Chama cha Mapinduzi(CCM) wamtoa machozi Eric Shigongo, wamwambia kunywa maji

Hakusaidia chama mkuu! Alifanya biashara na chama. Ni sawa tu na wale wanaopata tenda ya kushona sare za chqma n.k

Acha mhemko, tafakari, andika tena
 
Alimpigia kampeni JK, sio JPM, amfuate JK sasa..

na bado.. kwani aliombwa kupiga kampeni..? si alijipendekeza ili madili yake ya biashara afanikiwe kupitia mgongo wa CCM, mpiga dili huyooo..!!

Kwnn miaka yote asimfuate JK, tokea 2010 aje leo kulia kinafiki..

Chizi huyo.. na bado
Duh ....kumbe deni la muda mrefu sana .....ila mlipeni jamani, si mwa ccm mwenzenu?
 
Kuna taarifa kwamba katika hiyo tenda ali-quote Sh 95,000 kwa tisheti moja na Sh 50,000 kwa kofia moja, sasa kama hili ni kweli sijui kama mwenyekiti mpya ataruhusu malipo ya namna hiyo hata kama kuna mkataba!
Du hiyo tshirt ilikua na TV ?
 
Kuhusu Eric Shigongo na Kunywa maji mwanangu!

Nakumbuka siku Mh Magufuli anakutana na wafanyabiashara aliuliza kama Je kuna mfanyabiashara yeyote aliyemsaidia kuwa Rais anyooshe mkono! Ukweli hapakuwa na kidole cha mtu sio mfanyabiashara tu, na hapakutokea yeyote aliyejitokeza na kujibu wote walikaa kimya!!

Takribani Miezi kumi imepita sasa amejitokeza mfanyabiashara wa magazeti ndugu Eric Shigongo na malalamiko lukuki yakuwa amedhulumiwa pesa zake nyingi na chama cha mapinduzi (CCM)baada ya kukisaidia kwenye kipindi cha kampeni kwa mkataba angelipwa baada ya uchaguzi kumalizika...................

Badala ya kulipwa akaambiwa kunywa maji mwanangu!

Wenye akili timamu wanajiuliza kwanini siku ile ukumbini alishindwa kunyoosha mkono? ...,.......,........teeehh teeeehhh unafiki na uoga wa wafanyabiashara utatunyima kibali cha kuiona Mbingu!! Kwanini Leo ananyoosha peni badala ya kidole huu sio unafiki huu?? Huu si uoga huu?

Hivi wewe unaakili...pale uambiwe unyooshe mkono na wewe unyooshe kweli hata kama unadai....sio utaratibu huo...
 
Duh ....kumbe deni la muda mrefu sana .....ila mlipeni jamani, si mwa ccm mwenzenu?

Hapati kitu, sbb unakuta dili alipiga na costs ana triple, ili kukinyonya chama, hatuna wanachama wapiga dili sasa hivi.. si mmemsikia MWENYEKITI WETU, JPM.. wapiga dili hakuna tena.. na bado, huyu lazima anyooke tu..
 
Mkuu atalia machozi mbele ya JPM mpaka amuonee huruma ....ila naye alizida na vijarida vyake vya kuponda watu ....inakula kwake sasa......
 
ila mkuu kumbuka mh. magufuli alikutana na wafanyabishara kama rais wa nchi na si mwenyekiti wa ccm.
 
Mkuu atalia machozi mbele ya JPM mpaka amuonee huruma ....ila naye alizida na vijarida vyake vya kuponda watu ....inakula kwake sasa......

Ha haaa.. alijua akiponda UPINZANI.. CCM itamlipa, na vikanga na videla vyake.. amekuja kwa pupa CCM kuvuna fedha, alivyo kichwa maji eti anasema anaipenda CCM hadi kufa, na amekisadia sana CCM, huyu si mzima, kaja juzi tu CCCM, intruder, sasa kama anaipenda sana CCM..kwanini anakidai chama..? akina Lowassa waliwekeza mabilioni kwa mabilioni, kwa miaka na miaka, akakosa Urais, ameondoka kimyaaa kimyaaaa hata siku moja kukichafua CCM hakuna, tena husikii akikisema vibaya CCM, ndio maana mamilioni bado tunamheshimu Lowassa hadi kufa, pamoja ameondoka but ana heshima kubwa, sbb ni mtu ana moyo na roho kubwa kuliko normal human being.. ndio maana Lowassa ni tishio sana sbb ya hekima na busara zake, sio mali, bali utu wake, moyo wake na kauli zake, ndio tishio sana, sbb anaeleweka sana kwa vitendo na maneno yake, na ana hekima kubwa kupindukia, ndio maana wote CCM tunamwogopa na wengi tunampenda sana bado

Sasa huyu intruder, Eric, mvamizi mtafuta hela, msanii chizi ana mapenzi na CCM huyu..? Mpiga dili tu, wengine tuko CCM kwa miaka tuko kimyaaa, ingawa tuna misimamo unwavering.. kutetea haki na ukweli, sio fuata mkumbo.. huyu hakuna kulipa.. na akiendelea kuchafua chama, tunafilisi na kumshtaki
 
Tageti yake ilikuwa ana subili ukuu Wa wilaya sasa Siku zmekuwa nyingi ameamua afunguke sasa.
 
Kuhusu Eric Shigongo na Kunywa maji mwanangu!

Nakumbuka siku Mh Magufuli anakutana na wafanyabiashara aliuliza kama Je kuna mfanyabiashara yeyote aliyemsaidia kuwa Rais anyooshe mkono! Ukweli hapakuwa na kidole cha mtu sio mfanyabiashara tu, na hapakutokea yeyote aliyejitokeza na kujibu wote walikaa kimya!!

Takribani Miezi kumi imepita sasa amejitokeza mfanyabiashara wa magazeti ndugu Eric Shigongo na malalamiko lukuki yakuwa amedhulumiwa pesa zake nyingi na chama cha mapinduzi (CCM)baada ya kukisaidia kwenye kipindi cha kampeni kwa mkataba angelipwa baada ya uchaguzi kumalizika...................

Badala ya kulipwa akaambiwa kunywa maji mwanangu!

Wenye akili timamu wanajiuliza kwanini siku ile ukumbini alishindwa kunyoosha mkono? ...,.......,........teeehh teeeehhh unafiki na uoga wa wafanyabiashara utatunyima kibali cha kuiona Mbingu!! Kwanini Leo ananyoosha peni badala ya kidole huu sio unafiki huu?? Huu si uoga huu?
Wewe ndo haujaread btn lines

Aliandika kuwa ni kampen za Mwaka 2010
 
Back
Top Bottom