Changamoto ya dini katika mahusiano!!

Changamoto ya dini katika mahusiano!!

Mmmmmh
Unataka kubadili dini kwa sababu ya Papuchi? Unaweza badili lakini jibu maswali haya

1). Nani alimtongoza mwenzake
2). Nani alilipa mahari
3). Nani ni kiongozi wa mwenzake
4). Nani anamuhudumia mwenzake kiuchumi na kijamii

Ukiwa wewe ndo unahudumiwa BADILI lakini kama unahudumia KUBADILI ni dalili ya UDHALILI! Fikiri tena
 
Jadilin kwanza wenywe swala la kubadili dini ili moune Nan yuko tayar kubadili then mtaenda kwa wazaz
 
Wadau miezi kadhaa iliyopita nilionana na binti mmoja ambaye nilitokea kumuelewa, niliomba mawasiliano na akanipa! Kwa muda huo sikuweza kujua kwa haraka kama ni muislam

Hivyo niliendelea kumzoea mpaka alipokubali kuingia katika mahusiano na mimi, kifupi moyo wangu umeridhika kwake na yeye anaonesha kuwa yupo hivyo!!

Kinachokuja kuniumiza kichwa ni huu utofauti wa dini ambao nimekuja kuujua baadaye, mi ni mkristo wa kawaida wala sina misimamo yeyote katika hii dini, pia kwao ni wale waislam wa ijumaa tu!

Ninachotaka kujua ni uzoefu kwa wale waliopiti mahusiano ya namna hii, je misimamo ya wenzetu wa upande wa pili ikoje? Wanaweza ruhusu nimuoe binti yao na kila mtu abaki na misimamo yake? Je nikiamua kusilimu ni changamoto gani zilizopo huko? Je kuna uwezekano wa yeye kubalika kuja upande wangu?

Nahitaji uzoefu maana naogopa kuzama alafu mwisho wa siku nikashindwa kutoka!!

Asanteni

Ndoa za namna hiyo utasukumwa na mihemuko lakini huko mbeleni itakugharimu. Oa mtu ambaye mtakuwa dini moja, la sivyo watoto wanaenda kupoteza uelekeo. Nimeona wengi walioanza kama wewe lakini sasa hivi wanajuta.Na mara nyingi ikitokea mmekosana na mke atarudi tena kwenye dini yake.
 
A gud student is the one who do prohibited things. Ingia humo uje uwe mwalimu mzuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom