Chama cha Mawakili chatetea kusajiliwa CCJ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chama cha Mawakili chatetea kusajiliwa CCJ

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 30, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tendwa apondwa kwa kutoisajili CCJ


  na David Frank, Arusha

  CHAMA cha Mawakili Tanzania (TLS) Mkoa wa Arusha, kimemkosoa msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa kwa kukataa kukisajili Chama Cha Jamii (CCJ) kwa madai ya kutokuwa na fedha za kuhakiki wanachama wake walioko mikoani. Mawakili hao wamemtaka Tendwa kukisajili chama hicho na vyama vingine bila ubabaishaji kwa kile walichoeleza kuwa hana sababu ya msingi ya kukataa kusajili vyama kwa madai ya kutokuwa na fedha kwani kufanya hivyo ni ukiukaji wa sheria.

  Wamesema kitendo cha msajili huyo cha kuweka visingizio kadhaa vya kukisajili chama hicho kinaweza kumtia matatizoni kwa kushtakiwa kwa kutofuata sheria kwa kuwa hakuna sheria inayomtetea kwa hilo.

  Tamko lao la Mei 28 mwaka huu lililosainiwa na Mwenyekiti wa TLS Mkoa wa Arusha, Duncan Oola, limebainisha Tendwa ana wajibu wa kusajili na kutoa hati ya usajili wa kudumu kwa chama hicho na vingine vilivyowasilisha maombi na kutimiza masharti yaliyowekwa kisheria.

  "Tunachukua fursa hii kumkumbusha msajili huyo kwamba kama cheo chake kinavyojieleza chenyewe, kazi yake ya msingi kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa Sura Na. 258 (R.E. 2002) kama ilivyorekebishwa na Sheria Na 7 ya 2009 ni kusajili vyama vya siasa," inaeleza sehemu ya tamko hilo.

  Aliongeza kuwa kifungu cha 8 (5) cha sheria hiyo kinatamka wazi kwa lugha ya Kiingereza kuwa lugha iliyotumika katika kifungu hicho ni ‘shall' na siyo ‘may' kwa maana Msajili hana hiari kukubali au kukataa kusajili chama ambacho kimetimiza masharti ya kisheria ya kupewa usajili ama wa muda au wa kudumu.

  Tamko hilo liliongeza kuwa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inatakiwa kupokea na kushughulikia maombi ya usajili wa muda na wa kudumu wakati wote kwa kuwa sheria haijatenga kipindi maalumu cha kuwasilisha maombi ya kupewa usajili huo na kwamba sheria haijatamka muda ambao msajili anaruhusiwa kutopokea maombi ya usajili wa chama cha siasa.

  Tamko hilo lilisema kuwa msajili anawajibika kuahirisha shughuli zote ambazo si za msingi ili kushughulikia maombi ya usajili wa chama cha siasa ikiwa ni pamoja na maombi ya Chama Cha Jamii kwa kuwa ndiyo kazi yake ya msingi.

  Aidha, lilisema Tendwa anawajibika kuomba au kutafuta fedha za kumwezesha kutimiza majukumu yake ya msingi bila kutafuta visingizio kwani kutofanya hivyo ni kukwepa wajibu wake wa kisheria unaoweza kusababisha ashtakiwe kwa mujibu wa kifungu cha 6 cha sheria iliyotajwa hapo juu.

  Hivi karibuni vyombo vya habari vilimnukuu msajili huyo akiwaambia viongozi wa muda wa CCJ kuwa hana fedha za kuzunguka kufanya uhakiki wa wanachama wake na kwamba kwa sasa ana majukumu mengine muhimu ya kufanya.

  CHANZO: Tanzania Daima
   
 2. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Huyu msajili ni mjinga tu anatumiwa na mafisadi wa Chama cha Majambazi.
   
 3. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tatizo nokwamba Tendwa na CCJ wote wako kwenye game moja ambalo ni kuua movement. Pona yetu ni pale tutakapo wagundua mapema na kuwaachia waendelee na maigizo yao na kuendelea na harakati zetu.

