Chakula cha Mama Ntilie na utamu wake

Chakula cha Mama Ntilie na utamu wake

maxresdefault.jpg
 
Kuna mmoja nyanda za juu kusini alikuwa anachanganya na damu ya Siku zake na maji ya kupikia kuanzia chai hadi chakula, watu walikuwa wanaja kwenye banda lake hatari.
 
Bongo its the only place ukipitia maisha ya shida unaitwa hero...lets fight this mentality
 
Mimi sijawahi kula kwa mama ntilie kwani Nina kinyaa sana, wakitoka chooni hawanawi wanaendelea tu kupika mikono imebeba kinyesi halafu utakuta anashika nyanya anakatakata, ndiyo maana mnasema mchuzi ni mzito halafu mtamu kumbe mnakula mavi, wakati mwingine wanashika tambala la kudekia kula wakati bila kunawa mikono kwa maji na sabuni wanaendelea kushika vyakula, wengine mbaya zaidi wana watoto wachanga kutwa wakiwatawaza watoto mavi halafu hawanawi mikono yao kwa maji yanayotitirika na sabuni
Umekulia ushuani mkuu huku kwetu kawaida hatuangalii hayo mkuu
 
Mtu alieshikwa tumbo la kuhara akiwa stendi ya mabasi huwa anasifia sana jinsi choo cha stendi kilivyomsitili.... uwezo wetu wa kujikuna umeishia hapo, hatuna jinsi ya kuviona vitamu regardless vinaandaliwa na nani au katika mazingira yapi.
Wain roone na wenzake walikula kwa mamantilie na wakasifia vile vile kuwa vitamu
 
Kwa maisha ya Kitanzania hakuna mtu ambaye hajawahi kula chakula cha mtaani /vibanda hodi /uchochoroni au kwa jina maarufu 'Mama Ntilie'.

Bei yake huwa ni ya kawaida sana (pengine robo ya chakula cha hotelini) na huwa kinawekwa kingi sana kwa jina maarufu 'cha kushiba'.

Zifuatazo ni sifa au tabia za chakula cha mama ntilie:-

1. Ujazo wake ni mkubwa sana (cha kushiba)

2. Rosti yake (mchuzi wa nyama/samaki) huwa ni mzito sana unaovutia machoni. Masalu hufanya kazi yake.

3. Bei yake huwa inaanzia TZS 800.000 mpk TZS 1.5000 kwa sahani moja

4. Huwa kinagombaniwa sana

5. Bakuli na sahani huwa ni chache sana na huwazinasuuzwa tu na kuwekea chakula cha mlaji mwingine

6. Wapishi wengi huwa wanene

7. Mazingira huwa machafu sana. Ila chakula kitamu

8. Chakula hiki huisha mapema sana

Nini siri ya utamu wa vyakula ambavyo hupikwa sehemu chafuchafu. Hata Kitimoto nae anahusika!
Assessment yako ni nzuri mkuu, ila hizo bei mbona hazieleweki.T.Sh.800.000 mpaka 1.5000! Nadhani labda ni T.Sh.800 mpaka 1,500!

Anyway,hiyo sio point yangu muhimu.Point yangu muhimu ni kwamba mimi niliacha kula huko. Nilikuwa napenda sana niwapo maeneo ya kazi isolated ambapo hakuna respectable restaurants kula kwao.Siku moja niliwahi asubuhi na mapema nikashuhudia jambo la ajabu sana.Niliona kwa macho yangu Mama Ntilie mmoja akikojolea chai!Dah,hamu iliniisha mkuu.Yule mama alinisihi sana na kuniambia nimtunzie siri yake.Nilifanya hivyo,ila dah,nilichoka.

Baada ya kuchunguza na kuuliza kulikoni, nimeambiwa kwamba wengi wao wanatumia ushirikina kuvuta wateja kwenye biashara zao.Tena nimeambiwa there is more than that!Tangu hapo mama ntilie na mimi mbali mbali kabisa mkuu.
 
Mkuu wala si kitu kibaya saaana,.ww kula kama huna budi Ila kama unauwezo wa kujipikia mwenyewe si vibaya.
Kama inafaa ninon'goneze huku pm vinginevyo umeniogopesha nikijua nitakuwa huru kula hata kama wanapikia maji ya mochwari
 
kuna mama alikua anaitwa mama jero mitaa ya biasi alikua anauza mia tano plate had mia saba. Hicho cha mia saba mnaweza kula watu wawili.maharagwe unaweza kukuta yako manne tu mchuzi utaukuta chini ya ubwabwa. ule Michele sijui alikua anautoa wapi. amesaidia masela wengi walio kua wanapiga Pasi ndefu.
 
Back
Top Bottom