Changamoto ya kuzidiwa kipato na mwanamke wangu jinsi ilivyobadili mwelekeo wangu wa maisha

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Tangu nipo mahusiano na huyu mwanamke nimejikuta mwelekeo wa maisha maana kuna vitu nilikuwa sivifanyi nimejikuta nafanya ili twende nae sawa kama ifuatavyo ...::

1.Nimefungua biashara ya aina tatu tofauti ili kujiongeza kipato zaidi at least ndani ya mwezi nitengeze laki 5 ambayo sawa na mshahara wa mchumba at least twende sawa

2.nilikuwa naishi kwa ndugu nimejikuta nahamia kwangu ambako sasa nimepanga maana nilikuwa najisikia vibaya nikiona mchumba wangu Anajitegemea mie bado nipo naishi kwa ndugu

3.nilikuwa mtu wa pombe viwanja sasa hivi nimejikuta nawaza maisha nataka kuwa maisha ambayo familia ya mchumba waone yes umepata mchumba

4.nilikuwaga sina tabia ya kukaa chini kuwaza maisha ya badae yatakuwaje lakini sasa hivi nawaza hatari maana

5.Hela yangu nilikuwa naipeleka sana kwenye anasa nikipata saivi naitumia kufanya vitu vya kimaendeleo

6.Elimu yangu ilikuwa diploma sasa hivi nipo degree najiongeza kielimu

Yapo mengi zaidi nakuja kusimulia
 
Only if ukizichukulia in positive way. In negative way utaona nindharau. Nampongeza mtoa post kwa jinsi alivyo fikiria in positive way
Unapokuwa na mwanamke aliye juu yako unapaswa kujifunza namna ya kulingana naye na sio kuchukulia kuwa ni dharau ..... Wanaume wengi huwa ndio tunakwsma hapa badala ya kupambambana mpk aseme nina mpambanaji ...

sent from HUAWEI
 
Tangu nipo mahusiano na huyu mwanamke nimejikuta mwelekeo wa maisha maana kuna vitu nilikuwa sivifanyi nimejikuta nafanya ili twende nae sawa kama ifuatavyo ...::

1.Nimefungua biashara ya aina tatu tofauti ili kujiongeza kipato zaidi at least ndani ya mwezi nitengeze laki 5 ambayo sawa na mshahara wa mchumba

2.nilikuwa naishi kwa ndugu nimejikuta nahamia kwangu ambako sasa nimepanga

3.nilikuwa mtu wa pombe viwanja sasa hivi nimejikuta nawaza maisha

4.nilikuwaga sina tabia ya kukaa chini kuwaza maisha ya badae yatakuwaje lakini sasa hivi nawaza hatari

5.Hela yangu nilikuwa naipeleka sana kwenye anasa nikipata saivi naitumia kufanya vitu vya kimaendeleo

6.Elimu yangu ilikuwa diploma sasa hivi nipo degree najiongeza kielimu

Yapo mengi zaidi nakuja kusimulia
Chagua tundu lissu kwa mustakali wa maisha yako ya baadae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanamke wako ana bahati sana kukupata....
Kwanza unamuadress vizuri "mwanamke wangu"
Pili unajua kupambana kama hivi unavyoelezea na kwenye ule uzi wako mwingine

Mwenyezi Mungu awajaalie mapenzi yenu yadumu
Mwanamke wangu joanah...nakusalimiaa
 
Hongera Sana, wewe ni mwanaume siyo vivulana vinavyoshindana na wanawake au kuwa marioo.
 
Upo naye kwa miaka mingapi mchumba wako, make kutoka diploma hadi degree si mchezo!

Kipato chako ni laki tano jumla, hongera!
 
Back
Top Bottom