Chaguo la Mchungaji: Mgombea Urais wa CCM

Rev.Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
4,526
Reaction score
1,552
1. Awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ya mpito, inahitaji utashi wa hali ya juu wenye busara na hekima kuturudisha mstari ulionyooka ili tushikamane.

2. Ni ndoto, hasa kwa Watangaza Nia wanaokuja na ahadi za maziwa na asali, kuwa bila kurudisha Taifa katika mshikamano na unyoofu, tutaneemeka!

3. Busara na hekima zenye kutuunganisha na kuleta mshikamano na si mgawanyiko ndio uongozi tunaouhitaji, turudi kuwa Taifa imara la Umoja na Utu!

4. Ni kwa sababu hizo, za kujenga Taifa linaloaminiana na kuheshimiana Kiitikadi na tofauti zetu zote nyingine, Awamu ya 5 inahitaji busara kubwa sana na si ahadi za kuleta neema!

5. Ningekuwa mjumbe wa CC, NEC na hata Mkutano Mkuu wa CCM, anayefaa kuleta umoja wa kweli, kuzingatia haki, utu na chachu ya uwajibikaji na uadilifu.

6. Ningepiga kura yangu kwa Mwana CCM ambaye Taifa linamhitaji wakati huu mgumu wa majaribu na mpito Mh. Jaji Augustine Ramadhani agombee Urais wa Tanzania.

7. Sambamba ya kumchagua Jaji Augustino, Bi. Asha Migiro angekuwa chaguo langu kuwa mgombea mwenza na makamu wa Rais. Hii ndio tiketi ya ushindi kwa CCM yenye kutaka kuirudisha Tanzania katika umoja, uaminifu, uadilifu, mshikamano na uwajibikaji.

8. Lakini kama nitakuwa upande ule wa maslahi na ahadi zisizoeleweka, basi Watangaza Nia wengine wote watapitishwa kulinda maslahi ya Chama na maslahi binafsi ya makundi yanayovutana na kugombania utawala ndani ya Chama.

9. Hatuwezi kujenga nchi, kupiga vita na umasikini, ujinga na maradhi tukiwa tumetengamana na tuna visasi au kukosa busara kujenga umoja.

10. Tukiamua kuwa vipofu wa hali tete ya miaka 15 iliyopita, tukakimbilia maslahi na kutafuta utajiri eti kuondoa adha na tabu, tutapotea!

11. Hatuwezi kutengeneza Asali na Maziwa tukiwa na mivutano ya kitaifa au hata ndani ya vyama (CCM), huko ni kujenga nyumba mchangani!

12. Amani na mshikamano wetu, umeingia dosari kutokana na udhaifu unaotokana na tamaa za kutajirika na sera uchwara za neema za giza na za haraka haraka kutafuna rasilimali zetu.

13. Tusipokuwa na Serikali makini yenye busara na hekima, inayoendesha mambo kwa pupa, kejeli,kukiuka demokrasia na sauti tofauti, tutajuta na kuangamia zaidi katika dimbwi la umasikini, ufisadi na utengamano.

14. Tunaweza kurudi kwenye mstari mnyoofu bila kukurupuka kumaliza rasilimali zetu kiholela kwa haraka ya kuongeza pato la Taifa.

15. Shubiri ya kujenga mfumo imara wa uzalishaji mali ni Seikali imara iliyo sikivu, inayojihoji na kujikosoa, inayoangalia maslahi ya umma kwa ujumla na kwa manufaa ya umma mzima wa Watanzania na si maslahi ya Watanzania wachache au wawekezaji wa kigeni.

16. Hatutaweza futa umasikini, tengeneza ajira au kuota Matumaini, Upya na Mabadiliko bila kuwa na viongozi wenye Busara na Hekima.

17. Narudia tena, awamu ya 5 ni ya kutupitisha nyikani ambako tuna mifarakano mikubwa ya itikadi, kidini, kipato, maslahi na vipaumbele.

18. Tunajitaji kiongozi imara na ndani ya CCM atakayeweza kazi hii kwa hekima ni Jaji Ramadhani! Wengine tunaweza kuwataka Ila hawahitajiki !
 
Wote hao hawafai, miaka 10 nchi ikienda mrama wamepiga kimya na huyo Migiro alishiriki katika ujambazi na uhuni wa kuchakachua maoni ya Watanzania kuhusu katiba mpya. Hawatufai wote.

7. Sambamba ya kumchagua Jaji Augustino, Bi. Asha Migiro angekuwa chaguo langu kuwa mgombea mwenza na makamu wa Rais. Hii ndio tiketi ya ushindi kwa CCM yenye kutaka kuirudisha Tanzania katika umoja, uaminifu, uadilifu, mshikamano na uwajibikaji
...
 
