Wapo wapinzani wengi wa CHADEMA. Sijaona wala kusikia mwenye hoja dhaifu kama hii! Poor analysis! Bado unajaribu kuita CDM kuwa ni chama cha udini wakati kimesheheni wanachama wa dini zote? Fanya utafiti utaona! Bado unaita CDM chama cha ukanda wakati kimeenea nchi yote!
CDM inatawala mji wa Kigoma, (magharibi) Mji wa Mbeya, (Kusini) Jiji la Mwanza na Mji wa Musoma, (Kaskazini) Arusha na Moshi ( Kaskazini mashariki) Dar-es Salaam, (majimbo mawili) Katikati ya nchi (Singida na Iringa) Na sasa utafiti unaonesha kuwa kinaungwa mkono sana Mtwara na maeneo yote ya nchi! Bado unafikiri kuwa Chadema ni kama fasheni inayopita wakati CCM imepoteza mvuto kabisa mioyoni mwa watyanzania? Kimegeuka kuwa chama cha WALA NCHI badala ya Chama Cha Wajenga nchi. Watanzania hatukujua kuwa CCM kingetugeuka haraka kwa kiasi hiki.
Chama kilichokuwa na kinasema "RUSHWA NI ADUI WA HAKI, SITAPOKEA WALA KUTOA RUSHWA" kimekuwa mstari wa mbele kwa rushwa ndani ya chama na hata katika serikali yake. Chama kinawaonea aibu wala rushwa na mafisadi. Kimeishia kuwaita magamba tu basi. Hatukujua kuwa CCM kitawageuka wafanyakazi katika nchi hii haraka namna hii. Kilikuwa chama cha wakulima na wafanyakazi. Baada ya kufunga ndoa na mafisadi na wezi wa rasilimali za Watanzania kimewatupa wafanyakazi chini kabisa. Iko wapi morali ya madaktari leo.
Kafanye utafiti Mhimbili utaojionea mwenyewe! Waalimu wana mgomo baridi. Wanaofundisha darasani hata wale waliosahihisha mitihani ya kitaifa. Wala hapakuwa na haja ya kuunda tume kuchunguza kufeli kwa kidato cha nne. Kama wangelijibu sawali la "JINSI GANI TUBORESHE MASILAHI YA MSINGI YA WAALIMU NA KURUDISHA MORALI YAO?" wangepata jibu la kuiokoa elimu ya kizazi kijacho cha Watanzania. Lakini hata kule kwingine ambapo utendaji hauonekani dhahiri kama wa Walimu bado morali ya wafanyakazi ipo chini sana! CCM imewatupa.
CCM imewatupa wakulima. Mikoa ya Lindi na Mtwara wanalalamikia Korosho. Nyanda za juu Kusini wanalalamikia Pembejeo hasa mbolea! Lakini hata wakivuna, wanakatazwa kuuza mazao yao kama wanavyotaka. Kaskazini kule wakulima wanakatazwa kuuza mazao yao waliyolima wenyewe Kenya penye soko zuri na huku wauza mafuta wakiruhusiwa kupandisha bei kila uchao na kufanya maisha ya mkulima kuwa magumu.
Yako wapi yale maisha bora kwa kila Mtanzania tuliyoahidiwa na CCM? Huduma mbovu za katika vituo vya Afya, miundombinu mibovu, maji hakuna, pamoja nakuwa nchi yetu ina gesi lakini umeme unakatika ovyo, na bei yake iko juu, na VYOTE HIVI NA VINGINE CHANZO NI CCM NA SERIKALI YAKE. Kwa nini Mtanzania wa kawaida awe na sabababu ya kuipenda CCM? Naweza nisiipende CDM lakini sina sababu ya kuichukia kama ninavyochukia CCM kwa sababu haijawahi kupewa nchi na kufurunda kama CCM.
Watanzania wanayo sababu ya msingi ya kuichukia CCM iliyotawala miaka 50, na sasa kujizatiti kuingiza chama kingine madarakani tuone kama hapawezi kuwa na mabadiliko. Ni hoja dhaifu kuwa wafuasi wa CDM ni bendera fuata upepo. CCM imetutupa, inatunyayasa, inaiba rasilimali zetu, imetugawa kidini, inawaunga mkono mafisadi na wala rushwa, inawafumbia macho wale walioficha fedha Uswis, kwa ujumla haina habari na Mtanzania wa kawaida. Tumeiacha kwani ukijaribu kishika, kama wewe sio mnafiki utakuta inateleza. Haishikiki tena.