Chakula cha Mama Ntilie na utamu wake

Chakula cha Mama Ntilie na utamu wake

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,606
Kwa maisha ya Kitanzania hakuna mtu ambaye hajawahi kula chakula cha mtaani /vibanda hodi /uchochoroni au kwa jina maarufu 'Mama Ntilie'.

Bei yake huwa ni ya kawaida sana (pengine robo ya chakula cha hotelini) na huwa kinawekwa kingi sana kwa jina maarufu 'cha kushiba'.

Zifuatazo ni sifa au tabia za chakula cha mama ntilie:-

1. Ujazo wake ni mkubwa sana (cha kushiba)

2. Rosti yake (mchuzi wa nyama/samaki) huwa ni mzito sana unaovutia machoni. Masalu hufanya kazi yake.

3. Bei yake huwa inaanzia TZS 800.000 mpk TZS 1.5000 kwa sahani moja

4. Huwa kinagombaniwa sana

5. Bakuli na sahani huwa ni chache sana na huwazinasuuzwa tu na kuwekea chakula cha mlaji mwingine

6. Wapishi wengi huwa wanene

7. Mazingira huwa machafu sana. Ila chakula kitamu

8. Chakula hiki huisha mapema sana

Nini siri ya utamu wa vyakula ambavyo hupikwa sehemu chafuchafu. Hata Kitimoto nae anahusika!
 
Bei nafuu na wingi wa chakula,sababu ni tatu, hawalipi kodi kubwa, Ada ndogo ya maeneo ya Biashara, gharama ndogo ya usafi na uendeshaji.
 
Wali jaa (wali wa jana), mchuzi juu (mchuzi wa juzi), natania tu jaman ila kwa wale wamama chakula ni kitamu bei ni ndogo
 
Mimi sijawahi kula kwa mama ntilie kwani Nina kinyaa sana, wakitoka chooni hawanawi wanaendelea tu kupika mikono imebeba kinyesi halafu utakuta anashika nyanya anakatakata, ndiyo maana mnasema mchuzi ni mzito halafu mtamu kumbe mnakula mavi, wakati mwingine wanashika tambala la kudekia kula wakati bila kunawa mikono kwa maji na sabuni wanaendelea kushika vyakula, wengine mbaya zaidi wana watoto wachanga kutwa wakiwatawaza watoto mavi halafu hawanawi mikono yao kwa maji yanayotitirika na sabuni
 
Una una uhakika huko mahotelini huwa wananawa wakitoka chooni? Au huwa hawaendi kunya wao?
Tena bora mama ntilie wanapikia sehem ya uwazi kabisa kuliko hao unaowaita "wastaarabu" wanajifungia jikoni huko ndo balaa tupu
 
NAKUMBUKA SEKONDARI TULIKIPA HESHIMa SANA HIKI CHAKULA NA TUKAITA NI RB yaani rice&beans ==700 tsh kwa fedha halali ya kitanzania 300 matunda kwisha njaa

upload_2018-2-9_10-21-26.jpeg
 
Mimi sijawahi kula kwa mama ntilie kwani Nina kinyaa sana, wakitoka chooni hawanawi wanaendelea tu kupika mikono imebeba kinyesi halafu utakuta anashika nyanya anakatakata, ndiyo maana mnasema mchuzi ni mzito halafu mtamu kumbe mnakula mavi, wakati mwingine wanashika tambala la kudekia kula wakati bila kunawa mikono kwa maji na sabuni wanaendelea kushika vyakula, wengine mbaya zaidi wana watoto wachanga kutwa wakiwatawaza watoto mavi halafu hawanawi mikono yao kwa maji yanayotitirika na sabuni
Si vinapikwa na kuchemsha mkuu?
 
Usizoee kula kwa mama ntilie aka mama kapemba; utamsahau mkeo ohooo shauri yako!!
 
Back
Top Bottom