Chaguzi za Zanzibar na Wabara

Chaguzi za Zanzibar na Wabara

dos.2020

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2009
Posts
14,163
Reaction score
11,823
Moja ya tatizo kubwa kwenye chaguzi za Zanzibar ni Wabara kuingizwa na CCM katika kupiga kura za kuchagua Rais wa Zanzibar pamoja na wawakilishi katika baraza la wawakilishi.

Hili ni kinyume na taratibu kwani Wabara wanaoishi Zanzibar wanatakiwa wapige kura ya kuchagua Mbunge pamoja kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano tu. Kwa hiyo huwa hahusiki moja kwa moja na ZEC.

Lakini CCM toka mwaka 1995 wamekuwa wakiwatumia wabara kwenye upigaji wakura. Na hili limechangia kwa asilimia kubwa kuzidisha chuki baina ya Wazanzibari na Wabara.

Asilimia kubwa ya Wabara wanaoishi Zanzibar husapoti chama cha CCM wengi wakijazwa kasumba nyingi chafu ili waendelee kuamini kuwa CCM ndio usalama wao.

Hivi miezi ya karibuni kumekuwa na zoezi la kuwapatia Wabara waliohamia Zanzibar miaka ya karibuni vitambulisho vya Zanzibar ili waweze kuwaandikisha kwa ajili ya upigaji kura za mwakani.

Hili jambo ni hatari sana, linaendelea kuwaumiza nakuwatia hasira sana Wazanzibari.

Ndugu zangu wa bara mnaoishi Zanzibar kwanini hamtulii mkafanya mlioyaendea ya kama kutafuta hela ustick na ishu zako tu kwanini huwa mnajiingiza kwenye siasa za watu?

Hamuhisi kama mnajitafutia matatizo na kuwatafutia wenzenu ambao hawana hayo mambo?

Tusije kushangaa siku za mbele tu yakaanza kutokea kama yale yaliotokea Afrika Kusini. Tusije kutafuta mchawi ni nani.

Ninavyoamini mimi kama CCM hawayajaacha madaraka kule Zanzibar ipo siku kitunaka kule ndipo tutakapotafutana.
 
Lakini mkuu,mbona hapa kwetu mbagala mnachagua hata diwani na kuchaguliwa pia,yaani wao kuchagua tu hutaki!siku wakchanguliwa si utakufa wewe. Say like spika wa baraza la wawakilshi awe Johnson Mwalubadu kutoka Jimbo la Mwera.
 
Mkuu wale ni watanzania, kwahiyo wanahaki ya kuchagua kura yoyote inayohusiana na Utanzania. Ila kura ya Raisi wa Zanzibar na Mwakilishi Zanzibar ni kwa ajili ya wazanzibari tu. umenipata vizuri hapo?
 
Wanahaki Zanzibar kujichagulia wenyewe kiongozi wao. Hao wabara Ni walowezi kama walowezi wengine. Kama vipi watimueni, ndiyo maana mnaserikali yenu na sisi huku hatuna serikali yetu tuna ya muungano tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazoweeni tu hao mnao.
 
watimuliwe na nani? Na wanalindwa na CCM?
 
musije kuishia kulalamika tu kama Zanzibar wabaguzi, makatili kwa yatakayokuja tokea mbeleni
Ni nyie tu na roho zenu..sema tu ukitaka kufanya kisasi chimba makaburi mawili huenda moja likawa lako.
 
Mkuu wale ni watanzania, kwahiyo wanahaki ya kuchagua kura yoyote inayohusiana na Utanzania. Ila kura ya Raisi wa Zanzibar na Mwakilishi Zanzibar ni kwa ajili ya wazanzibari tu. umenipata vizuri hapo?

Yaani nyinyi mna haki zote mkiwa Tanzania Bara! Na hakuna anayewabagua kwa sababu ya huo Uzanzibari wenu, ila sisi hatuna haki tukiwa Zanzibar! Bora tuendelee tu kuwatawala maana hamueleweki mnataka nini.
 
Punguza jazba mkuu, Muundo wa Muungano wetu ni wa Serekali mbili. Ya Zanzibar na ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Kwahiyo kwa mujibu wa muundo wa muungano wetu kuna Mzanzibari na Mtanzania hivyo ndivo mulivyoutengeneza sasa munalalamika nini?
Miaka yote hiyo vyama vya upinzani vimekuwa vikipigania kuwepo na serekali tatu ili kumaliza hayo matatizo hamutaki, Halafu bado munaendelea kulalamika.
 
Back
Top Bottom