CHADEMA yazidi kung'aa Bukoba Mjini

CHADEMA yazidi kung'aa Bukoba Mjini

Asante sana kamanda , hata TEMEKE cdm inasonga mbele kwa kasi mno , keko machungwa , keko mwanga , kurasini , keko juu ccm kwisha kazi .
 
Good job! tunawapongeza....waonesheni nguvu ya cdm nje ya bunge. Maana huko wametukana watanzania kwa kupitisha sheria hovyo.
 
Naelewa sana moto unaowaka hapo kwa sahivi kijani lazima wahame tu.
 
Asante sana kamanda , hata TEMEKE cdm inasonga mbele kwa kasi mno , keko machungwa , keko mwanga , kurasini , keko juu ccm kwisha kazi .

Mtajiliwaza kwa mambo ambayo ukweli wake unaonekana. Wabunge wenyewe ambao ndiyo viongozi wakuu wa CHADEMA wanataka kutoana macho kwa sababu ya sitting allowance.
Lissu awalaumu viongozi wa Chadema Dar

Dar es Salaam. Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, amewaponda viongozi wa Chadema mkoani Dar es Salaam kuwa wameshindwa kufanya kazi za siasa za kukijenga chama hicho.

Lissu amesema viongozi hao wamekuwa wakitumia muda mwingi kukiponda chama tawala, badala ya kutumia nguvu kubwa kukipigania chama chao.

Aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara, uliofanyika katika Jimbo la Segerea, mkutano ambao ulihudhuriwa na idadi ndogo ya wanachama.

Kwa mujibu wa Lissu, idadi ya wanachama aliowakuta katika Jimbo la Segerea ni ndogo kuliko ya kijiji kimoja cha Jimbo la Singida Mashariki.

Alisema idadi ndogo ya wanachama katika mkutano huo, ni ishara kwamba viongozi wa Chadema mkoani Dar es Salaam, wameshindwa kufanya kazi za siasa.

Alisema viashiria kwamba viongozi wa Chadema, mkoani humo hawafanyi kazi za siasa, vinadhihirishwa na hali katika majimbo ya uchaguzi.

“Dar es Salaam ndiyo moyo wa Tanzania, ni jiji linalotakiwa kutegemewa sana kisiasa, lakini cha kushangaza inapata wabunge wawili wa upinzani, inakuwa nyuma na mikoa ya Shinyanga na Kigoma, hii ni aibu,” alisema Lissu.

“Wilaya ya Ilala ina madiwani wawili tu wa upinzani, viongozi wa Chadema wapo na wameridhika wanaona hilo ni jambo la kawaida, tutaboresha vipi maisha ya wananchi kwa kuwa na madiwani wawili,” alisisitiza Lissu.

Alisema mageuzi yoyote makubwa ambayo yamewahi kutokea katika nchi mbalimbali, yalianzia katika miji mikubwa kama Dar es Salaam.

“ Mageuzi hayaji kwa kulalamika kwamba CCM wametuibia kura, wakati wanaiba kura nyinyi mlikuwa wapi, hiyo inaonyesha kwamba hamfanyi kazi ipasavyo,” alisema Lissu.

Alisema malalamiko ya kuibiwa kura hayana msingi katika kipindi hiki kwa sababu kama CCM wanatuhumiwa kuiba kura kwa nini walishindwa kufanya hivyo katika majimbo ya Ubungo, Kawe na Singida Mashariki.

Lissu alisema viongozi wa Chadema wanapaswa kubadilika na kufanya kazi za siasa kama kweli wanataka mabadiliko mwaka 2015 na kwamba vinginevyo, wataendelea kulalamika.

Lissu awalaumu viongozi wa Chadema Dar - Habari - mwananchi.co.tz
 
Kufikia 2014 October kila palipo na balozi wa ccm kuna balozi wa chadema
Huu ndiyo ukweli.
CHADEMA kipo kwenye ulingo wa kisiasa kuanzia 1992 ambapo ni miaka kama 21 kwa sasa ambapo hakina hata mabalozi to match CCM halafu unaongelea miezi ndiyo wataweza kufanya kazi hiyo. You must be joking.

