Chama cha CUF kiko hatarini kufutwa na Msajili wa vyama vya siasa

Good People

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
945
1,819
Anaandika Masoud Sanani.

Chama cha Wananchi (CUF) ni moja ya
vyama vikongwe vya siasa nchini ambavyo vimekuwa na maendeleo tangu kuanza kwa mfumo wa siasa wa vyama vingi nchini mwaka 1992.

Miaka ya nyuma, CUF iliwahi kuwa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania kabla ya kuondolewa hivi karibuni na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho kwa sasa ndicho kinaongoza upinzani.

Mbali na hilo, CUF ndicho chama cha siasa chenye nguvu zaidi kwa upande wa Zanzibar, katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Katika chaguzi mbalimbali zilizopita, CUF imekuwa inashinda majimbo yote ya kisiwa cha Pemba na baadhi ya majimbo ya Unguja na kukiacha Chama cha Mapinduzi (CCM)
ambacho ndicho kinachotawala kikipata baadhi ya majimbo ya kisiwa cha Unguja pekee.

Hata hivyo, CUF hivi sasa haina uwakilishi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar na mabaraza ya miji, baada ya CCM kushinda viti vyote vya uwakilishi na madiwani kutokana na chama hicho cha upinzani kukataa kushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar baada ya matokeo ya ule wa Oktoba 25, 2015 kufutwa.

Mgogoro wakomaa
Kwa sasa CUF ipo katika mgogoro mkubwa uliosababishwa na Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba ambaye alijiuzulu nafasi hiyo, lakini akaamua kurudi miezi 10 baadaye.

Kitendo hicho kimesababisha mgogoro
ambao unazidi kufukuta na iwapo
hakutakuwa na hatua za kuumaliza
unaweza kukiyumbisha zaidi chama hicho. Profesa Lipumba alijiuzulu miezi michache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 jambo ambalo lilikifanya chama hicho
kuingia katika uchaguzi mkuu bila ya kuwa na mwenyekiti.

Hakuna mwenye uhakika kwamba uamuzi wa Lipumba wakati anajiuzulu ulikuwa na lengo gani, lakini kwa hisia za baadhi ya watu ni kwamba ulilenga kukifanya chama hicho kufanya vibaya katika uchaguzi huo

Hata hivyo, CUF ambayo ilishiriki katika
uchaguzi huo ikiwa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ulioundwa na vyama vya Chadema, NCCR Mageuzi na NLD
ilifanya vizuri kuliko katika Uchaguzi Mkuu mwingine wowote ule.

Kwa upande wa Tanzania Bara, chama
hicho badala ya kupata majimbo mawili au pungufu kama ilivyokuwa katika kila uchaguzi ilipata wabunge katika majimbo 10 na kwa mara ya kwanza ikaundahalmashauri za wilaya.

Kwa upande wa Zanzibar, kabla ya matokeo kufutwa CUF ilikuwa imeshinda viti 27 vya wawakilishi waliokabidhiwa vyeti vya ushindi sawa na CCM.

Hata mgombea wa Chadema na Ukawa kwenye urais wa Muungano, Edward lowassa akiungwa mkono na CUF yenye nguvu Zanzibar, alipata kura nyingi visiwani humo kuliko mgombea wa CCM.

CUF baada ya kufanya vizuri katika
uchaguzi huo, Profesa Lipumba aliamua kurudi kwenye nafasi ya uenyekiti, jambo ambalo bila shaka yoyote ndilo limekiingiza chama hicho katika mgogoro mkubwa.

Inaelekea msomi huyo wa uchumi baada ya kugundua kuwa kujiuzulu kwake hakukuleta madhara yoyote, bali manufaa zaidi, akaamua kurudi katika nafasi hiyo na kuleta mgogoro.

CUF inapoteza mwelekeo

Katika mgogoro huu ambapo upande wa uongozi unaompinga mwanasiasa huyo kurudi madarakani ukiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad ulimfukuza uanachama, lakini naye hakukubali na sasa ametengua vyeo vya wakurugenzi wa chama.

Akiungwa mkono na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ambaye alimtambua kuwa ni mwenyekiti halali wa chama hicho, Profesa Lipumba amekifanya chama hicho kuelekea kupoteza mwelekeo. Hivi sasa CUF ambayo ina kesi mahakamani ipo katika wakati mgumu kwani ni vigumu katika mazingira waliyo nayo kuwashawishi
wanachama wapya kujiunga au kupata
wafuasi wapya hasa vijana.

Mazingira yanayoizunguka CUF ni vigumu kumshawishi mtu yeyote kujiunga nayo. Hata hivyo, inatoa mwanya mkubwa kwa wanachama wa chama hicho kujiunga na vyama vingine. Serikali inaweza kukifuta
Haieleweki dhamira ya Profesa Lipumba na mgogoro huu uliosababishwa na kurudi
kwake kwenye uongozi, lakini kuna
uwezekano kwa Serikali kukifuta chama hicho ambacho kilipata umaarufu mkubwa nchini.

