GE2025 Chama cha Kijamii (CCK): Tukichukua nchi kila mtumishi tutamjengea nyumba

GE2025 Chama cha Kijamii (CCK): Tukichukua nchi kila mtumishi tutamjengea nyumba

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Kijamii (CCK), David Daud Mwajojele, amewasili katika Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Njedengwa, Jijini Dodoma, akiwa ameambatana na mgombea wake mwenza, kwa ajili ya kuchukua fomu za kuteuliwa kugombea nafasi ya Rais na Makamu wa Rais katika Uchaguzi Mkuu 2025.

Baada ya kukabidhiwa fomu hizo na Mwenyekiti wa INEC, Jaji (Rufani) Jacobs Mwambegele, Mwajojele amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais, serikali yake itaandaa mazingira bora kwa watumishi wa umma, ikiwemo kuwajengea nyumba ili waishi maisha yenye hadhi baada ya kustaafu.

Soma Pia: Mgombea Urais wa Chama cha Kijamii (CCK) awasili kuchukua fomu INEC

Amesisitiza kuwa, hilo litasababisha wafanyakazi kutoogopa kustaafu kwa hofu ya kuishi maisha magumu.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Kijamii (CCK), David Daud Mwajojele, amewasili katika Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Njedengwa, Jijini Dodoma, akiwa ameambatana na mgombea wake mwenza, kwa ajili ya kuchukua fomu za kuteuliwa kugombea nafasi ya Rais na Makamu wa Rais katika Uchaguzi Mkuu 2025.

Baada ya kukabidhiwa fomu hizo na Mwenyekiti wa INEC, Jaji (Rufani) Jacobs Mwambegele, Mwajojele amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais, serikali yake itaandaa mazingira bora kwa watumishi wa umma, ikiwemo kuwajengea nyumba ili waishi maisha yenye hadhi baada ya kustaafu. Amesisitiza kuwa, hilo litasababisha wafanyakazi kutoogopa kustaafu kwa hofu ya kuishi maisha magumu.

CHANZO: Jambo Tv​
 
Copy and Paste:
====
Sijasikia ambaye anaahidi, kuwa ataweka mipango ya Kuiwezesha Tanzania iingie kwenye kundi la nchi zenye Uchumi wa kwanza kiuhalisia ndani ya miaka 10.
====
Kujengewa nyumba, hela watazipata wapi? Au watauza kipande cha Ardhi ya nchi yetu.? Wataje watapata wapi hela na watazirudishaje?
 
Sasa watumishi ndio wananchi pekee hadi wawe favored
 
Wanaongea chochote kwa kuwa wanajua hawapati hata asilimia moja
 
Ndugu zangu hawa jamaa wapewe nchi, wana kitu.
 
Back
Top Bottom