CHADEMA yazidi kusisitiza kwamba Wakuu wa Wilaya hawatakiwi Nchini Tanzania maana hawana kazi yoyote

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,723
218,285
Akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara huko Sengerema , Mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema , Ezekia Wenje amesema kwamba kila Wilaya nchini Tanzania ina DSO mwenye mafunzo yote na ina OCD mwenye mafunzo yote , lakini eti wanaletewa DC asiyejua lolote kuwa Boss wao, Wenje amedai kwamba ndio maana Chadema inataka Katiba Mpya ili pamoja na mambo mengine hawa Wakuu wa Wilaya waondolewe maana zaidi ya kulinda ccm hawana kazi nyingine yoyote ya maana.

Labda kwa wale ambao hawajui majukumu halisi na ya kweli ya Mkuu wa Wilaya , ukiacha yale ya uongo yanayotajwa ya kwamba eti DC ndio Mkuu wa ulinzi na Usalama wa Wilaya , Kazi halisi ya DC chini ya ccm ni hii hapa .

1. Kutetea Maslahi ya ccm kufa na kupona ikiwemo Wizi wa kura kuiba masanduku na kuhujumu vyama vya upinzani ikiwemo kuwateka viongozi wake (kama Sabaya , Jerry Muro nk)

2. Kufungua mikutano mbalimbali ikiwemo makongamano ya Ukimwi na Malaria

3. Kupokea na kuwakirimu viongozi wa kitaifa na wa ccm wanaotembelea Wilaya yake .

4. Kusimamia kikamilifu mbio za mwenge kwenye wilaya yake

5. Kusimamia kampeni ya kutokomeza Kipindupindu na kuhamasisha chanjo ya Polio pamoja na kusimamia usambazaji wa Dawa za Mabusha na Matende .

Kuna haja gani ya kuwa na Mtu maalum wa mambo mepesi kama haya wakati kuna Mganga Mkuu, DED, AFISA USALAMA na MKUU WA POLISI ?
 
Hawa chagadema wamechanganyikiwa. Mwisho watasema hamna haja ya kuwepo katekista kwa sababu padre yupo au watasema hakuna haja ya kuwepo padre kwa sababu askofu yupo au watasema hakuna haja ya kuwepo maaskofu kwa sababu maasko wakuu wapo au hankuna haja ya kuwepo maaskofu wakuu kwa sababu makadinari wapo au hakuna haja ya kuwa na makadinari kwa sababu papa yupo. Au watasema hakuna haja ya kuwa na msiongori kwa sababu vica generals wapo. Au hakuna haja ya kuwa na abate kwa sababu askofu yupo.

Hivi chadema Kuna mtu ameenda shule kweli au wanaongozwa na mizuka tu.
 
Hawa chagadema wamechanganyikiwa. Mwisho watasema hamna haja ya kuwepo katekista kwa sababu padre yupo au watasema hakuna haja ya kuwepo padre kwa sababu askofu yupo au watasema hakuna haja ya kuwepo maaskofu kwa sababu maasko wakuu wapo au hankuna haja ya kuwepo maaskofu wakuu kwa sababu makadinari wapo au hakuna haja ya kuwa na makadinari kwa sababu papa yupo. Au watasema hakuna haja ya kuwa na msiongori kwa sababu vica generals wapo. Au hakuna haja ya kuwa na abate kwa sababu askofu yupo.

Hivi chadema Kuna mtu ameenda shule kweli au wanaongozwa na mizuka tu
Haya ni yako
 
Wakimalizana na wakuu wa wilaya wataanza wakuu wa mikoa, wakurugenzi, makatibu wakuu, manaibu mawaziri na mwishowe mawaziri.

Hao chafema ni wa kupuuzwa maana huwa hawajui wanataka nini.

Hapo wanaongea kwa experience ya yule bwana alivyomnyoosha Mbowe kule Hai.
 
Chadema ni kama CCM tu, hata kimuundo, Chadema nao Wana muundo wa "Kamati Kuu", hawa kwa asilimia 100 ni kama CCM tu
 
Back
Top Bottom