Ruyama
JF-Expert Member
- Sep 6, 2019
- 367
- 561
Hakika walimu tunaonewa,kunyonywa na kukandamizwa na hiki chama tokea kilipo anzishwa hadi leo.
Binafsi ninakatwa makato makubwa elfu 30 kila mwezi na hichi chama lakini kila baada ya miezi 3 ninapata gawio la elfu 5 tuu,cha ajabu May Mosi ya mwaka huu hatujapewa matisheti wamesema eti zilipelea
Mwalimu akistaafu CWT inampa mabati 15 sasa jiulize amechangia shillings ngapi aje apewe mabati 15, iko hivi walimu waliostaafu 2019 hadi leo hii hawajapewa hayo mabati 15 mwalimu huyo mstaafu amefatilia wee lakini anapigwa kiswahili njoo siku fulani hadi leo 2021 tunaelekea katikati ya mwaka hajapewa.
CWT imejenga majengo makubwa nchini kote Tanzania wameyapangisha lakini mwalimu hanufaiki hata shilling 100, viongozi wa CWT wanakaa nyumba za bure, usafiri bure,mawasiliano(vocha bure),vikao wanajilipa mapesa mengi.
Nchi hii inawalimu wengi lakini hatujawahi nufaika na hichi chama.Kuna chama kipya kilianzishwa kinaitwa CHAKAMWATA hiki chama kilikuwa mkombozi CWT kuhofia kupoteza wanachama kikapigwa marufuku kikaondolewa.
Tumeshapaza kelele nyingi mnoo juu ya hiki chama maana sio mkombozi kwa mwalimu,sijui ninani aje atuondolee haya machungu,hayati Magufuli alishindwa na alikuwa mwalimu .
Ndugu zangu nibora mjue adha tunayoipata walimu kupitia hiki chama kandamizi na cha kinyonyaji.