Kwanini Victoria Charles Mwanziva, Makamu Mwenyekiti UVCCM Taifa 2022-2027

Shabani Ajaha

Member
Aug 18, 2021
78
60
KWA NINI VICTORIA CHARLES MWANZIVA MAKAMU MWENYEKITI UVCCM TAIFA 2022-2027

Kuna mambo Matano Muhimu sana katika Maisha ya kawaida mtu anapotaka kununua kiwanja katika eneo Fulani na kujenga nyumba lazima azingatie upatikanaji wa huduma muhimu za Kijamii kama Maji, Umeme, Nyumba za Ibada, Shule na Hospitali.

Vivyo hivyo hata katika uwanja wa siasa wananchi wanapoenda kupiga kura kwa mgombea Fulani lazima wazingatie mambo makubwa Matano muhimu kutoka kwa mgombea. Moja dhamira ya dhati ya mgombea katika nafasi anayoiomba, Pili Historia yake ya uongozi na kazi mbalimbali alizowahi kuzifanya, Tatu Maono na sera za mgombea kwenye nafasi anayoiomba kwa ujumla, Nne Mahusiano ya mgombea na Jamii anayoomba kuiongoza, Tano uwezo wa mgombea katika kujenga hoja na kulinda maslahi ya jamii anayotazamia kuiongoza.

Uongozi ni dhamana ambayo mtu hupewa na watu ili awaongoze kuyafikia malengo mbalimbali wanayojiwekea kama taasisi au jamii. Tunaenda kwenye Uchaguzi Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi 2022, Jumuiya inakwenda kupata viongozi ambao wanatakiwa kuisogeza hapa ilipo na kuipeleka mbele zaidi. Kuna mazuri yamefanyika katika Jumuiya lakini pia yapo mengi yanahitaji kufanyika ili kuijenga UVCCM imara na inayojiendesha kitaasi zaidi kwa maslahi ya Vijana wa Taifa letu na Chama Cha Mapinduzi.

Ili kuyafikia haya yote Vijana tunataka kumpata Kiongozi ambaye ana uthubutu wa kufanya kazi kwa bidii na weledi wa hali ya juu huku akizingatia kanuni za Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Cha cha Mapinduzi.

Victoria Charles Mwanziva ni mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM ambaye amejipambanua kwa uwezo wake kiuongozi na kusimamia maslahi ya vijana, tumeshuhudia akipambana kuwakutanisha vijana na fursa mbalimbali za kitaifa na kimataifa, lakini pia tumeshuhudia akifuatilia maagizo mbalimbali ya Mhe. Rais kwenye Wizara kadhaa kuhusu fursa za vijana ili kujikwamua kiuchumi.

Victoria Charles Mwanziva ni Kiongozi aliyesheheni sifa zote za kiuongozi nilizozianisha hapo mwanzo, ana mahusiano mazuri na Vijana ambao wanakwenda kuweka Imani kwake kuwaongoza kwa kipindi cha miaka mitano ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi.

Victoria Charles Mwanziva ni kiongozi mwenye maono na amejipambanua kuwa ni mtu mwenye uwezo wa kuyatafsiri maono yake ya kuwatumikia vijana kwa vitendo.

Victoria Charles Mwanziva ni Kiongozi asiyejikweza mara zote anajishusha kuwasikiliza anaowaongoza ni mshauri kwa vijana wengi wanaohitaji ushauri kutoka kwake.

Victoria Charles Mwanziva ni kijana anayekipenda Chama cha Mapinduzi na amekitumikia kwa moyo wake wote kwa kujitoa ngazi zote Kuanzia matawini hadi ngazi ya Taifa.

Victoria Charles Mwanziva ni muunini wa Siasa za hoja na uongozi shirikishi akiamini katika umoja ili kuyafika matokeo bora na ya haraka katika Taasisi

Victoria Charles Mwanziva ni mwanamke hodari anayeamini katika uwezo kiutendaji na vipaji vya watu

Victoria Charles Mwanziva ni Dada mlezi kwa vijana wengi akitumia karama yake ya uongozi kuwalea na kuwainua wengine kukua kiuongozi.
IMG-20221118-WA0241.jpg
 
Hafai huyu mama ,my girl at UDSM back then in 2014.
Mkimchagua huyu mtajuta,mkatili ,mbinafsi,mbaguzi kujiona mzungu kisa mama yake ni anatokea kwa Putin.
Sifa mbaya zaidi ni kutotulia atawaketea kashfa ya ngono chamani.yuko tayari kutumia mwili wake kufanikisha jambo lake.
Tuliosoma nae tunamjua
 
Ina maana anasaliti ndoa yake ๐Ÿ™‚
Anaonekana down to earth
 
Ina maana anasaliti ndoa yake ๐Ÿ™‚
Anaonekana down to earth
Kwenye siasa hakuna cha down to earth. Hapo anawaza jinsi atakavyo piga hela baada ya kushinda au kutafuta ubunge au cheo baada ya kushinda ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Usijidanganye na wanasiasa. Wewe unajua chanzo chake cha mapato ni kipi? Pesa anayoitumia hapo kwenye kampeni atairudishaje? ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Jiongeze!
 
Kweli aisee hakuna linaloshindikana mwenyewe nimecomment tu kuchangamsha jukwaa ๐Ÿ˜„ kichwan tayari najua lolote linawezekana
 
๐Ÿ˜‚
Hata video zake za ig zimekaa kimtegomitego sana ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚. Na ni Full uchawa tu

Hivi mbona anaonekana mkubwa kiumri? Au ni mshibo wa kulamba asali?
Sio mkubwa kivile ana 28 au 29
Amekulia familia bora ,baba yake ni daktari alusomea urusi ndio akamuoamama yake
 
Hafai huyu mama ,my girl at UDSM back then in 2014.
Mkimchagua huyu mtajuta,mkatili ,mbinafsi,mbaguzi kujiona mzungu kisa mama yake ni anatokea kwa Putin.
Sifa mbaya zaidi ni kutotulia atawaketea kashfa ya ngono chamani.yuko tayari kutumia mwili wake kufanikisha jambo lake.
Tuliosoma nae tunamjua
Wacha fitna majungu yasiyokuwa na maana kama vile wewe ndiyo umekuwa mkamilifu. Unamsema atawaletea kashfa wenzake wakati wewe ndiyo unamkashifu.
 
Sio mkubwa kivile ana 28 au 29
Amekulia familia bora ,baba yake ni daktari alusomea urusi ndio akamuoamama yake
Aisee kumbe ni Toto la kishua. Kwa hiyo ni mambo safi na Wala hana haja ya ajiraportal ๐Ÿ˜‚

Hizo safari kibao anazosafiri kila siku na anapost mtandaoni pesa anaotoa wapi? Maana uvccm huko ni njaa tupu. Au mzee wake anampa hela? Au ana "vyanzo vya mapato" visivyojulikana?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom