Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,194
- 4,112
Chama cha madereva wa usafirishaji kwa njia ya mtandao (Toda) kimetoa siku saba kukutana na wamiliki wa kampuni za huduma ya usafiri kwa njia ya mtandao za Uber na Taxify ili kujadiliana kuhusu changamoto zinazowakabili madereva.
Kimesema kama itashindikana kukutana na wamiliki hao watawafungulia kesi mahakamani.
Toda imetoa kauli hiyo baada ya kuibuka kwa madai kuwa wamiliki hao wanachukua asilimia kubwa katika kila safari anayofanya dereva, kushusha bei za safari kila siku bila kuzingatia gharama za usafirishaji.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Desemba 19, 2019 mwenyekiti wa Toda, Linus Chuwa amesema awali biashara hiyo ilikuwa ikivutia kampuni nyingi na kipato kilikuwa kizuri lakini kwa sasa hali ni tofauti.
“Wakati kampuni hizi zinaanza biashara nchini benki nyingi ikiwemo CRDB zilivutiwa kutoa mikopo ya magari kwa madereva ambayo walikuwa wakiilipa kwa miaka miwili lakini sasa suala hilo limekuwa gumu kutokana na bei za usafirishaji kuwa ndogo,” amesema Chuwa
Amesema wakati mwingine ni ngumu kujua dereva anavyoumia kwa kuwa kampuni hizo hazimiliki magari na baadhi ya madereva waliokopa wakishindwa kulipa madeni na magari yao kupigwa mnada.