Chadema.

Chadema.

ferg

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2015
Posts
1,329
Reaction score
1,819
habari za muda huu mdau, nami ninayo machache ninayopenda kujadili nawe juu ya chama kikuu cha upinzani nchini mwetu.

binafsi nilianza kukifuatilia chama hiki tangu uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingu ulipoanza nchini. chadema ndio chama cha kwanza kutoa mbunge wa upinzani nchini mwetu (mwaka 1994 dr kabourou aliposhinda uchaguzi mdogo kigoma mjini baada ya mbano kufariki)

Tangu kipindi hicho tumeshuhudia chadema ikikua na kukubalika kwa kasi katika duru za siasa za nchi yetu. wapo wanasiasa mashuhuri walioibuka na kuimarishwa na chadema na ambao wamekipigania chama kwa nguvu zote, huku baadhi yao wakiondoka ndani ya chama kwa namna ambayo haipendezi(rejea dr kabourou, zitto na wengine)

kwa muda mrefu sana chadema imekuwa ikijipambanua kama chama kinachopinga ufisadi naa mafisadi wakitajwa hadharani na viongozi wa chadema. ni hawa hawa chadema walioibua na kusimamia hoja nyingi za ufisadi nchini na kupelekea mabadiliko kadhaa ya viongozi serikalini.

Ujio wa lowasa chadema umebadili taswira ya siasa za nchi yetu. kwa mara ya kwanza tutashuhudia siasa za ushindani kwenye uchaguzi wa mwaka huu.(amani itawale).

Yapo mambo kadhaa yananitatiza.
Mosi, chadema imesahau damu na jasho la watanzania lilivuja na kumwagika wakati tukipinga ufisadi?,
mbona walipokuwa wanamshambulia lowassa hawakusema kuwa ufisadi wake unatokana na mfumo wa ccm?
iwapo lowassa atashindwa kwenye uchaguzi (inawezekana) ataendelea kuwa mwanachama mtiifu wa cdm?

Pili, tetesi juu ya dr Slaa si za kupuuzwa. wengi wameanza kumbeza na kumtukana huku wakisahau kuwa amekipigania chama tangu alipokuwa mbunge kwa mara ya kwanza. wengine wanasema kuwa amesusa kisa uroho wa madaraka. mimi ninapinga, amesusa kwa sababu dhamiri inamshutumu kwa kile anachokiamini.
Nashauri cdm wamalize tofauti zao na dr Slaa arudi kundini. huyu ni kada na mpambanaji wa kweli. Na gharama ya kumpoteza ni kubwa kuliko tunavyodhani

Tatu, iwapo Lowassa na chadema watashindwa kwenye uchaguzi basi wananchi watapunguza imani kwa chama. mlituaminisha lowasaa ni fisadi lakini leo mnamsafisha, maana yake kauli na matamko yenu si ya kuaminiwa tena. mnaweza kutoa tamko na baadae mkalikana. (mnatugeuza kama chapati)
Pia hii inaonesha hata wale mliowaita wasaliti, haikuwa kweli na ipo siku mtatuambia hawakuwa wasaliti kama mlivyofanya kwa lowassa.

Naomba niwashauri wanachama na wapenxi wa vyama vya siasa. si kila tamko linalosemwa na kiongozi wa siasa ni lakuaminika, usimtusi mtu kisa kiongozi wako kamtuhumu.

Naomba niache swali. Iwapo dr Slaa ataondoka chadema, ataitwa msaliti kama waliowahi kuondoka?
Wasalamu
 
...makala ndeeefu lakini yoote ni maroroso tupu,kama mfuatiliaji wa makala za jf utagundua hoja zako karibia zoote zimejadiliwa na majibu mujarabu yameshatolewa...
 
...makala ndeeefu lakini yoote ni maroroso tupu,kama mfuatiliaji wa makala za jf utagundua hoja zako karibia zoote zimejadiliwa na majibu mujarabu yameshatolewa...

ahsante kwa mchango wako,
 
Vipi kama Lowassa akishinda baba! Naona unazungumzia akishindwa tu.
Halafu mbona yeye mwenyewe Lowassa halalamiki kwamba CDM walimchafua, mnalalamika nyinyi wengine?
Kweli Lowassa amewatikisa nyinyi CCM.
 
usidhani kila mtu ni ccm.
kama lowassa akishinda itakuwa tofauti na nilivyoeleza
ahsante
 
Unapochambua kitu unapaswa uchambue kwa mapana. Umetumia muda mrefu ukielezea upande wa kushindwa tu.
Ndiyo maana nikakuuliza hilo swali. Samahani kwa kukuita CCM wakati kumbe siyo kwani wengi wenye kutoa hoja kama hizo ni CCM.
Tanzania yetu ndiyo nchi ya FURAHA pote ulimwenguni watu wote watambu, Tanzania yetu ndiyo nchi ya FURAHA.
Naye baba ndiye wetu muhisani, yeye ndiye aliyeleta Uhuru, Tanzania yetu ndiyo nchi ya FURAHA...
NAUPENDA SANA WIMBO HUU.
 
niliingalia zaidi chadema kwani ndio ambao wako kwenye risk if they lose election. ukitakari kwa upande huo utaona ninachoona.
pia angalia mpasuko uliopo chadema
 
Lengo la #UKAWA ni kuipeleka ccm alipokwenda #Komba hakuna njia nyingine lazima ccm iondoke lakini mimi naamini #Lowasa ana nguvu kubwa sana lakini #Lowasa hatawezi kushinda uraisi bila sapoti na nguvu #Dr .Slaa bado kuna haja kubwa sana viongozi wa #UKAWA kutambua mchango mkubwa #Dr .Slaa ndani ya chama na taifa kwa ujumla ukimya wa #Dr .Slaa umetukwanza na kutuweka njia panda watu wengi sana tumeambiwa kesho Dr.#Slaa atashiriki kwenye vikao vya kamati kuu ya #CHADEMA tunamsubiri kwa hamu sana kumsikia na kumwona .
 
uko sahihi kabisa Emma, ndio maana nimesema wayamalize mapema kabla dr Slaa hajaamua kinyume na madhumuni ya ukawa
 
Back
Top Bottom