Mwl. Kaijage
JF-Expert Member
- Jan 3, 2015
- 216
- 214
KWA KUWA tumeamua kupambana dhidi ya rushwa, ufisadi, uzembe na uvivu;
NA KWA KUWA tumeamua kuhakikisha kuwa maliasili ya Nchi yetu Tanzania ni mali ya wananchi wote na kwamba lazima itumike kutokomeza umasikini nchini kwetu na kuleta
maendeleo sawia na endelevu ya kiuchumi, kijamii,kiutamaduni na kisiasa;
NA KWA KUWA tumeamua kujenga Chama cha siasa chenye lengo la kuchochea ujenzi wa Taifa la Kujitegemea, lisilo na unyonyaji wala ubaguzi wa rangi, dini, kabila, jinsia, maumbile, hali ya kipato na kwa kuzingatia misingi ya haki kwa watu wake wote;
NA KWA KUWA tumeamua kushiriki katika ujenzi wa Umoja wa Afrika ili kuwaenzi waasisi wa
ukombozi wa Mwafrika na kujenga bara lenye sauti yenye nguvu na ushawishi katika jamii ya mataifa ulimwenguni;
NA KWA KUWA tumeamua kupigania demokrasia,umoja, utu, uadilifu, uwajibikaji, uzalendo kwa Taifa;
NA KWA KUWA kwa nia moja tumeamua kujenga Chama chenye kufuata misingi ya Ujamaa wa
Kidemokrasia (Democratic Socialism), na misingi asili iliyoasisi Taifa letu (Unyerere) ikiwemo Azimio la Arusha; na
NA KWA wajibu tulio nao wa kujenga, kukuza na kuendeleza demokrasia na utamaduni wa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania;
HIVYO BASI; Sisi Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama cha Wazalendo (ACT) uliofanyika Dar es salaam leo tarehe 28 Machi 2015,
Tumepitisha KATIBA MPYA ya Chama chetu itakayojulikana kama KATIBA YA ACT YA MWAKA 2015.