Ni rahisi katika hali hiyo mgogoro ukatumia mwanya huo Serikali ikakichukulia hatua na hata kukifuta kwa madai kwamba kinatahatarisha amani na utulivu nchini. CUF itafute suluhu Kuna haja kwa chama hicho kutafakari upya na kutafuta suluhu ya kuumaliza mgogoro huo kabla ya kuleta athari kubwa kwani Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 haupo mbali.

Inabidi kujipanga upya kuondokana na
mgogoro huo ili iweze kufanya vizuri katika uchaguzi kwa upande wa Tanzania Bara ili isirejee kama miaka ya nyuma ya kupata wabunge wawili.
CUF ikiondokana na mgogoro huo itakuwa katika mazingira mazuri zaidi ya kufanya Viizuri katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, hata kama usimamizi wa uchaguzi huo utakuwa na mizengwe kiasi gani.

Kwa upande wa Zanzibar, CUF ina nguvu kubwa ambayo kwa namna yoyote ile na kwa vyovyote haiwezi kuzuilika kushinda katika majimbo kadhaa ya Unguja na Pemba.

Kwa hiyo uongozi unapaswa kutafakari na kutafuta njia ya kukiokoa chama chao na njia rahisi kuliko zote ni kusameheana na kuelewa kwamba yaliyopita si ndwele wagange yajayo.

Kutokana na mgogoro huo kuendelea
kukimong’onyoa chama hicho hadi watu waliokuwa marafiki zamani kugeuka kuwa mahasimu, pengine dawa pekee ya kumaliza mgogoro huu ingepaswa kutoka nje ya chama baada ya jitihada za ndani kuonekana kugonga mwamba.

Hata hivyo, swali la kujiuliza ni nani
atajitokeza kuifanya kazi hiyo ya kuwakabili mahasimu wawili, Profesa Lipumba na Maalim Seif na wafuasi wao ili kuwasihi wakae pamoja na kumaliza sintofahamu zao kwa ajili ya mustakabali wa chama hicho?
Katika moja ya tahariri zake, gazeti hili
liliwahi kupendekeza Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa iingilie kati na kunusuru hali ya mambo, kwa kuwa msajili ndiye mdau na mhimili mkuu wa vyama vya siasa ambaye anaweza kujivika jukumu la usimamizi kwa sura ya ulezi na kuacha kubagua au kuonekana kuwa na upande.

Mwandishi ni mwanahabari mwandamizi nchini na amefanya kazi Televisheni Zanzibar, magazeti ya Uhuru na Mzalendo,Majira na Mwananchi.

Source: Mwananchi
 
Huu ni wakati mzuri wa TLS kufanya kazi yake kwenye masuala muhimu kama haya kupindisha sheria naamini huu utakuwa mtihani muhimu sana kwa Lissu.
 
Mwandishi ni mwanahabari mwandamizi nchini na amefanya kazi Televisheni Zanzibar, magazeti ya Uhuru na Mzalendo
 
Hili ni jepesi sana likitokea wananchi wanaweza kuli-solve kwa dakika 1 tu., Asikudanganye mtu chama ni rasilimali watu, CUF ni chama kikubwa ikibidi kutokea hayo uliyotarajia hivyo ni viongozi wa juu tu wa CUF kutamka neno 1 tu kwamba sasa kura pigieni Chadema ama Tumeanzisha chama kipya jina lake ni hili sasa kura zipigiwe cha kwnye jina la chama hiki.,

Zanzibar ni tofauti sana na sehemu nyengine yeyote duniani unayoijuwa ama uliyowahi kuijuwa, kauli ya Kiongozi mkuu wa CUF (maalim seif) inafanya kazi kwa mara moja na kusambaa chini ya sekunde 1 na kufanyiwa kazi na wananchi wake kuliko hata umeme unavyoweza kukuathiri katika mwili wako kama utaushika kwa mkono.

Wazanzibari na wana CUF ni wanachama sugu sana wana misimamo isiyotetereka. Ata ufanye nini wakienda kwenye sanduku la kura wanakuwa hawafanyi makosa. Huyo propesa baada ya kujiuzulu anachokifanya sasa ndio ajira yake atafika mwisho tu atakwama CUF ina uzoefu mkubwa wa haya yanaendelea kutokea na baadae chama husimama imara.
 
Anaandika Masoud Sanani.

Chama cha Wananchi (CUF) ni moja ya
vyama vikongwe vya siasa nchini ambavyo vimekuwa na maendeleo tangu kuanza kwa mfumo wa siasa wa vyama vingi nchini mwaka 1992.

