Chaguzi za Ujumbe Nec zaiweka CCM kitanzini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chaguzi za Ujumbe Nec zaiweka CCM kitanzini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Sep 17, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Lowassa adaiwa kumhujumu Sumaye, kumbeba Nagu
  .Mwenyewe ang�aka, asema wote ni marafiki zake
  Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na Nagu.
  Chaguzi zinazoendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimekuza wigo wa makundi yanayopingana, yakielekea kujiimarisha kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.

  Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE Jumapili kwa zaidi ya wiki mbili, umebaini kuwepo mikakati inayohusisha mbinu chafu ikiwemo kuwahonga baadhi ya viongozi na wajumbe wanaoshiriki vikao vya maamuzi.

  Makundi yaliyoanzishwa na kujiimarisha baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2005, yameibuka ingawa safari hii, miongoni mwa waliokuwa pamoja, wameganyika.

  Mgawanyiko huo unahusishwa na kashfa za ufisadi zilizosababisha mawaziri watatu, akiwemo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kujiuzulu.

  Vyanzo mbalimbali kutoka ndani ya CCM vimeeleza kuwa pamoja na kuwepo hali hiyo nyakati za chaguzi kwa miaka iliyopita, hivi sasa makundi hayo yamejijenga kwa ‘sura’ ya uhasama usiokuwa na tija kwa chama hicho.

  “Zamani tulishindana kwa hoja, lakini sasa hivi tumefikia hatua ya kutaka hata kuuana, ushindani wa hivyo hauna tija kwa CCM,” kilieleza chanzo chetu.

  Kwa upande wa hujuma, inaelezwa kuwa vinara wanaoongoza kundi moja lenye uwezo mkubwa kiuchumi, likiwahusisha watuhumiwa wa ufisadi, limepandikiza watu wanaotakiwa kuingia kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec).

  Lengo la kuwaingiza watu hao, linatajwa kuwawezesha kuungwa mkono kwa wagombea watakaojitokeza kuwania udiwani, ubunge na urais.

  Hali hiyo imesababisha kuwepo msuguano mkali unaosababisha kuwepo vitendo vya kuhujumiana, huku wana-CCM waadilifu wakidhibitiwa kwa nguvu ya fedha.

  “Watu wanapewa hongo, wanabadilisha muhtasari wa mkutano ili kupenyeza majina ya waliokataliwa,” kilieleza chanzo kingine mkoani Manyara.

  Chanzo ambacho hakikutaka kutajwa jina lake, kilieleza kuwa, aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alionekana juzi huko Endasak wilaya ya Hanang mkoani Manyara, akimpigia kampeni za chini-chini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Mary Nagu.

  Hata hivyo, NIPASHE Jumapili ilipowasiliana na Lowassa, aling’aka, huku akisema yupo jijini Dar es Salaam.

  “Mimi nipo Dar es Salaam, ninashangaa wanaosema nilikuwa Endasak, sijui maneno hayo yanatoka wapi, lakini ukweli ni kwamba sikwenda kufanya kampeni yoyote,” alisema.

  Hanang’ ni moja ya wilaya zenye mvutano mkali kwa wagombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM, ukiwahusisha zaidi Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na Nagu. Pia yumo Leonsi Marmo.

  Hata hivyo, Nagu amekuwa akishutumiwa kuhusika na njama za kulipenyeza jina lake kinyemela, baada ya kuenguliwa katika ngazi ya wilaya.

  Lakini Lowassa alisema hana upande wowote anaouunga mkono kati ya Sumaye na Nagu, akiongeza, “wote hao ni marafiki zangu, ninawaheshimu, siwezi kusimama upande wowote.”

  Alisema, “wananchi wanapaswa kuyapuuza na mimi ninaamini mmoja wao akishinda, chama kitakuwa kimemchagua hivyo jukumu langu ni kumuunga mkono.”

  Hata hivyo, taarifa zaidi zilieleza kuwa hali ya kutoaminiana imejitokeza kwenye kundi linalomuunga mkono Nagu, huku baadhi yao wakishutumiwa kwa kubadili msimamo na kumuunga mkono Sumaye.

