Chalamila: Wakimvaa Rais Samia nami nitawavaa

Katiba mpya ifute hivi vyeo vya kijinga. Mkuu wa mkoa amebakia kufanya uchawa Hana jipya.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema wakati fulani yeye na wenzake wanachukia majukwaani na wakati mwingine hata kuwa na lugha nzito, kwasababu hawapo tayari kuona Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akitukanwa na kurushiwa mawe ambapo ameahidi Watu wakimvaa Rais Samia na yeye atawavaa.

Akiongea Jijini Dar es salaam mbele ya Rais Samia leo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania, Chalamila amesema “Sisi Mh. Rais unaweza kutuona wakati fulani tunachukia sana majukwaani na wakati mwingine tumekuwa hata na lugha nzito, utuwie radhi kwelikweli lakini tunafanya hivi kwa sababu hatuko tayari kuona ukitukanwa na kurushiwa mawe”

“Hawa Polisi wameimba hapa wakikuvaa tutawavaa, na Mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam naahidi wakikuvaa, nitawavaa, juzijuzi uliona nipo soko la mabibo nilichukia sana, lile soko halijawahi kuleta hata senti moja Serikalini, tumekaa na DC Ubungo mpaka mwisho wa mwaka wa fedha litakuwa limeingiza sio chini ya bilioni 2 ambazo zilikuwa zinaingia kwenye mifuko ya Watu binafsi, hivi katika hali hiyo nicheke au nifanyaje?”

“Nimeamua kuwa mkali, na hiyo ndiyo kamba nitakayoendelea kuinyoosha ili matusi yasiende kwa Mheshimiwa Rais, niendelee kutekeleza maono yake kama Kiongozi aliyeniteua katika Mkoa huu wa Dar es Salaam, namshukuru Waziri wangu wa Mambo ya Ndani (Masauni) ni Mtu mmoja mtulivu sana Mimi moyo huo sina na sijawahi kumuomba hata Mungu anipe hata nusu kwasababu nitafeli kazi na watanionea na ufupi nilionao”
Hii simbilisi nayo haifiki mbali
 
Ni mwendo wa kujitoa akil ili kulinda ugali 🤣🤣🤣🤣
 
Huyu anahisigi anaogooopwa kwani aogopwe yenani? Anabreini yakimakonde naye atavaliwa au kuvuliwa kavp!!
 
omba utakao wavaa wasikuvae.
Kuna uhitaji wa kupimwa afya ya akili kabla ya kupewa kazi ya umma.
Namhurumia sana ikifika ile siku ya kukosa kuongoza.
Hivi anajua kuna kifo baada ya haya maisha na Mungu ndiye mwamuzi. Hiki kiburi majivuno dharau ushamba kimepita yote!
 
Mpk polisi nao wanajikomba kwa rais eti "wakikuvaa tutawavaa". Najuta kuzaliwa Tanzania. Bora kuzaliwa mende Ulaya
 
Hivi Job Description ya Mkuu wa Mkoa ni Ipi ?

Na katika kazi zake kuwa Chawa au kuvaa watu ni moja ya job kazi zake au hio ni Overtime ?
 
Back
Top Bottom