chaguo la kumezea au malipizi......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

chaguo la kumezea au malipizi.........

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Rutashubanyuma, Nov 30, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,596
  Likes Received: 415,719
  Trophy Points: 280
  hasira za mkizi hutuponza kujenga makusudio ya kulipiza kisasi..............................lakini hayo huwa ni kivuno cha mvuvi................kisasi humfunga mlenga kwa mlengwaji........................kwani kusudio la kulipiza kisasi hukufanya umfuatilie kwa karibu mlengwa kwa kusudio la kumwonyesha kazi bila ya kujijua ya kuwa ni wewe ambaye utaonyeshwa kazi kwa kutumia muda mwingi kutekeleza azma tajwa.........

  kwa lugha nyingine mwindaji hugeuka kuwa mwindwa.....................hata ukifanikiwa katika lengo la kumkomoa mlengwa wako bado utajiona una pengo la kutaka kumkamua zaidi.........................kwa sababu hata ile adhabu utakayomtwisha mlengwa wako bado utaoana haitoshi................ungelipendelea kumwongezea nyingine.............................

  lakini kumezea pamoja na kuonekana kuwa ni udhaifu hukuondolea kifungo cha kumfuatilia mlengwa wako na kukufanya uwe huru......................huhitaji kujua anafanya nini wala huguswi na nyendo zake kwa sababu umemsamehe bila hata ya kusubiri kuombwa msamaha..........................................na uhuru tajwa wakuwezesha kuendelea na shughuli zako bila kukosa usingizi au zengwe la aina yoyote ile......................................................

  makala hii imehamasishwa na msamaha ambao jerry Muro aliutoa kwa wote ambao walinuia mabaya yamkumbe wawe ndani au nje ya dola.........................................kwa maoni yangu Muro kajipatia uhuru wake na hivyo sasa hahitaji kujua maadui zake wanafanya nini......................ili akawaonyeshe kazi..........................................he just moves on with his life after all the trouble real and imaginary walizomletea........hongera sana muro kwa kutachia urithi huu ambao ndiyo dhana nzima ya uafrika.........................kumbuka kenyatta na mandela baada ya kutoka kwenye vifungo vyao walisema.........................."forgive and forget"..................hawakusubiri waombwe msamaha...............they just moved on..............................what a lesson to all of us??????????????????
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Nov 30, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Ruta, ungepunguza hiyo midoti doti ingependeza zaidi.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,596
  Likes Received: 415,719
  Trophy Points: 280
  siwezi..................hiyo ndiyo staili yangu ya uandishi....................tujifunze kuzoea staili mbalimbali za uandishi............lengo ni kufupisha na kukuonyesha kuwa lengo tajwa..........................
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Nov 30, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Heheheheee haya bana. Hamna neno.
   
Loading...