  Jamani chadema mbona mko kimya na mnaacha hawa wasanii wanatuchezea hivyo? CCJ ya hawa viongozi wawili + mpendazoe leo hii karibu mwezi wa sita eti wanataka kuchukua nchi pengine ukiwaongeza na makapi mawili matatu yatakayo chunjwa na mafisadi. Wamekosa kabisa cha kusema wamebaki eti sisi tuna itikadi wamerekani walipokuwa wanamtoa baru muingeleza walikuwa na itikadi gani. Itikadi ni luxury baadaya nchi kuwa shwari ndipo unapoaanza kuwapa wanachi luxury ya kuchagua directions. Huwezi leta itikadi katika nchi hii iliyooza kama hii.

  Sasa Rwanda wanaweza kuleta itikadi siyo hii nchi ambayo asilimia karibu 70 hawana uwezo wa kufikiria sahihi.
   
 4. M

  Mundu JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hii inji hii, kila mmoja ni Mungu mtu.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  May 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  haya ni matusi kwa Watanzania; wasiokuwa na uwezo wa kufikiri ni wale ambao wanafikiria kuwa ati wakiindoa CCM madarakani tu basi matatizo yetu yataisha. Hawajui kama wanaweza kusababisha watu waililie CCM baada ya miaka michache tu.
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Hawana hela ya kusajiri chama wana hela ya kuileta timu ya mpira ya Brazil. Kweli nimeamini bora kukosa mali kuliko kukosa akili!!!
   
 7. k

  kausha Member

  #7
  May 30, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 73
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  unachekesha
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  And here lies the real danger, most likely CCM iking'oka leo itakuwa ndiyo bye bye!!!!! Chama kipya kitashika madaraka na kuwa dominant in the same old way. Na make no mistake the same pple, cadres, apologists unaowaona kwa CCM leo ndiyo hao hao utawaona kwenye chama kipya kilichotwaa madaraka wakiendeleza bootlicking.But what we actually need ni kuwa na vyama vikubwa na vyenye nguvu in such a way kimoja kikiboa kinatolewa na kuingia kingine lakini si kuua kile kilichoboa. Kwa mtindo huu ile dhana ya mpiga kura ndiye bosi inakuwa practical.

  Anywayz turudi kwa CCJ, huyu msajili ameshaanza kuendesha zile semina za sheria mpya alizotuambia????????. Maana is more than 2 wks now toka alipotoa hilo tamko which means angepita just along the famous major highways, Dar - Namanga , Dar Tunduma , Dar - Mwanza angekuwa amemaliza kuhakiki wanachama wa CCJ bara. This coming Monday angeenda Zenj and by the end of the week zoezi lingekuwa limeisha. This guy anapaswa kutambua kuwa yuko kwenye ile ofisi kutimiza wajibu wake kikatiba na siyo Ngonjera kama nazoziendeleza hivi sasa.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  May 31, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  of course.. wapo Watanzania wanaopenda kuchekacheka...
   
 10. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ukweli utabaki kuwa ukweli daima: Hivi kweli kama mngekuwa mnawaachukulia kuwa watanzania wana uwezo wa kufikiria kweli mngekuwa mnawatania hivyo. Yaani wewe na wale washikaji wawili of course plus mpendazoe watu ambao pekee mnajua itikadi katika vyama vya tanzania mnaunda chama cha kijamaa kinachofuata mlengo wa kulia na kuanza kuwavizia watu wasio na itikadi kutoka vyama vingine na kuwabatiza hiyo itikadi yenu, na mara tu wanapoingia kwenye hicho chama chenu wanakuwa conservative!

  Yes watanzania wengi ni wavivu wa kufikiri na ndiyo maana maaluki wa ccm wamekuwa wanawachezea sana. Mwambie mpendazoe arudjishe kadi ya ccm na pia aandike barua ya kujiuzuru bungeni, haitasaidia sana lakini at list itaweka kuwa mipango yenu ni ya uhakika
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Mods unganisheni hii thread, zipo mbili zingine toka jana
   
Loading...