Sitting allowance kwa viongozi wenu wa kitaifa zinataka kuwatoa macho. Uchaguzi wa ndani ya CHADEMA, viongozi wanaogopa kuufanya. Mtaweza kupambana na mazingira na mtandao wa CCM nchini?.

Fikra zako ni placebo ya kisiasa.
 
Naona Mwanadiwani unaumia macho kila ukisoma neno CDM ...mtakaa sana,CDM ni baba lao iwe masika,kiangazi ama vuli CDM haitamwacha yeyote mpaka akina mkubali.
 
Lema anakiua chama nyie mko hapa mnafarijiana.
Poleni misukule.
 
Hii habari kuna watu wanaipokea vibaya utafikiri wapokea taarifa ya msiba.Ni uzembe tu kukataa ushauri wa Mkiti wenu kuwa muanze kujiandaa kisaikolojia CCM itakapo kuwa chama kidogo cha upinzani.Asante sana makamanda kwa kazi nzuri
 
Sehemu ambapo kiwango cha elimu ni kikubwa kama Bukoba inabidi ccm itokomezwe kabisa!

CDM Kagera tunawategemea mpate ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Hongereni kwa kazi nzuri. Hizi bila shaka ni rasharasha, tunasubiri mvua zenyewe mwakani. Our prayers are with you!

nimeipenda hii comment nzuri, wahaya bhana kiboko, kagasheki wanamtreat kama mbunge alopora kura zao na kupata ubunge ivo hawampi ushirikiano kabisa.
 
Lema anakiua chama nyie mko hapa mnafarijiana.
Poleni misukule.

ah ah, nimebaini kumbe ccm mpo pia?? hii habari lzm iwaume.

ivi wakumbuka jk kasema: ccm kwa rushwa ilivokua juu 2015 mjiandae kushindwa vibaya, na ninavowajua kwa rushwa hamtaacha
 
Huu ndiyo ukweli.
CHADEMA kipo kwenye ulingo wa kisiasa kuanzia 1992 ambapo ni miaka kama 21 kwa sasa ambapo hakina hata mabalozi to match CCM halafu unaongelea miezi ndiyo wataweza kufanya kazi hiyo. You must be joking.

Sitting allowance kwa viongozi wenu wa kitaifa zinataka kuwatoa macho. Uchaguzi wa ndani ya CHADEMA, viongozi wanaogopa kuufanya. Mtaweza kupambana na mazingira na mtandao wa CCM nchini?.

Fikra zako ni placebo ya kisiasa.

masikini unachangia kwa kuwa ndo ushapewa buku7 na mwigulu then utafanyaje lzm uandike kitu kibaya angalau dhidi ya chadema, japo aujiulizi hao wa kitendagulo uko bukoba wamechukia nini ccm au hawajazielewa propaganda zenu?

ivi wajua wanaofanya grand corruption kt nchi hii ni akina nani? wajua wahasisi wa richmond, epa, bot tower, majority ni makada wa chama chako, na mnadhani watanznia hatjui ilo? ng'ang'aneni na chadema mkihisi itawarudishieni imani kwa watanzania japo aitawasaidia
 
Huu ndiyo ukweli.
CHADEMA kipo kwenye ulingo wa kisiasa kuanzia 1992 ambapo ni miaka kama 21 kwa sasa ambapo hakina hata mabalozi to match CCM halafu unaongelea miezi ndiyo wataweza kufanya kazi hiyo. You must be joking.

Sitting allowance kwa viongozi wenu wa kitaifa zinataka kuwatoa macho. Uchaguzi wa ndani ya CHADEMA, viongozi wanaogopa kuufanya. Mtaweza kupambana na mazingira na mtandao wa CCM nchini?.

Fikra zako ni placebo ya kisiasa.

Dogo, nawe unaongea propaganda tu. Kiukweli, ccm ishachokwa.

CCM ni chama mfu, labda kama ulivyo wewe na fikra mfu. Take care idiotum.
 
Back
Top Bottom