Chakula hufungua moyo

yule single mother wa jirani yupo karibu kufungua moyo wa mtu
 
Kuna kajike kamekula baga chips bata Ceres za kutosha azam milk mwezi mzima hata bao moja sijapata wala kuitikia MWALIKO geto
 
Mifano ipo mingi tu kwenye biblia juu ya utoaji wa chakula na upokeaji wa mibaraka,
kwa mfano: Nabii Eliya na yule mama wa Serepta, yule mama alibarikiwa sana baada ya kumkarimu Nabii Eliya kwa chakula.

Hata baba wa familia akiihudumia vizuri familia yake chakula bila manung'uniko bhasi milango ya riziki huongezeka.

Biblia pia inasema ktk kitabu cha mithali kuwa mwanamke mwenye hekima ni yule afanyaye kazi ili kulisha familia yake.

Pia kitabu cha mhubiri kinasema mambo yote ni ubatili isipokuwa tu Kula, kunywa na kuvaa. Maana chakula kinaifurahisha nafsi. Ndiyo maana wale waliyozaliwa vijijini wana utamaduni wa kuwachinjia ndugu au wazazi wao mara wanapopatwa na matatizo fulani.

Kutoa Chakula kwa moyo mweupe ni kuomba mibaraka ya ajabu kutoka kwa Mola.

Hata matajiri baadhi hapa Tanzania huwa wanafanya hafla ya chakula kwa walemavu au watu fulani kwa lengo la kufurahisha nafsi zao. Kwa mfano: Ndugu Reginald Mengi.
 

hivi mwaka huu, Mengi amefanya hafla ya chakula kwa walemavu kweli?? Sokoro waito
 
Mkuu [HASHTAG]#OKOYOKO[/HASHTAG] Kwa mwaka huu sijajua kama Ndugu Mengi ameshawafanyia hafla ya chakula walemavu na mimi huwa napenda utamaduni wake huu.
 
Chakula ni cha kiroho, what you eat, the whole of it goes straight to your soul, na ndo maana chakula kitamu ni kilichopikwa either na mkeo au mzazi wako( it feels different). anayekulisha ndo anayekumiliki
 
Ndio maana wamama wanaambiwa usimuache sana hgal ampikie chakula mumeo siku nenda siku rudi. Yatakukuta utalia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…