A
Anonymous
Guest
Habari, tunaomba msaada wa kupaza sauti kuhusu changamoto ya kutolipwa mishahara inayotukabili wafanyakazi wa TBE katika miradi mbalimbali ya ujenzi wa Gridi ya Taifa ya Umeme, isipokuwa mradi wa Chalinze.
Hadi kufikia tarehe 6 bado hatujapokea mishahara yetu, licha ya utaratibu wa malipo kuwa kati ya tarehe 1 na 5 ya kila mwezi.
Kinachotushangaza zaidi ni kwamba tangu tarehe 2 tumekuwa tukipewa sababu zinazohusishwa na changamoto za kimtandao, lakini hadi sasa hakuna malipo yaliyofanyika wala ufumbuzi wa uhakika uliotolewa.
Tunaomba uongozi wa TBE pamoja na mamlaka zinazohusika zifuatilie suala hili na kuhakikisha wafanyakazi tunalipwa mishahara yetu kwa wakati. Wafanyakazi wana majukumu na mahitaji ya kila siku yanayotegemea kipato chao, hivyo ucheleweshaji huu unawaweka katika mazingira magumu.
Tunaomba suala hili liangaliwe kwa uzito na hatua zichukuliwe ili kuhakikisha haki za wafanyakazi zinazingatiwa.
Asanteni.