Chama kikuu cha ushirika KDCU chapata bodi/uongozi mpya

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Chama Kikuu cha Ushirika cha wilaya za Karagwe na Kyerwa (KDCU) kimefanya uchaguzi wa wajumbe wa Bodi ya Uongozi. Hii ni baada ya Bodi ya mpito iliyokuwepo kumaliza muda wake.

Uchaguzi huo umefanyika katika mkutano mkuu wa kawaida, ambao umefanyika hapo jana katika ukumbi wa ELCT Kayanga mjini. Maudhui ya Mkutano huo yalikuwa kupitisha makadrio ya Mapato na Matumizi (Maksio) ya chama hicho pamoja na Uchaguzi wa wajumbe wa Bodi ya uongozi.

Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi ambaye ni Mrajis wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Kagera Ndg. Robert Kitambo alisoma majina ya wajumbe waliogombea na kupenya kwenye mchujo. Alisisitiza kuwa vigezo mbalimbali vilizingatiwa ikiwa pamoja na uadilifualisema mchujo ulikuwa mkali.

Majina yaliyopitishwa kugombea ni
- Ndg. Peter Clonery
- Ndg. Ndyamkama Libent
- Ndg. Witness Kabyazi
- Ndg. Rushasi
- Ndg. Ndamugoba
- Ndg. Fidoline Kasenene
- Ndg. Revelian Majune
-Ndg. Anselmi Alphonce

Kati ya wajumbe hawa 8 ilibainishwa kuwa wajumbe wanaotakiwa ni watano (Watatu kutoka wilayani Kyerwa na wiwili kutoka wilayani Karagwe.). Hii ni kutokana na gharama za kuihudumia Bodi kuwa kubwa.

Vilevile kama Mwenyekiti akitoka upande mmoja wa wilaya hizi makamu wake atokee upande mwengine.

Kura zilipigwa, kutoka wilayani Kyerwa walichaguliwa
-Ndg. Anselim Alphonce
-Revelian Majune
-Ndg. Fidoline Kasenene.

Wakati huo huo kutoka wilayani Karagwe walichaguliwa
-Ndg. Witness Kabyazi
-Ndg. Ndyamkama Libent

Katika hatua nyengine aliyepata kuwa Mwenyekiti na Makamu wa Bodi ya mpito Ndg. Theobald Muganga na Ndg. Brighton Kaijage majina yao hayakufanikiwa kupita katika mchujo.

Katika hotuba yake pamoja na neno la shukurani, mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Ndg. Shaban Lissu aliwataka viongozi hawa kuwa waaminifu na waadilifu ili kuweza kuinua tasnia ya Ushirika na zao la kahawa kwa ajili ya maslahi mapana ya wakulima.

Aidha Mkuu huyo wa wilaya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Karagwe wote walisisitiza juu ya maagizo ya serikali kuwa kahawa yote itauzwa kwa Vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) kuanzia msimu huu wa 2018/19 . Waliongeza kwa kuwataka walanguzi wote waliotoa fedha kwa walima kwa ajili ya kununua kahawa changa (BUTURA) wasahau hiyo kahawa na "kuhesabu maumivu".

Mkutano huo Mkuu ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa, viongozi wa dini, asasi za kiraia pamoja na wajumbe (wanachama).


20180306_095801.jpg
20180306_114711.jpg
 
Back
Top Bottom