Elections 2010 Chama gani kina Ilani ya uchaguzi iliyo makini?

mozze

Senior Member
Aug 27, 2010
185
28
Wale wanaoweza watuwekee ilani za vyama mbalimbali ili tulio katika forum hii tuweze kufanya uchambuzi makini, tuache ushabiki wa majukwaani.
Tukiwa na Ilani ndio tutajua mgombea gani anasema ukweli na yupi ni makini katika utendaji.
Hii pia itasaidia kujua yale yanayosemwa humu ukumbini, kama AHADI teletele za Kikwete na Chama chake au UFISADI unaosemwa na Slaa na chama chake vipi kwenye Ilani au ni usanii tu!
 
Mkuu wangu kwa mwenye akili yeyote hawezi kuunga mkono sera zozote zinazoendelea ujenzi wa jengo ambalo tayari halifai kuishi watu.Wakati CCM inasisitiza kujenga juu ya jengo ambalo tayari nguzo zake zimeweka Ufa, Chadema wanakuja na sera mpya za kubomoa nguzo za ujenzi uliopo .. Wanachokifanya CCM ni kuhadaa watu kwamba hali yetu sio mbaya hivyo, uchumi wetu sii mbaya hivyo na kwa bahati mbaya Watanzania hatuna kipimo chochote isipokuwa kulinganisha na umaskini wa maskini wengine.

Mkuu wangu, Tanzania ni sawa na meli inayozama, hakuna sera bora zaidi ya kuokoa kwanza Taifa letu na hakika ni kurudi nyuma na kutazama tumekosea wapi.

Adui wetu ni watatu.. UJINGA, MARADHI na UMASKINI pasipo kutazama vitu hivyo ni sawa na kupaka rangi mpya ktk jengo la zamani. na ndivyo CCM wameegemea sera na ilani zao. Lakini Chadema wanachotupa ni kuvunja nguzo zote zilizopo kuhusiana na ELIMU, AFYA na KILIMO kwa makusudi ya kupambana na adui zetu hao watatu pasipo kuweka matabaka baina yetu na kikubwa zaidi kuweka mbele ufanisi wa sekta zote zinazohusiana na vita hii.

Soma Ilani ya CCM utakuta kwamba wanafikiria kuelendeleza yale yale waliyoyaanza iwe ni ELIMU, AFYA na KILIMO hakuna changes isipokuwa kuweka nguvu zaidi wasijue kwamba mikakati yote ya chama iliyotangulia ktk sekta hizo ime fail wananchi kutokana na sera zao. Kwa fikra zao wanafikiria tukiweza kupata misaada zaidi ya fedha basi tatizo la elimu, Afya na umaskini utakwisha.

Wachina wanasema mfundishe maskini kuvua samaki (kesho ataenda mwenyewe kuvua samaki) na sio kumpa kipande cha samaki kila anaposikia njaa, hujamsaidia ila unamwongezea matatizo yeye na wewe mwenyewe.
 
Ilani za vyama vyote ni nzuri sasa cha msingi ni kuchagua mtu mwenye uthubutu, moyo, nia, na uwezo wa kuzitekeleza. JK kesha onesha udhaifu!!
 
Mkuu wangu kwa mwenye akili yeyote hawezi kuunga mkono sera zozote zinazoendelea ujenzi wa jengo ambalo tayari halifai kuishi watu.Wakati CCM inasisitiza kujenga juu ya jengo ambalo tayari nguzo zake zimeweka Ufa, Chadema wanakuja na sera mpya za kubomoa nguzo za ujenzi uliopo .. Wanachokifanya CCM ni kuhadaa watu kwamba hali yetu sio mbaya hivyo, uchumi wetu sii mbaya hivyo na kwa bahati mbaya Watanzania hatuna kipimo chochote isipokuwa kulinganisha na umaskini wa maskini wengine.

