Chagua CCM.....Chagua Kikwete

Brooklyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
1,459
284
mafurikokilosa.jpg

Wakazi wa Wilaya ya kilosa Mkoani Morogoro wakijaribu kuyanusuru maisha yao baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko makubwa yaliyosababisha kuvunjika kwa nyumba wilayani humo (Source: Mwananchi 29/12/09)

Licha ya ugumu wa maisha waliyonayo watanzania toka uhuru mwaka 1961, bado wana mapenzi ya dhati na imani kubwa juu ya chama chao cha CCM kama inavyooneshwa pichani mkazi wa kilosa akijaribu kujiokoa toka kwenye mafuriko yaliyobomoa nyumba zao huku akiwa amevaa T-shirt ya CHAGUA CCM....CHAGUA KIKWETE!!
 
Mwenzio hilo ni vazi tena inawezekana ndilo la kutokea hilo. Umaskini ni mkubwa sana Bongo kiasi kwamba hata mitumba ni ghali. Sasa hizi T-shirt na khanga za SISIEM zinawaokoa kweli especially ile 70 % ya wafuata upepo.
 
Na hivyo vivazi ndio vinavyowapa kura,wakati sisi tunapigana kufa na kupona kuking'oa madarakani,wao wanapanga mikakati ya kutafuta t shirt za MANGA ili kuongeza ubora wa hivyo vivazi,tutashinda kweli ktk mtindo huu?
 
mafurikokilosa.jpg

Wakazi wa Wilaya ya kilosa Mkoani Morogoro wakijaribu kuyanusuru maisha yao baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko makubwa yaliyosababisha kuvunjika kwa nyumba wilayani humo (Source: Mwananchi 29/12/09)

Licha ya ugumu wa maisha waliyonayo watanzania toka uhuru mwaka 1961, bado wana mapenzi ya dhati na imani kubwa juu ya chama chao cha CCM kama inavyooneshwa pichani mkazi wa kilosa akijaribu kujiokoa toka kwenye mafuriko yaliyobomoa nyumba zao huku akiwa amevaa T-shirt ya CHAGUA CCM....CHAGUA KIKWETE!!

kwa staili hii mkuu tutafika kweli tunakokwenda? asante kwa kutukumbusha, hii picha ni kielelezo tosha.
 
Ni shida ya mavazi tu hiyo, na umasikin uliobobea...Hii ni uthibitisho kwamba wanasiasa wa TZ wanatakiwa kufanya matendo si saundi!
Kuna mtaalamu mmoja alipata kusema kuwa.."Hakuna maelezo ya umasikini zaidi ya MAPANYA NA MENDE"

Huko hata ukipeleka za t-shirt za CHAMA cha PakaJimmy, na ukaongezea labda na Pensi nyanya watazivaa na kunichagua fasta, NA hawatamwelewa atakayekuja na maneno matamu, hata akiwa kikwete gani!.

Umasikini ni kitu mbaya sana!
 
Bado tuna safari ndefu sana kuelekea kuwa na kizazi kitakachokuwa kinapiga kura kutokana na sifa na utendaji wa wagombea (based on merits) na sio kanga, T-shirt na pilau. Sidhani kama wananchi walio wengi (70% kama alivyosema Mh. Rais JK) wanajua maana ya Uchaguzi.

Ndio maana CCM badala ya kukaa na kutafakari mbinu mpya za kuleta maisha bora kwa kila mtanzania (mbinu zilizopo zimefeli kabisa) wanaagiza Toyota Landcruiser 150 kwa ajiri ya kubebea wapambe, kanga, kofia, TOT na T-shirt!!

Laiti kama hawa 70% wangejua maana ya kupiga kura na impact yake, basi 2010 tungeshuhudia mtikisiko wa kisiasa Tanzania!!
 
Back
Top Bottom