Changamoto tulionayo vijana kwa wazee ni kuongea ukweli

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
CHANGAMOTO TULIYONAYO VIJANA KWA WAZEE NI KUONGEA UKWELI

Mara zote sema ukweli, ni rahisi sana kwa sababu hutakuwa na haja ya kukumbuka mengi. Unapodanganya inabidi utunze kumbukumbu sana, ili wakati mwingine usiseme kinachopingana na ulichosema mwanzo.

Halafu pia unapodanganya, unahitaji kuendelea kudanganya zaidi, ili kufunika uongo wa kwanza, na inafika hatua huwezi kuendelea kudanganya tena na ukweli wote unajitokeza hadharani.
Kuepuka yote haya ni vyema kusema ukweli, mara zote, kwa sababu hii itakusaidia sana. Ni changamoto kubwa sana kufanya hivi kwa sababu huenda kuna mambo mengine unaona ukisema ukweli utapoteza.

Lakini ukweli ni kwamba hata ukipoteza, ni kidogo kwa sasa na baadaye mambo yatakuwa mazuri.

Sasa kuna changamoto nyingine ya kusema ukweli, na changamoto hiyo ni ujasiri wa kusema ukweli, uthubutu wa kusema ukweli.

Unaweza kuwa upo tayari kabisa kusema ukweli, ila ukakosa ujasiri wa kufanya hivyo, ukakosa uthubutu.
Na changamoto hii inakuwa kubwa zaidi pale ambapo wewe pekee ndiye unayesimamia ukweli, na wanaokuzunguka wote wanakwepa ukweli.
Ni rahisi kuzuiwa na nguvu hii ya wengine na kujikuta unaukimbia ukweli, lakini kumbuka uongo ni uongo, na kuna siku mambo yatakuwa wazi. Na hutakuwa na utetezi kwamba hukuthubutu kusimamia ukweli.

Pale unapokuwa na wasiwasi, pale unapokosa ujasiri wa kusimamia ukweli, hapo ndipo unahitaji kujikumbusha kwamba ukweli hauuliwi, bali unaweza kufichwa kwa muda. Na kadiri unapouficha ukweli ndipo unazidi kutengeneza matatizo mengine makubwa baadaye.
 
Uongo utabakia kuwa uongo tu,haka ukikaririwa miaka 800.nimejiapiza kusema ukweli hata kama nitashikiwa panga shingoni. Wengi wamepatwa na madhara kwa kusingiziwa uongo au kutolewa shuhuda za uongo.
 
Kuwa mkweli utakuwa huru tatizo letu ni hilo ndo maana watu wengi wanaishi fake life sababu ya kuhisi kudhalilika ndugu kama huna hadhi flan huna tu ya nini kuikalifisha nafsi.
 
Ukitaka kuwa mkweli kama mimi.Sio lazima kuongea kila unachokijua.Kunyamaza sometimes kutakupunguzia kusema uongo.Tatizo tunaongea sanaaa.Yaani kila kitu tunataka kuelezea au kujibu unajilazimisha hadi unadanganya.
 
Well said Galacha Maestro!!

Kwetu sisi wakristo,Ndani ya kitabu kitakatifu 'Biblia' kuna Mstari unasema hivi "Tuijue kweli,Nayo kweli itatufanya kuwa huru".Vijana wa karne hii tunazidi kupotoka sana,kabla ya kufanya,Kuongea chochote lazima tudanganye kwanza,huwa nashindwa kuelewa huu utamaduni tumeupata wapi.Ni tabia mbaya sana na aibu mtu mzima kudanganya.
Kwa upande Mwingine ni kama 'Toba',Yaani kukiri kosa ulilolifanya ili kusamehewa dhambi!! Ukikiri kosa ni rahisi sana kusaidiwa kutatua kosa ulilolifanya!

Way forward!!
Tujifunze kuwa na utamaduni wa kuongea ukweli Muda wote.Ukweli Utatufanya kuwa karibu na Mwenyezi Mungu na Kufanikiwa katika Mengi tuyafanyayo chini ya anga.
 
Vizuri kwakuwa msomaji mzuri wa neno la Mungu.
 
Back
Top Bottom