Nadhani toka December 22, 2017 maji yalipotoka hadi wiki ya pili ya February 2018 ndipo maji yalipotoka tena baada ya Mange Kimambi kupost tatizo la maji Chalinze. Yakatoka kama wiki moja na nusu tukashukuru.
Cha kwanza cha kushangaza mwezi wote wa January 2018 maji hayakutoka hata siku moja, lakini tumeletewa ankara za kulipia maji tena kubwa kuliko miezi ambayo maji yalitoka walau mara tatu kwa mwezi.
Sasa toka katikati ya mwezi uliopita hadi leo zaidi ya mwezi maji hayajatoka, na maji ya visima vya hapa huwezi kunywa kupikia, hata kuoga yanawasha machoni, kufulia sabuni haikolei labda uoshee vyombo kwa chumvi kali iliyokuwepo ndani ya maji.
Leo hii inabidi tununue maji dumu la lita 20 linauzwa sh 800, kwa kubania nahitaji madumu matano kwa siku ni sh 5000 hiyo daily.
Msoga hapo maji hayakatiki wanashindwa kuwafungia hata siku moja kwa wiki watupe na sisi maji?
Wauzaji wa maji wanaenda kununua Msoga kuja kuuza hapa Chalinze, je ni hujuma ya mamlaka ya maji hapa Chalinze?
Unawezaje mwezi mzima ukazuia maji kwa wananchi wako, kwani wanaokaa Msoga wakikosa maji hata mara moja kwa wiki watadhurika?
Jamani naanza kuichukia nchi yangu