Chagua moja, who wanna be

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
CHAGUA MOJA ,

Unaweza kuwa mtu mmoja tu kati ya watu hawa wawili.Huwezi kuwa wote wawili, au huwezi kuwa katikati, ni moja tu.Unaweza kuwa mtu mwema au unaweza kuwa mtu mbaya.Unaweza kuwa mchapakazi au unaweza kuwa mvivu.

Unaweza kuishi maisha ya furaha na mafanikio au unaweza kuishi maisha ya mateso na kushindwa.Na uzuri ni kwamba wewe mwenyewe ndiye unayechagua uwe mtu yupi kati ya hao.Hakuna mtu yeyote anayekuchagulia, hakuna mtu yeyote anayekulazimisha uwe mtu wa aina gani.

Ni wewe mwenyewe, kwa kujua au kutokujua, unachagua uwe mtu yupi kati ya hao.

KUPOTEZA MUDA
Kuna watu wengi wamekuwa wakipoteza muda wakifikiri wanaweza kuwa katikati, au kuwa watu wote wawili.

Yaani mbele za watu uonekane mwema, lakini ukiwa mwenyewe au ukiwa na watu fulani unawafanyia ubaya.

Ukiwa mwenyewe unatega kufanya kazi, lakini mbele za watu unataka uonekane mchapa kazi.Wewe mwenyewe ndani yako unajua maisha unayoishi siyo ya furaha, lakini nje unajionesha kama ni mtu mwenye furaha na mafanikio.

Huku ni kupoteza muda na kuchagua maisha ambayo mwisho wa siku kila mtu atajua ya kwamba uko upande upi, na mara zote upande utakaojulikana ni ule mbaya.

Amua leo ya kwamba unachagua kuwa mtu mwema, unachagua kujitoa kwenye kile unachofanya na chagua kuwa na maisha ya furaha na mafanikio. Ndio ni njia ngumu kuliko hiyo nyingine, lakini inalipa sana.
 
Umeongea vizuri, lakini kuna msemo kuwa,
No matter who tries to teach you about LIFE, you won't understand till you GO through it by YOURSELF. Kwa hiyo walioelewa hicho ulichosema ni wale waliopitia, ambao bado hawajayapitia....
 
Umeongea vizuri, lakini kuna msemo kuwa,
No matter who tries to teach you about LIFE, you won't understand till you GO through it by YOURSELF. Kwa hiyo walioelewa hicho ulichosema ni wale waliopitia, ambao bado hawajayapitia....
Asante kwa udadavuvi mzuri.
 
Back
Top Bottom