Chalamila: Tuko hatua za mwisho kuboresha Mwendokasi, Wananchi kuweni na Uvumilivu

Chalamila: Tuko hatua za mwisho kuboresha Mwendokasi, Wananchi kuweni na Uvumilivu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert John Chalamila amewataka Wananchi kuwa na Uvumilivu kidogo kwani tayari Serikali iko kwenye hatua za mwisho, za Utatuzi wa Changamoto ya upungufu wa Mabasi yaendayo haraka (Mwendokasi).

Chalamila amesema serikali inatambua changamoto hiyo na tayari imechukua hatua madhubuti kwa kuagiza mabasi zaidi ya 200 ili kuboresha huduma.

Soma
>
Chalamila: Mwendokasi Mbagala kuanza wiki ijayo
> Chalamila: Njia ya Kimara yatakuja mabasi 200, ukisema hatuitaki CCM haisaidii
 
Hayo mabasi yako wapi? Njia ya Mbagala ilikuwa ianze mwezi wa 8 mpaka leo kimya. Na mabasi tulionyeshwa yakiwa yameshafika bandarini. Na mwekezaji alishapatikana. Shida nini?

Hii ya Kimara na huko Mbezi nako ahadi kila siku. Huyo mwekezaji wa Kiarabu kagoma kuja au kuna nini?
 
Asante chalamila unaongoza watanzania walioko kwenye jiji kuu la nchi lililo na watu wa kila aina, lakini uzuri zaidi kwao sio uvumilivu, hawajitambui.
 
Leo Kimewaka kwenye vituo vya mwendokasi hapo Magomeni, nashangaa mpaka sasa hakuna uzi humu
 
Back
Top Bottom