Ng'wanza Madaso
JF-Expert Member
- Oct 21, 2008
- 2,268
- 333
Chama cha MDC cha Tsvangira chatishia kususia shughuli za serikali.
Harare:
Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai amesema chama chake cha Movement for Democratic Change -MDC- kitasusia kwa muda serikali ya Umoja wa kitaifa ya nchi hiyo.
Amesema kujitoa huko katika shughuli za baraza la mawaziri kutamalizika iwapo tu masuala mbalimbali ya kugawana madaraka kati ya MDC na chama cha ZANU PF kinachoongozwa na Rais Robert Mugabe yatakaposuluhishwa.
O ton Tsvangirai
''.. Ni haki yetu kujitoa kutoka kwa mshirika ambaye si muaminifu na si wa kutegemewa.
Kwa hali hiyo huku tukiwa serikalini, tutajiengua kufanya shughuli na chama cha ZANU PF, hasa katika shughuli za baraza la mawaziri mpaka wakati ambapo imani na heshima itakaporejeshwa tena katika uhusiano huu...''
Amesisitiza kuwa chama chao hakitajitoa katika makubaliano ya kugawana madaraka na kwamba kitarudi iwapo masharti yatatimizwa.
Kauli hiyo ya Bwana Tsvangirai imekuja siku moja tu baada ya mmoja wa wanachama waandamizi wa chama cha MDC, Roy Bennet, kuwekwa kizuizini baada ya dhamana yake juu ya mashtaka yanayomkabili ya ugaidi kufutwa.
Hata hivyo Bwana Bennet ameachiliwa huru leo kwa dhamana.
Source:http://www.dwelle.de/dw/function/0,,82228_cid_4798240,00.html