storyteller
JF-Expert Member
- Nov 5, 2014
- 1,544
- 1,874
usiwaze sana huwa wanakunywa vidonge vya kutuliza njaaWanajamvi, wasalaam
Nimekua nikiwaza kuhusu vifaa vinavyoenda kufanya tafiti kwenye sayari zingine mf. Apolo, vifaa hivi nina hakika vimetengenezwa kuwa na mwendikasi kwa kuzingatia vigezo vingi, mf. Uzito na idadi ya watu wataokapanda, vifaa vya uchunguzi vitakavyobebwa n.k
Swali langu ni kwamba, wanaapolo(wanasayansi wanaoenda kufanya tafiti nje ya dunia) wanaopanda mule maisha yao yanategemea chakula, sasa,
Je, wakati wa uundaji wa hivyo vyombo(apolo) huwa wanaweka buti la misosi, je, debe ngapi za dona na maharagwe zinaweza kuingia?
Na kama hawabebi chakula, huwa wanakula nini katika kipindi chao cha uchunguzi huko angani.?
Nawasilisha.
usiwaze sana huwa wanakunywa vidonge vya kutuliza njaa
Hahaha eti dona..ngja tusubiri wataalam
usiwaze sana huwa wanakunywa vidonge vya kutuliza njaa
huko angani wana vituo vyao vya kuhifadhia mizigo ikiwemo vyakula
Wanajamvi, wasalaam
Nimekua nikiwaza kuhusu vifaa vinavyoenda kufanya tafiti kwenye sayari zingine mf. Apolo, vifaa hivi nina hakika vimetengenezwa kuwa na mwendikasi kwa kuzingatia vigezo vingi, mf. Uzito na idadi ya watu wataokapanda, vifaa vya uchunguzi vitakavyobebwa n.k
Swali langu ni kwamba, wanaapolo(wanasayansi wanaoenda kufanya tafiti nje ya dunia) wanaopanda mule maisha yao yanategemea chakula, sasa,
Je, wakati wa uundaji wa hivyo vyombo(apolo) huwa wanaweka buti la misosi, je, debe ngapi za dona na maharagwe zinaweza kuingia?
Na kama hawabebi chakula, huwa wanakula nini katika kipindi chao cha uchunguzi huko angani.?
Nawasilisha.
A hahahahaha haha, kaka umenikumbusha kipindi nipo mtoto kulikuwa na katuni ya TOm and jerry, ilikuwa inahusu trip ya kwenda mwezini. Mle kuna professor alitengeneza magic foods kwa kutumia unga, ukiweka drop ya maji ile unga unabadilika kutokana na contents zake. Mfano unga ni wa beef burger basi chakula kinabadilika na kuwa beef burger. Wakaenda nao mwezini siku zote ndo nilikuwa chakula chao.
asante mkuu
Mkuu una miaka mingapi sasa mbona hiyo katuni haivuki miaka mitano toka imetoka mm mzee na bado naangalia katuni na wanangu raha sana
Umeuliza maswali ya muhimu. Kwa ufupi niseme hakuna binadamu aliyewahi kusafiri angani zaidi ya kilomita laki 4. Safari ya mwisho ya binadamu anga za mbali ilikuwa ni mwezini mwaka 1972. Kwa sasa kuna Kituo cha Kimataifa cha Anga (International Space Station) kilichopo kilomita zaidi ya 420 angani, ambacho huzunguka dunia kila baada ya dakika 90 kwa mwendo kasi wa maili 18,000 kwa saa. Katika kituo hicho huwepo wanasayansi wanaoishi na kufanya tafiti mbalimbali za kisayansi hasa sayansi ya anga za juu.
Kituo hicho hupata mahitaji kutoka duniani. Wanasayansi (wakiwemo wa Marekani) hupelekwa na kurudishwa duniani na chombo cha safari za anga cha Urusi kinachoitwa Soyuz baada ya kile cha Marekani, Shuttle, kusitisha huduma.
Safari za anga za mbali hufanywa kwa kutumia vyombo peke yake. Kwa mfano, NASA ilituma chombo, New Horizons, kwenda kuchunguza sayari ya Pluto, ambayo Jumuiya ya Kimataifa ya masuala ya anga ilishaiondoa kwenye orodha ya safari. Chombo hicho kilisafiri maili zaidi ya bilioni 3 kwa muda wa miaka 9.5 na mwaka huu ulipita Pluto ambapo imethibitisha kuwa ni sayari.
Jibu la swali lako kwa uhakika ni kwamba binadamu hajawahi kwenye umbali wa kilomita zaidi ya laki 4 (Mwezini).
Kaa ujue na hili kuwa hakuna binadamu aliyewahi kufika Mwezini.Umeuliza maswali ya muhimu. Kwa ufupi niseme hakuna binadamu aliyewahi kusafiri angani zaidi ya kilomita laki 4. Safari ya mwisho ya binadamu anga za mbali ilikuwa ni mwezini mwaka 1972. Kwa sasa kuna Kituo cha Kimataifa cha Anga (International Space Station) kilichopo kilomita zaidi ya 420 angani, ambacho huzunguka dunia kila baada ya dakika 90 kwa mwendo kasi wa maili 18,000 kwa saa. Katika kituo hicho huwepo wanasayansi wanaoishi na kufanya tafiti mbalimbali za kisayansi hasa sayansi ya anga za juu.