Changamoto unazopitia ziwe funzo kwa mwanao

Changamoto unazopitia ziwe funzo kwa mwanao

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
36,569
Reaction score
89,204
Habarini wakuu..?

Watu hutoka stage moja kwenda nyengine,natumai kila mzazi anapendelea kuona mtoto wake akitoka stage moja kwenda nyengine, hali hii humuimarisha mtoto kiakili.

Siku hizi kumekuwa na ongezeko kubwa la watu kujiuwa na kukata tamaa!.
Hakika si jambo zuri kabisa kwani tunatengeneza kizazi kisicho imara.
Kama mzazi yakupasa kumkalisha mtoto chini(katika umri husika) na kumwambia changamoto ulizopitia ktk maisha na jinsi ulivyopambana nazo,
hii huweza kumpa mtoto moyo wa kuendelea kuishi,kujitegemea n.k
na hapa tunakuwa tunaunda kizazi kilicho imara maana bongo zao zitakuwa zinakuwa kutokana na changamoto zinavyowakabili.
kwanza lazima umwambie kuwa kwenye maisha kuna changamoto nyingi,hivyo yampasa atumie bongo yake kuzivuka ili afike stage fulani.

Mzazi usimnyime mwanao maarifa,si kila tatizo linatatuliwa kwa bakora.
tell him/her the truth of life.
Lkn pia si lazima umwambie changamoto zote bali mwambie ambazo zitakuwa za muhimu kwake.

Elimu ya mzazi hupelekea kujitambua kwa mtoto
 
Word Up.
 
Kama sio mama yangu ningekua nimefariki mapema sana aliponieleza Na yeye aliyopitia nilijiona Nina nafuu
 
Mf kushabikia CCM na wakati huohuo huna hata pesa ya kumnunulia mtoto sukari.akikuwa na naye anakuwa kilaza tu.

swissme
 
yeah ni lazima kuwa na muda na kids,, tena muda maalum,,, kuongea nao, kucheza, kuzurura sehemu mbalimbali ili wajua na wajifunze.........
Thank you...
 
Umesema vyema mkuu,kosa kubwa ambalo wazaz hulifanya ni kuto kuwaelekeza watoto mbinu za utafutaj wa pesa..badala yake ushaur pekee wanao wapa watoto wao ni huu "Soma saana,upate A,s.Upate kazi nzuriii kwenye makampuni binafsi au ya Umma ili ulipwe mshahara mkubwa".....hii ni kwa mujibu wa Mwandshi Robert Kiyosaki
 
Pande hizi mbili matajiri na maskini wanatakiwa wajue jinsi gani ya kuwapa elimu watoto wao.
Unakuta mtoto wa tajiri anajua maisha ya luxury tu,lkn hajui kuhusu umaskini!
akifirisika anashindwa kuhandle ile hali hivyo huweza kufanya maamuzi mabaya.
Pia kwa maskini mtoto anakuwa hakanywi kuacha tabia mbaya mf.wizi n.k hali hii mtoto hukua nayo na kwa jinsi hana idea mpya ya kutafuta pesa lazima achanje hapohapo.lkn pia mtoto huyu lzm afundishwe matumizi ya mali kwa ufasaha,coz unakuta mtt wa maskini anatajirika lkn baada ya muda kupita anarudi kulekule it so sad.!

PARENT CAN CHANGE THE WORLD OF HIS/HER CHILD.
 
Back
Top Bottom