Mkuu wangu, Tanzania ni sawa na meli inayozama, hakuna sera bora zaidi ya kuokoa kwanza Taifa letu na hakika ni kurudi nyuma na kutazama tumekosea wap.
i
..... Lakini Chadema wanachotupa ni kuvunja nguzo zote zilizopo kuhusiana na ELIMU, AFYA na KILIMO kwa makusudi ya kupambana na adui zetu hao watatu pasipo kuweka matabaka baina yetu na kikubwa zaidi kuweka mbele ufanisi wa sekta zote zinazohusiana na vita hii.
.

Napenda kuunga mkono hoja yako Bwana Mkandara. Kama watanzania wote tungeweza kuelewa tatizo la nchi yetu katika perspective hiyo tungeweza, tena mapema kabisa kuinusuru nchi yetu.

Tatizo kubwa, wengi hatujuwi shida imekujaje na hivyo hatuwezi kujuwa itaondokaje. Kutokana na ukweli huo matatizo yetu ni mawili au matatu, ambayo ni makubwa kabisa. La kwanza ndio hilo la kukosekana kwa sera sahihi katika matatizo yetu na la pili ni kutokuwa na viongozi wenye sifa za uongozi (leadership vacuum). CCM chini ya Kikwete imepoteza sifa hizo kwasababu ya kukosa uwezo (leadership capality), njozi (vision), uzalendo (patriotism) na na dhamira (objectives) sahihi ya kuongoza watu masikini wa nchi hii. Mtizamo wao wa kutengeneza kundi dogo la watu watakaomiliki biashara na uchumi wanchi umesababisha kuikabidhi nchi mikononi mwa wageni wachache wajanja wenye nguvu ya pesa. Hawa wanamtandao wao wa kulinda masilahi yao kwa kutumia nguvu ya pesa zao kununua haki ya watu masikini sana waliokuwa wajamaa juzi..ni masikini kweli na wengi hawana elimu. Hawa watu hawawezi kujipigania dhidi ya matajiri fisadi wenye nguvu. Wanahitaji kulindwa na viongozi wao waadilifu kwa miaka mingi ijayao.

Kuna ugonjwa mwingine unaochangia katika jambo hili ni mtizamo wa udini..CCM inatizamwa kwa dini ya Kikwete (m?kiti wa Chama) na Chadema kwa dini ya Mbowe (M/Kiti wa Chama)na Slaa (Mgombea Urais). Katika hali ya namna hiyo wengi hawataweza kuangalia sera za vyama bali wataangalia mtu kwa misingi ya dini yake. Hivyo uchaguzi wa mwaka huu itakuwa kama kupigania Uislam na Ukristo vitu ambavyo havitasaidia katika kutatua tatizo la msingi ambalo Mkandara ameliita nyufa katika jengo.

Kwahiyo taizo la msingi litashindwa kutatuliwa kwa sababu mbili au tatu ambazo mimi naziweka katika mafungu ya
1. Chuki dhidi Ufisadi wa raslimali ya nchi yetu na chuki ya mafisadi dhidi ya sauti dhaifu zinazolalama dhidi ya Ufisadi
2. Chuki za Kidini, Ukristo na Uislam, zinazotaka kujitafsiri katika midani ya siasa za nchi yetu katika wakati huu ambapo hakuna mtu wa kuweza kuzikemea au kuzidhibiti
3. Ukabila (kwa kiasi flani..sio serious sana) lakini unajionesha katika lugha za kila siku sasa..mkwere, mchagga nk

Chuki hizo zitaendelea kukua kwa kasi itakayotegemea kiongozi aliyepo madarakani. Kiongozi atakayekuwa na misimamo ya kanisani au msikitini kwa siri na kitaifa kwa kudhihaki atasababisha kasi ya tatizo hilo kuzidi. Kwa hali hiyo anahitajika kiongozi atakayesimama kama alivyosimama Nyerere kuwaunganisa watu wote na kupiga vita Ufisadi, Udini na Ukabila.

Bila hilo haitachukua muda mrefu Tanzania itapigana VITA vya wenyewe kwa wenyewe. Tanzania ITAPIGANA VITA!
 
Back
Top Bottom