Siyo kurithishana kwa watoto tu ndugu Chikaka Sumuni, pia wake na wachumba zetu kama ilivyo Mushumbusi na wa Dubai ambaye mpaka sasa Ndoa ya Mkuu wangu wa chama iko mashakani kama siyo kubomoka kabisa. Nadhani kwenye swala la kurithishana siyo issue ya kuzungumza Tanzania maana wapo wanoshindana wanashinda na wanaoshindwa kama ilivyoArumeru kama ni kurithishana kusingekua na kushindwa (refer Equitorial Guenea, Uganda, Malawi, Pakistani, India nk) usije ukaniambia George Bush alirithishwa, au Dr. Hussein Mwinyi au Kikwete au Godfrey Mgimwa au Nape la hasha wameshindanishwa na wakashindana sana na ndiyo maana wameshinda kwa mbinde siyo kuwekwa tu.
Jiulize vyama vya upinzani vimeanza lini Tanzania na kama vina umri wa kijana wa kuoa ama la kama Ridhiwani alikua kwenye chama tangu 1990 sijui alitumia nguvu za babaye kuwa kwenye uongozi wa chama ama la. Mi nadhani wazo zuri ni kujadili nani hasa anaihujumu nchi kwa staili uliyoitaja ya deep green, kagoda nk. Na mleta mada anachotaka kusema ni kuwa CHADEMA ni chama kinachotarjiwa kuyakimbia hayo ya uhujumu nchi lakini kiukweli viongozi nia yao ni kupata ulafi na mwisho ni kuturudisha tunakotaka kukimbia.
Tuache kuona tunapambana kichama bali tupambane kifikra mbadala na kila wazo liheshimiwe ila si lazima likubaliwe.