Utotole
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,604
- 4,259
Ameongeza kuwa, chama chao sio cha Upinzani na kinaheshimu chama kilichopo madarakani hivyo, kinaahidi kushirikiana na Chama Tawala kuenzi mazuri yanayofanywa na chama hicho.
‘’Chama chetu sio cha upinzani, tunataka nchi nyingine duniani ziwe zinakuja kujifunza Tanzania kuhusu amani na maendeleo tulionayo’’, alisema Nkembo.
Aidha, amebainisha kuwa, chama chao cha CM-TANZANIA kitatoa ajira za kudumu kwa Wanachama wake na hata kwa wale wasiokuwa wanachama ambapo kimeshaandaa Idara ya usimamizi mzuri wa huduma kwa jamii kama vile Wazee, Wajane, Walemavu pamoja na Yatima.
CM-TANZANIA ni Chama cha 23 kupokea usajili baada ya Vyama vingine vya siasa 22 vyenye usajili wa kudumu.
1. Kama si chama cha upinzani, ina maana ni chama tawala au? na anaposema wataenzi mazuri yanayofanywa na xhama kilichopo madarakani, anasemaje kuhusu yale mabaya yanayofanywa na chama kilichoko madarakani? Kama hana lengo la kukosoa chama kilichopo madarakani, kuna haja gani ya kuanzisha chama kipya? Si angejiunga na chama tawala kama kada tu na kutafuta uongozi huko? Maana kwa sasa chama kitakuwa redundant kwa kujaribu kutekeleza ilani ya chama tawala wakati hawapo serikalini.
2. Amesema watatoa ajira za kudumu kwa waanachama na wasio wanachama, mbona hajasema hizo ajira zitakazotolewa na chama hicho ni kwenye maeneo gani? Chama kina miradi tayari au ni vipi?