Chama Cha Wafanyakazi Bulyanhulu NUMET chaeleza mazungumzo kati yao na Uongozi wa Mgodi juu ya kupunguza wafanyakazi

jmchimbadhahabu

JF-Expert Member
Sep 26, 2014
218
106
Comrades Salaam.

Jana tumeanza majadiliano juu ya nia ya mwajiri ya kupunguza shughuli za uchimbaji wa madini katika mgodi wa Bulyanhulu.

Katika hotuba ya kufungua mjadala huo, Meneja Mkuu wa Bulyanhulu amesema kuwa , Bodi ya wakurugenzi wa Acacia baada ya kutathimini hali halisi ya uendeshaji wa mgodi kwa kipindi cha miezi 6 baada ya zuio la kusafirisha makinikia, imeagiza,

1. Kusitisha shughuli zote za uzalishaji mgodini na kupunguza wafanyakazi wote 1,200 walioajiriwa na BGML na wakandarasi wote wapatao 800.

Sababu za kuchukua uamuzi huo ni pamoja na ,

1. Zuio la kusafirisha makinikia limesababisha kampuni kukosa pesa ya kujiendesha.

2. Majadiliano baina ya Barrick na Serikali bado yanaendelea na Acacia kwakuwa sio sehemu ya majadiliano hawajui yataisha lini.

3. Mikataba ya kununua makinikia imevunjika kiasi kwamba hata wakiruhusiwa kusafirisha makinikia sasa hivi, hawawezi kusafirisha kwa mara moja mpaka yafanyike majadiliano mapya.

4. Mabadiliko ya sheria za sasa yameweka mazingira kuwa magumu kiasi kwamba watahitaji kufanya tathimini kuona kama bado kampuni inaweza kujiendesha kwa faida katika mazingira ya sasa.

5. Kufunga mgodi sasa hivi kutawawezesha kuwalipa wafanyakazi, wakandarasi na suppliers kuliko kusubiri kuwa declared bankrupt.

Aidha, baada ya maelekezo hayo, uongozi wa mgodini ( site management) waliamua kwamba, watabakiza Shughuli chache kama vile kuchakata taillings, na kuhifadhi machines na miundo mbinu ya underground.

Baada ya taarifa hizo Uongozi wa NUMET ulikubaliana na mwajiri kuwa , hatuwezi kuendelea na mjadala juu ya jambo hili hadi taarifa muhimu kuhusu uendeshaji mgodi zipatikane. Kampuni ilikubali kuzitoa taarifa hizo leo tarehe 07.09.2017 na mjadala rasmi baina ya NUMET na Management utaendelea tena tarehe 09.09.2017 saa nne asubuhi.

Mpaka tutakapokuwa tumepata taarifa tulizoomba na tumejiridhisha juu ya hoja ya mwajiri ndipo tutaweza kutoa msimamo wetu kama chama. Kwasasa tunaendelea kuamini kwamba ni muhimu ajira za wafanyakazi zisiguswe kwasababu wao sio sababu ya mgogoro huu.

Lakini pia tunaamini kuwa ni muhimu kampuni kujizuia kuchukua hatua zitakazo leta madhara kwa wafanyakazi katika kipindi ambacho majadiliano yanaendelea baina ya Serikali na kampuni.

Naomba kuwafahamisha.

Nicomedes Kajungu

Katibu Mkuu

NUMET
 
wasilete mchadala huko. wajibu wao sasa nikufunga mgodi waondoke ili wachoji tuingie kazini
 
Ooooops, acha noma na iwe noma,madini siyo nyanya kwamba yataoza,watakuja wengine kuchimba tu,wafanyakazi wapewe haki zao tu cha muhimu!!!!
 
Hii shida sasa,nimekimbia Dom,kuja kutafuta maisha Kahama,maana niriambiwa mzunguko wa pesa ni mkubwa,sasa mgodi ukifungwa,wapi pa kwenda,
 
Back
Top Bottom