Miaka ya nyuma, CUF iliwahi kuwa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania kabla ya kuondolewa hivi karibuni na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho kwa sasa ndicho kinaongoza upinzani.

Mbali na hilo, CUF ndicho chama cha siasa chenye nguvu zaidi kwa upande wa Zanzibar, katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Katika chaguzi mbalimbali zilizopita, CUF imekuwa inashinda majimbo yote ya kisiwa cha Pemba na baadhi ya majimbo ya Unguja na kukiacha Chama cha Mapinduzi (CCM)
ambacho ndicho kinachotawala kikipata baadhi ya majimbo ya kisiwa cha Unguja pekee.

Hata hivyo, CUF hivi sasa haina uwakilishi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar na mabaraza ya miji, baada ya CCM kushinda viti vyote vya uwakilishi na madiwani kutokana na chama hicho cha upinzani kukataa kushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar baada ya matokeo ya ule wa Oktoba 25, 2015 kufutwa.

Mgogoro wakomaa
Kwa sasa CUF ipo katika mgogoro mkubwa uliosababishwa na Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba ambaye alijiuzulu nafasi hiyo, lakini akaamua kurudi miezi 10 baadaye.

Kitendo hicho kimesababisha mgogoro
ambao unazidi kufukuta na iwapo
hakutakuwa na hatua za kuumaliza
unaweza kukiyumbisha zaidi chama hicho. Profesa Lipumba alijiuzulu miezi michache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 jambo ambalo lilikifanya chama hicho
kuingia katika uchaguzi mkuu bila ya kuwa na mwenyekiti.

Hakuna mwenye uhakika kwamba uamuzi wa Lipumba wakati anajiuzulu ulikuwa na lengo gani, lakini kwa hisia za baadhi ya watu ni kwamba ulilenga kukifanya chama hicho kufanya vibaya katika uchaguzi huo

Hata hivyo, CUF ambayo ilishiriki katika
uchaguzi huo ikiwa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ulioundwa na vyama vya Chadema, NCCR Mageuzi na NLD
ilifanya vizuri kuliko katika Uchaguzi Mkuu mwingine wowote ule.

Kwa upande wa Tanzania Bara, chama
hicho badala ya kupata majimbo mawili au pungufu kama ilivyokuwa katika kila uchaguzi ilipata wabunge katika majimbo 10 na kwa mara ya kwanza ikaundahalmashauri za wilaya.

Kwa upande wa Zanzibar, kabla ya matokeo kufutwa CUF ilikuwa imeshinda viti 27 vya wawakilishi waliokabidhiwa vyeti vya ushindi sawa na CCM.

Hata mgombea wa Chadema na Ukawa kwenye urais wa Muungano, Edward lowassa akiungwa mkono na CUF yenye nguvu Zanzibar, alipata kura nyingi visiwani humo kuliko mgombea wa CCM.

CUF baada ya kufanya vizuri katika
uchaguzi huo, Profesa Lipumba aliamua kurudi kwenye nafasi ya uenyekiti, jambo ambalo bila shaka yoyote ndilo limekiingiza chama hicho katika mgogoro mkubwa.

Inaelekea msomi huyo wa uchumi baada ya kugundua kuwa kujiuzulu kwake hakukuleta madhara yoyote, bali manufaa zaidi, akaamua kurudi katika nafasi hiyo na kuleta mgogoro.

CUF inapoteza mwelekeo

Katika mgogoro huu ambapo upande wa uongozi unaompinga mwanasiasa huyo kurudi madarakani ukiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad ulimfukuza uanachama, lakini naye hakukubali na sasa ametengua vyeo vya wakurugenzi wa chama.

Akiungwa mkono na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ambaye alimtambua kuwa ni mwenyekiti halali wa chama hicho, Profesa Lipumba amekifanya chama hicho kuelekea kupoteza mwelekeo. Hivi sasa CUF ambayo ina kesi mahakamani ipo katika wakati mgumu kwani ni vigumu katika mazingira waliyo nayo kuwashawishi
wanachama wapya kujiunga au kupata
wafuasi wapya hasa vijana.

Mazingira yanayoizunguka CUF ni vigumu kumshawishi mtu yeyote kujiunga nayo. Hata hivyo, inatoa mwanya mkubwa kwa wanachama wa chama hicho kujiunga na vyama vingine. Serikali inaweza kukifuta
Haieleweki dhamira ya Profesa Lipumba na mgogoro huu uliosababishwa na kurudi
kwake kwenye uongozi, lakini kuna
uwezekano kwa Serikali kukifuta chama hicho ambacho kilipata umaarufu mkubwa nchini.

