CHADEMA imeanza mwaka 2013 pasipo mashiko wala dira ya waendako. Hali hii ni faida kwa watanzania kwa vile imetupa fursa ya kupata kutambua uwezo wa viongozi wa CHADEMA kuhusiana na maendeleo ya nchi yetu.
Leo ni siku ya tano, Januari 2013 viongozi wao wamekuja na kauli zinazothibitisha ufinyu na uwezo mdogo waliokuwa nao;-
1. Kamati ya Utendaji CHADEMA iliirukia HUTOBA ya Rais JK kuwa amefanya kosa kutoa ratiba ya mchakato wa kuelekea KATIBA MPYA; leo wameumbuliwa na Jaji Warioba.
2. Mbowe katoa kauli ya kumuunga mkono Dr.Slaa kuwa mgombea wa Urais kupitia chama chao 2015; kauli ambayo imethibitisha ukosefu wa demokrasia ndani ya chama chao pamoja na kuwepo kwa mwenyekiti asiyejua mipaka ya kutoa kauli.
3. Leo Kikao cha BAVICHA kimekuja na fungua mwaka ya KUUNGA MKONO Madai ya Watu wa Mtwara yanayoonyesha kuvunja UTAIFA;
Hiki chama hakina muono wa mbali badala yake wamekuwa hodari wa kurukia hoja kila kukicha!