Changamoto Matokeo: Wazazi wengi wanafurahia "Pass" Hawaelewi Chochote kuhusu Merit na Distinction

PROSPER 05

JF-Expert Member
Oct 14, 2013
226
217
Baada ya Matokeo ya Kidato cha pili Kutangazwa na NECTA, wengi wa wazazi niliobahatika kuwaangalizia matokeo online, Hawakuwa na uelewa wowote na upangaji wa madaraja ya ufaulu yaani "DISTINCTIONS" Kwa wastani wa juu, "MERIT" kwa wastani wa kati na "PASS" kwa wastani wa chini.

Wengi wameonekana kufurahia zaidi unapompa taarifa kuwa mwanae amepata "PASS" na wengi wameonekana kushangaa unapomwambia kuwa mwanae ana "MERIT"


Je utaratibu huu unakanganya au Wazazi Hawajapewa Elimu ya kutosha?
 
mkuu, Wazazi wengi hawaelewi distinction, merit,wala credit ni kitu gani...

kibaya zaidi hata wanafunzi wenyewe hawajui namna ya kucalculate hayo madaraja...kwa hiyo unapomwambia mzazi mwanao amepata pass, lazima afurahi kwa kuwa hajui pass ni nini na inaanzia ngapi...
Hebu tafakari, mwanafunzi anaepata D mbili na E moja huyo ana Pass, ana GPA ya 0.3..amefaulu kwenda form three. Upuuzi mtupu

Kiukwel haya madaraja yanaua elimu sana..tuna kila sababu ya kurejeshewa zile divisions za zamani..Zamani ukimwambia mzazi, mwanao ana division 3 ama 4 anakuelewa..lakini leo hii hamna lolote

hatuwezi kupeleka mwanafunzi form three, akiwa na F 6, D 2 na E 1....halafu serikali wanatuambia ufaulu umeongezeka..kweli?
 
Huu mpangilio unaficha madudu sana, kwa haya matokeo kama yakibadilishwa kwenda mfumo uliokuwa ukitumika hapo awali yataibuka mengi,...hili ni jipu!
 
Back
Top Bottom