  Pia inaelezwa kuwa, baadhi yao wanashutumiwa kwa kueneza propaganda zinazoelezea Nagu kuungwa mkono na Lowassa, hali inayodaiwa kutomsaidia (Nagu) kisiasa.

  Wakati hali ikiwa hivyo, kuna taarifa za kuwepo mikutano ya usiku, ikiwahusisha wagombea wanaotajwa kutokukubalika ndani na nje ya chama kukutana na wajumbe wanaotoka kwenye mikoa na wilaya zao.

  Wajumbe wanaohusishwa na vikao vya usiku ni watakaoshiriki kupiga kura kuchagua mjumbe mmoja kati ya walioomba ujumbe wa Nec.
  Matumizi ya hongo yanatajwa kuwa sehemu itakayozidi kukimega chama hicho, kwa vile fedha kwa kuzingatia uwezo wa kiuchumi ama ushawishi wa mjumbe.

  “Sasa wale wanaopata fedha kidogo, wakijiunga pamoja dhidi ya wanaolipwa fedha nyingi, chama kitazidi kumeguka,” kinaeleza chanzo chetu.

  Imeelezwa kuwa wapo wagombea wanaowagharimia wajumbe watakaopiga kura wakitoka maeneo ya mbali na mijini, kwa kuwalipia malazi na posho, wakati wakisubiri siku ya uchaguzi utakaofanyika kati ya Septembe 28 na 29, mwaka huu.

  Hali hiyo inatajwa kuwaepusha wasikutane na wagombea wengine, hivyo kuimarisha uhakika wa kupigiwa kura.

  Mathalani wilayani Hanang, mmoja wa wagombea ambaye ushiriki wake una utata (jina tunalo), anadaiwa kufanya kampeni usiku wa manane, ambapo Septemba 9, mwaka huu alikwenda ofisi za CCM, kata ya Gendabina na kuzungumza na wajumbe.

  Taarifa zinaeleza kuwa miongoni mwa wajumbe hao walitoka matawi ya Gocho, Bajomod na Gitinga.

  Kaimu Kamanda wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) mkoa wa Manyara, Samson Sanga, alisema ofisi yake haijapokea malalamiko yanayomhusisha mgombea yeyote na rushwa na kwamba atayafanyia kazi.

  Ingawa simu ya Nagu haikupatikana, lakini Sumaye, alithibitisha kuzisikia taarifa za hujuma zinazofanyika na kusisitiza kuwa hazifahamu.

  “Kwa kweli mimi sifahamu kama ni kweli japo nimekuwa nikiletewa taarifa za kufanyika kampeni za usiku…kama ni kweli ninaamini ni makosa kwa maana muda wa kampeni haujafika,” alisema.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Katika sinems itakayobadilisha 2015 hii ni moijawapo, nyingine mwaka kesho mapema.
   
 3. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Hivi popote anapokua Lowassa lazima pawe na hujuma, majungu na uchafu wote wa kisiasa?
   
 4. HANDO

  HANDO Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaaani hawa magamba cjui ndo mfumo wao nadhani wilaya ya mbulu KUNA PATASHIKA kati ya MZEE BAJUTA anayeegemea MRENGO wa nnywele nyeupe NA KATIBU MWENEZI WA CHAMA flatey ANAYEDAIWA ni kambi ya SUMAYE sasa cjui hawa wazee wanahangaika nn MAANA TUSHAAMBIWA NA UV CCM PWANI kwamba RAIS AJAYE HATATOKEA kanda ya kaskazini.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  CCM wanaweza kuweka record ya dunia kwa kutokuwa na msimamo. Walisema wanaondokana na mfumo wa mtu mmoja kuwa na vyeo vingi, kwa maana hiyo wabunge wasingeruhusiwa kugombea nafasi kama uenyekiti wa chama mkoa, au mawaziri wasingegombea nafasi NEC au CC. But true to their legendary status, sasa hivi wanameza matapishi mchana kweupe. Mary Nagu anagombea NEC wakati ni waziri? Hata kwenye CC wapo wengine ambao wapo kwenye cabinet!
   
 6. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  unashangaa ama unapigia mstari jawabu!!!
   
 7. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bdo hadi 2015 mengi yatajiri
   
Loading...