Chama kinachojipambanua kutetea wananchi

Maramla

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
584
644
Wanakosa umakini kisa kutawaliwa na kuendekeza ubinafsi.
Kila siku wanahubiri democracy kumbe wenyewe wala hawaijui, wala hawaitaki hiyo democracy. Iweje kwenye uchaguzi wa BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI wamepata nafasi mbili;

1) Wameshindwa kutoa Fursa kwa Idadi kubwa ya wagombea ili kuwapa wapiga kura wigo mpana wa maamuzi kama CCM na CUF walivyofanya.Wao nafasi mbili wanatoa kwa watu wawili na kutaka kulazimisha bunge kuwapitisha bila kupingwa na hivyo kuikanyaga demokrasia. AIBU!!

2)CHADEMA inaundwa na wanachama wa jinsia zote,wanawake na wanaume lakini kuna jumuia ya vijana (bavicha). Wao kwa wananchi wanahubiri Fursa Sawa kwa jinsia zote, lakini linapokuja suala la Fursa za ubunge wa afrika mashariki wanawake hawana nafasi kabisa. AIBU!

3) Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania inaundwa na nchi mbili - Tanganyika/Tanzania bara na Zanzibar /Tanzania visiwani. CCM wameweka wagombea wao kwenye uchaguzi wa bunge la Afrika mashariki kwa kuzingatia pande zote mbili,wao Chadema wanajinasibu kuwa ni chama cha kitaifa! lakini wameleta majina ya wagombea wawili,wote kutoka mkoa mmoja,wote kutoka MWANZA..... Hii tunaitaje? .. AIBU.

Uchaguzi huu unafuatiliwa kote Afrika mashariki, kwa kuwa Tanzania ni taifa kubwa na lenye ushawishi mwingi , hii ni aibu kwa chama kikuu cha upinzani, aibu,aibu aibu,aibu,aibu, aibu,aibu!!
 
Back
Top Bottom