Changamoto ya Maji Mwanga kuwa historia

Changamoto ya Maji Mwanga kuwa historia

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
757
Reaction score
1,822
[https://2]

MKUU wa wilaya ya Mwanga Aaron Mbogho amewataka wananchi wilayani humo kuwa wavumilivu katika kipindi hiki chenye changamoto ya uhaba wa maji hasa maeneo ya vijijini wakati serikali ikikamilisha miradi kadhaa ya maji itakayomaliza tatizo hilo



Hayo ameyasema ofisini kwake wakati akizungumzia changamoto ya maji inayoikabili wilaya hiyo na mikakati inayofanywa na serikali ikiwemo mradi mkubwa wa kutoa maji katika bwawa la Nyumba ya Mungu wenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 300.


Amesema Mradi huo utazinufaisha pia wilaya za Same na Korogwe pamoja na vijiji 38 vilivyopo katika eneo la mradi na kwamba wananchi wapatao 438,931 watanufaika’


Mbogho amesema kuwa mradi huo umeanza kutekelezwa kwa hatua ya kwanza ya ujenzi wa miundo mbinu ya uzalishaji wa maji na unajengwa kwa awamu mbili kwa fedha za serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na BADEA na OFID na unatarajia kukamilika desemba mwaka 2019.


Mkuu huyo amesema awamu ya pili ya utekelezaji wa miradi huo itakuwa ni kusambaza maji katika vijiji 29 vilivyoko kwenye wilaya ya Same,Mwanga na Korongwe


Mradi mwingine ni uchimbaji wa visima virefu sita unaotekelezwa kwenye vijiji vya Manguo,,Kisangani,Muriti,Muruma,,Mwaniko na Vichana Ndambwe wenye thamani ya shilingi milioni 173.2 na iwapo utakamilika unawanufaisha wakazi wapatao 9900 na kwamba hadi sasa upo asilimia 75.


Akizungumzia tatizo la maji katika kata za Toloha na Kiria ambako wananchi walimlalamikia mkuu huyo mbele ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro amesema jambo hilo linafanywa kisiasa kwani tatizo la maji eneo hilo linasababishwa na hali ya ukame kutokana kupungua kwa maji yanayotoka katika msitu wa Kindoroko na kushindwa kufika katika kata hizo


Hata hivyo Mbogho alipingana na hatua ya mkuu wake wa mkoa wa Kilimanjaro , Ana Mnghwira ambaye aliagiza mabomba yafungwe ili maji yaweze kuwafikia wananchi hao kwa kueleza kuwa hatua hiyo haitakuwa suluhu ya tatizo hilo kwani itasababisha pia malalamiko kwa wananchi waliofungiwa maji kwa sababu maji hayo pia hayatakuwa na nguvu ya kuvifikia vijiji hivyo.


Katika hatua nyingine mkuu huyo amewatupia lawama wataalamu wa maji katika wilaya hiyo kwamba wamekuwa hawawasaidii wananchi kutatua kero ya maji badala yeke wamekuwa wakijifungia ofisini na kusababisha malalamiko mengi yamaji jambo ambalo alikemea na kuahidi kuwachukulia hatua kali wahandisi wote wasiotekeleza majukumu yao ipasavyo
 
Back
Top Bottom