CHADEMA Z'bar kuitisha maandamano kudai umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA Z'bar kuitisha maandamano kudai umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee wa Kale, Dec 29, 2009.

 1. M

  Mzee wa Kale Member

  #1
  Dec 29, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Mwinyi Sadallah,

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar, kimeitisha maandamano makubwa kushinikiza viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ) warejeshe huduma ya umeme haraka au watangaze kujiuzulu, kabla ya maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, mwakani.
  Tamko hilo lilitolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Hamad Mussa Yussuph, alipokuwa akizungumzia athari za kukosekana umeme kwa wananchi wa visiwa vya Zanzibar.
  Alisema juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Zanzibar tangu kukosekana kwa umeme Desemba 10, mwaka huu, haziridhishi na wananchi wamekuwa wakiambulia ahadi hewa.
  Alisema maandamano hayo yataanzia katika viwanja vya Maisara mjini Unguja na kumalizia katika viwanja vya Kibandamaiti mjini Unguja, ambapo pia wataalikwa wawakilishi wa asasi zisizokuwa za kiserikali na vyama vya siasa.
  Alisema maandamano hayo yatafanyika Januari 10, mwaka huu ikiwa ni siku mbili kabla ya maadhimisho ya Mapinduzi Zanzibar.
  “Tunataka hadi Januari 12, mwaka huu umeme uwe umerejea Zanzibar au viongozi wawe wamewajibika kwa kushindwa kuwatumikia wananchi kama walivyoahidi”, alisema.
  Kukosekana kwa umeme kumesababisha matumizi makubwa ya jenereta, ambapo tayari yameanza kuleta athari baada ya mtu mmoja, Mahmuni Ali Abdallah, kulipukiwa na jenereta na kujeruhiwa vibaya na kulazimika kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
  Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma, alisema siyo kweli kwamba serikali haichukui hatua, lakini juhudi mbalimbali zinachukuliwa hivi sasa kutatua tatizo hilo.
  Alisema hivi sasa serikali imeweka mipango ya muda mfupi na mrefu ili kuhakikisha huduma hiyo inapatikana haraka iwezekanavyo na kupunguza athari kwa wananchi.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,765
  Trophy Points: 280
  chadema tanganyika haitahusika...???
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Vipi kama wangalisema Chadema Mwanza ama Shinyanya ungalitoa maoni gani hapo napo kama hapa unadai Tanganyika ?
   
 4. M

  Mzee wa Kale Member

  #4
  Dec 29, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu nadhani mngejikita kwenye hoja iliyopo mezani, Wakati wazanzibari wanaishi katika maisha ya tabu, CHADEMA kama chama wanayo haki ya kusimama na kudai uwajibikaji kwa Viongozi wao, tuanakumbuka tatizo kama hili lilipotokea Serikali ndani ya BAraza la Wawakilishi walitoa ahadi kwa wananchi na kusema kwamba halitotokea tena na kuwa historia hivyo kwa kuwa limetokea na kupiga msumari wa moto kwenye kidonda ni wazi naungana na CHADEMA kudai uwajibikaji.

  Tunakumbuka wametumia 3 Bilion kwa ajili ya kununua magari ya kifahari kwa viongozi, yapo majenereta 15 yaliyotolewa msaada na UNICEF lilipotokea tatizo hili mara ya kwanza sasa yameishia mikononi mwa baadhi ya mawaziri na kuwekwa kwenye hoteli zao za kitalii.

  Tutaungana nao tupo pamoja tutashiriki na kujitokeza kwa wingi CHADEMA mwendo mdundo.
   
 5. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  wajitahidi kujinadi, maana chadema haina watu zanzibar.

  na kwa huu muundo wao wa ukabila ndio kabisa wasitegemee kitu
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Tuwekee hapa muundo wa ukabila na tukiwa tuna endelea na kujikita katika hoja .Nimeomba hili ili kuonoa uongo ambao unapelekea hoja kuachwa ina elea .
   
 7. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280

  Wanadamganywa na propaganda za CCM wanakubali.
   
 8. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,765
  Trophy Points: 280
  Hata hapo ningeuliza tuu......... mimi nilidhani ni msimamo wa chama........ Hivyo walivyoamua itaonekana ni msismamo wa wanachadema walioko zenji..........
   
 9. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  .
  Inaonekana jina Tanganyika
  Halitakiwi tena! Tuitejae?
   
 10. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Tanganyika huweka viongozi wasiotakiwa na wazanzibari halafu sasa ati wawajibike, hawana uwezo wa kuongoza hao walioko madarakani wote wameingia kinyume na demokrasia.Sasa wakishindwa kazi na kulaza watu gizani kuna lipi la ajabu?

  Hata ile moto ya kuandamana wazenji hawana, maana viongozi wote ni watu wasiotakiwa!
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Dec 29, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,021
  Trophy Points: 280
  ..Zenj inategemea umeme toka Tanganyika.

  ..tena wanauziwa kwa bei nafuu kuliko Watanganyika wenyewe.

  ..kwanini hamuandamani Watanganyika tupate umeme wa uhakika?
   
 12. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwa chadema kufanya hivyo zanzibar ni sawa...kisiasa kwakuwa sasa upinzani zanzibar uko kwenye mkataba na ccm,l abda watapata wafuasi kadhaa...ila asiende askofu Slaa atawatibua wazenj...

  Inaweza kusaidia wale wazanzibar ambao si CUF wala CCM kutoa maoni yao

  wangeweza kuwashawisha CUF wawaunge mkono wangeenda one extra mile..though hiyo kutokea ni very remote.
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Dec 30, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Maandamano ni tarehe 10 yenye nia ya kushinikiza hatua tarehe 12...! Kazi ipo!
   
 14. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #14
  Dec 30, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hapo naona upo kwenye zile philosophy za kuonesha kama Zanzibar ni inferior kwa Tanganyika kwa kutumia hoja ya umeme.

  Zanzibar inanunua umeme, na inategemea na mkataba unavyosema.Kama mkataba utasema ongezeko la bei lisizidi 5% per year, wakati Tanganyika hakuna mkataba huo.?Tunaweza kuambulia Zanzibar kupata umeme rahisi kushinda bara!

  Shortly, umeme wenu kuuza Zanzibar sio kama ndio mmeshika mpini.Ziko njia nyingi za kutafuta umeme, na Zanzibar ilipata umeme mwanzo kushinda Tanganyika hio ni historia nakudokezea.

  Upande wa pili wameshakuja wawekezaji wengi wa umeme Zanzibar, na SMZ imewatimua kulinda soko la Tanesco.Kwa hiyo acheni kejeli za kuifanya Zanzibar kama ni mzigo kwa Tanganyika, hii dhana ni potofu na hatari kwa muungano mzima wa Tanzania.
   
 15. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #15
  Dec 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kazi nzuri sana Chadema na wanafanya vizuri sana sana
   
Loading...