Ni rahisi katika hali hiyo mgogoro ukatumia mwanya huo Serikali ikakichukulia hatua na hata kukifuta kwa madai kwamba kinatahatarisha amani na utulivu nchini. CUF itafute suluhu Kuna haja kwa chama hicho kutafakari upya na kutafuta suluhu ya kuumaliza mgogoro huo kabla ya kuleta athari kubwa kwani Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 haupo mbali.

Inabidi kujipanga upya kuondokana na
mgogoro huo ili iweze kufanya vizuri katika uchaguzi kwa upande wa Tanzania Bara ili isirejee kama miaka ya nyuma ya kupata wabunge wawili.
CUF ikiondokana na mgogoro huo itakuwa katika mazingira mazuri zaidi ya kufanya Viizuri katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, hata kama usimamizi wa uchaguzi huo utakuwa na mizengwe kiasi gani.

Kwa upande wa Zanzibar, CUF ina nguvu kubwa ambayo kwa namna yoyote ile na kwa vyovyote haiwezi kuzuilika kushinda katika majimbo kadhaa ya Unguja na Pemba.

Kwa hiyo uongozi unapaswa kutafakari na kutafuta njia ya kukiokoa chama chao na njia rahisi kuliko zote ni kusameheana na kuelewa kwamba yaliyopita si ndwele wagange yajayo.

Kutokana na mgogoro huo kuendelea
kukimong’onyoa chama hicho hadi watu waliokuwa marafiki zamani kugeuka kuwa mahasimu, pengine dawa pekee ya kumaliza mgogoro huu ingepaswa kutoka nje ya chama baada ya jitihada za ndani kuonekana kugonga mwamba.

Hata hivyo, swali la kujiuliza ni nani
atajitokeza kuifanya kazi hiyo ya kuwakabili mahasimu wawili, Profesa Lipumba na Maalim Seif na wafuasi wao ili kuwasihi wakae pamoja na kumaliza sintofahamu zao kwa ajili ya mustakabali wa chama hicho?
Katika moja ya tahariri zake, gazeti hili
liliwahi kupendekeza Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa iingilie kati na kunusuru hali ya mambo, kwa kuwa msajili ndiye mdau na mhimili mkuu wa vyama vya siasa ambaye anaweza kujivika jukumu la usimamizi kwa sura ya ulezi na kuacha kubagua au kuonekana kuwa na upande.

Mwandishi ni mwanahabari mwandamizi nchini na amefanya kazi Televisheni Zanzibar, magazeti ya Uhuru na Mzalendo,Majira na Mwananchi.

Source: Mwananchi
Kwa nini iwe CUF hiii ina nguvu Pemba tu? Tangu ukoloni Pemba ilkuwa nguvu ya Sultani na Waarabu; kitovu cha Biashara ya Utumwa, ndiyo maana haikubaliki kabisa sehemu zilizoathiriwa na biashara ya watunwa. Kama tunaangalia wingi wa watu, tuangalie Tanzania nzima si Pemba peke yake. Ni sawa na Wachagga wawe na chama cha Kilimanjaro kifutw. Wanyamwezi wakawa na chama chao Tabora tu; bora kifutwe. Sheria ya Vyama vya Siasa inataka kiwe na sura ya kitaifa. Kifutwe kifutwe kifutwe.
 
Ni mtu mwenye kichaa tu anaweza hata kufikiri kuwa chama chenya wabunge 50+ kinaweza futwa na MSAJILI huyu uchwara!
Hata yy akiifuta CUFmajaji watatu wa rufaa watakirudisha
 
Kwa nini iwe CUF hiii ina nguvu Pemba tu? Tangu ukoloni Pemba ilkuwa nguvu ya Sultani na Waarabu; kitovu cha Biashara ya Utumwa, ndiyo maana haikubaliki kabisa sehemu zilizoathiriwa na biashara ya watunwa. Kama tunaangalia wingi wa watu, tuangalie Tanzania nzima si Pemba peke yake. Ni sawa na Wachagga wawe na chama cha Kilimanjaro kifutw. Wanyamwezi wakawa na chama chao Tabora tu; bora kifutwe. Sheria ya Vyama vya Siasa inataka kiwe na sura ya kitaifa. Kifutwe kifutwe kifutwe.

Hujafany reaserch yyt bali umeandika tu!
Ni chama gani chenye wabunge wengi Mkoa wa Lindi?
CUF ndiyo chama pekee cha kitaifa Tanzania sababu wameshinda kiti cha ubunge Tanzania Bara,Unguja na Pemba!Kama kuna chama kinatakiwa kufutwa sababu hakija enea TZ nzima ni CCM,CHADEMA na NCCR!
CCM haijashinda kiti chochote Pemba 2015 hata cha udiwani na usheha!CCM ilipoteza hata wadi ya Chokocho sehemu anayo toka Dr Shein!
Mkinywa viroba muwe mna lala badala ya kujitia tu aibu!Au Lindi nayo ni Pemba?
 
Back
Top Bottom