalo siyo kweli ! Kwa hali hiyo tunaomba mamlaka husika zisimamie wafanyakazi wake ili tatizo la maji liweze kutatuliwa mapema kwa sababu kwa sasa maji yamekuwa tatizo kubwa!

Ni vizuri sasa wasimamizi wakuu watoke kwenye viti vyao wakasimamie walioko chini yao ili swala hili litatuliwe haraka.
 
Mimi kwangu yamerudi kwa pressure kama yote! Vumilia mkuu hiyo mbona ni shida ya muda mfupi? Ulikuwapo miaka ya 90 wewe?
 
Back
Top Bottom