Rama hawezi siasa za kisasa ukizingatia siyo mwanasiasa yule hawezi kwenda sambamba na kina Slaa,zitto,lipumba.
 
Nianze na kifungu cha 17. Taifa kuwa kwenye safari inayopitia nyikani pasipo na utulivu.

Uasisi wa Taifa ulifanyika kikamilifu Enzi hizo na kama mbegu ambayo ni lazima ioezi chini ardhini ili ichipue hilo limetokea. Kuharibika na kuoza huku ni kwa muda tu ili kupatikana mmea mpya utakao ota na kuchipua tena kwenye uso wa ardhi na kukomaa hadi kuvunwa kwa matumizi ya Taifa.

Uasisi umeharibika; Uasisi umeoza na waliouozesha kwa Ufisadi na Udhalimu mkubwa ni wengi ili kinara na NABII wake NI LAZIMA JINA LAKE LIKATWE. Na hakuna Ubishi litakatwa.

Mbegu ile ya Uasisi sasa itachipua na kuendelea kukuwa na kukomaa chini ya Ungozi mpya kama kinavyosomeka kifungu cha mwisho.

Kifungu cha 18. Jaji Agustino Ramadhani aendeleze ukomavu wa uasisi. Hatupuuzii hawa waliokatwa. Mchango wa kuozesha Taifa ulikuwa wa lazima ili kupata Mmea Mpya.

Walioozesha Taifa sasa wapumzike .. Muda wao umepita. Mchango wao hautasahaulika. Mwenyezi Mungu Awasaidie na kuwa tangulia.
 
ramadhani ccm kumpitisha ni sawa na kujitia kitanzi nani anamjua ,
mfano slaa amejiuza yapata miaka kumi lakini bado je huyu anayezaliwa leo kwenye siasa itakuwaje?nani atamuuza ?amefanya nini katika taifa hili kiasa cha kutuaminisha alichokifanya na kumpa nafasi
awe makamu wa MAGUFULI basi
 
Unajua utendaji wa Augustino Ramadhan. Alishakuwa judge Mkuu alishafanya nini? Kama huwezi ku manage taasisi utawezaje nchi. Kwa maoni yangu Augustino ndiye judge mkuu ovyo kuliko wote waliowahi kushika nafasi hiyo. Yes hali rushwa lakini ndiyo mwisho wake hapo.
 
taifa lilipofika haliitaji mchungaji linaitaji mtu mkali na mwenye uzoefu wa wakusimamia serikali kama MAGUFULI,
 
Unajua utendaji wa Augustino Ramadhan. Alishakuwa judge Mkuu alishafanya nini? Kama huwezi ku manage taasisi utawezaje nchi. Kwa maoni yangu Augustino ndiye judge mkuu ovyo kuliko wote waliowahi kushika nafasi hiyo. Yes hali rushwa lakini ndiyo mwisho wake hapo.

Nani anamjua?
kwanza,jaji mkuu lakini mahakama aliyokuwa anasimamamia ndo zinaongoza kwa kutunyanyasa masikini kwa rushwa ,kama alishindwa taasisi ndogo kama mahakana je serikali?
nafsi yake makamu wa mwandosya au maagufuli inamtosha ,wenye uzoefu na wanakubalika kwa kile walichokifanya ndani ya taifa hili awaachie nafasi,
 
1. Awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ya mpito, inahitaji utashi wa hali ya juu wenye busara na hekima kuturudisha mstari ulionyooka ili tushikamane.

2. Ni ndoto, hasa kwa Watangaza Nia wanaokuja na ahadi za maziwa na asali, kuwa bila kurudisha Taifa katika mshikamano na unyoofu, tutaneemeka!

3. Busara na hekima zenye kutuunganisha na kuleta mshikamano na si mgawanyiko ndio uongozi tunaouhitaji, turudi kuwa Taifa imara la Umoja na Utu!

4. Ni kwa sababu hizo, za kujenga Taifa linaloaminiana na kuheshimiana Kiitikadi na tofauti zetu zote nyingine, Awamu ya 5 inahitaji busara kubwa sana na si ahadi za kuleta neema!

5. Ningekuwa mjumbe wa CC, NEC na hata Mkutano Mkuu wa CCM, anayefaa kuleta umoja wa kweli, kuzingatia haki, utu na chachu ya uwajibikaji na uadilifu.

6. Ningepiga kura yangu kwa Mwana CCM ambaye Taifa linamhitaji wakati huu mgumu wa majaribu na mpito Mh. Jaji Augustine Ramadhani agombee Urais wa Tanzania.

7. Sambamba ya kumchagua Jaji Augustino, Bi. Asha Migiro angekuwa chaguo langu kuwa mgombea mwenza na makamu wa Rais. Hii ndio tiketi ya ushindi kwa CCM yenye kutaka kuirudisha Tanzania katika umoja, uaminifu, uadilifu, mshikamano na uwajibikaji.

8. Lakini kama nitakuwa upande ule wa maslahi na ahadi zisizoeleweka, basi Watangaza Nia wengine wote watapitishwa kulinda maslahi ya Chama na maslahi binafsi ya makundi yanayovutana na kugombania utawala ndani ya Chama.

9. Hatuwezi kujenga nchi, kupiga vita na umasikini, ujinga na maradhi tukiwa tumetengamana na tuna visasi au kukosa busara kujenga umoja.

10. Tukiamua kuwa vipofu wa hali tete ya miaka 15 iliyopita, tukakimbilia maslahi na kutafuta utajiri eti kuondoa adha na tabu, tutapotea!

11. Hatuwezi kutengeneza Asali na Maziwa tukiwa na mivutano ya kitaifa au hata ndani ya vyama (CCM), huko ni kujenga nyumba mchangani!

12. Amani na mshikamano wetu, umeingia dosari kutokana na udhaifu unaotokana na tamaa za kutajirika na sera uchwara za neema za giza na za haraka haraka kutafuna rasilimali zetu.

13. Tusipokuwa na Serikali makini yenye busara na hekima, inayoendesha mambo kwa pupa, kejeli,kukiuka demokrasia na sauti tofauti, tutajuta na kuangamia zaidi katika dimbwi la umasikini, ufisadi na utengamano.

14. Tunaweza kurudi kwenye mstari mnyoofu bila kukurupuka kumaliza rasilimali zetu kiholela kwa haraka ya kuongeza pato la Taifa.

15. Shubiri ya kujenga mfumo imara wa uzalishaji mali ni Seikali imara iliyo sikivu, inayojihoji na kujikosoa, inayoangalia maslahi ya umma kwa ujumla na kwa manufaa ya umma mzima wa Watanzania na si maslahi ya Watanzania wachache au wawekezaji wa kigeni.

16. Hatutaweza futa umasikini, tengeneza ajira au kuota Matumaini, Upya na Mabadiliko bila kuwa na viongozi wenye Busara na Hekima.

17. Narudia tena, awamu ya 5 ni ya kutupitisha nyikani ambako tuna mifarakano mikubwa ya itikadi, kidini, kipato, maslahi na vipaumbele.

18. Tunajitaji kiongozi imara na ndani ya CCM atakayeweza kazi hii kwa hekima ni Jaji Ramadhani! Wengine tunaweza kuwataka Ila hawahitajiki !
Watanganyika wengi, nikiwa mmoja wao, wanaona kumchagua mzanzibari kuwa rais wao kama dhihaka hasa baada ya kunyimwa Tanganyika yao na ccm. ccm wafanye kosa hilo waone tutakavyowatimulia vumbi.
 
Rama hawezi siasa za kisasa ukizingatia siyo mwanasiasa yule hawezi kwenda sambamba na kina Slaa,zitto,lipumba.[/QUOTE

Umesioma hiyo post na kuielewa vizuri? Hakuna mahali aliposema mgombea anahitajika kupambana na kina Zitto au Slaa.

CC: Rev. Kishoka
 
ramadhani ccm kumpitisha ni sawa na kujitia kitanzi nani anamjua ,
mfano slaa amejiuza yapata miaka kumi lakini bado je huyu anayezaliwa leo kwenye siasa itakuwaje?nani atamuuza ?amefanya nini katika taifa hili kiasa cha kutuaminisha alichokifanya na kumpa nafasi
awe makamu wa MAGUFULI basi

Ambye angejitia kitanzi si Jaji Ramadhani, bali ni CCM. Hawamjui, si mwenzao na kwa yeye kutokuwa na hata ncha ya doa au tuhuma, hawawezi kumrubuni na walihofia angewaangusha.

Nikiangalia wasifu wa 5 bora na kelele zote za CCM kudai kujivua magamba, uwajibikaji na uadilifu halafu aliye bora kuliko wote hata 5 bora hakupelekwa, ni wazi chama kinaendeshwa kimaslahi na kulinda uchafu uliomzaa Lowassa na ubabe kudhulumu unaofanywa na vyomo vya dola na waandamizi wa serikali na ccm.

Nilisema awali, mgombea mwenye busara na tunayemhitaji, wote kama Taifa bila makundi alikuwa ni Jaji Ramadhani. Lakini mgombea CCM waliyemtaka wapate Ikulu kwa udi na vumba ndio wamemchagua Magufuli na tumepumbaa sana na kusifia "huyu ni jembe mchapa kazi"!

Mlisikia kauli ya kejeli aliyotoa kwa wapinzani? kuendeleza kejeli na dharau alizozifanya Kikwete kabla ya Magufuli kuongea?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom